Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Baadhi ya wagombea Urais na Ubunge wamekwishapewa advance ya kuuza nchi

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Maneno haya kayasema leo singida mjini wakati akitambulishwa na mgombea urais wa CCM Dr John Pombe Magufuli alipokuwa akiomba kura ili apate ridhaa mara ya pili kuitumikia nchi.

Katika matamshi yake ummati ulilipuka kwa shangwe huku ukisapoti asemayo Mwigulu Nchemba.

Wanasingida wameahidi kuipa ccm kura zote za ndio kwa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani.

Wamesema chama cha wajanja janja (CHADEMA),kitaisoma namba.

Je, kuna ukweli wowote katika matamshi yake?

Tujadili hoja yake kama ina ukweli na si kumjadili mleta hoja (Mwigulu)personal

Karibuni wanajukwaa
 
Wewe na Mwigulu wote mnafanana akili (kama mnazo lakini).

Kwa mtu ambaye kakaa darasani muda mrefu sikutegemea kama angekuwa mropokaji, azungumze vitu bila ushahidi na kama anao ushahidi basi auweke hadharani.

Tunatukanwa sana wanaCcm kila kona kwa sababu ya wapuuzi wachache ambao hawawezi kuacha nguvu ya hoja ikafanya kazi na badala yake kutegemea hoja ya nguvu, shame on you and the likes!!!

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
 
Unazarauliwa hivi na bado unavotia ccm.
Wanatuona wajinga, wanatupa information za uongo hata mbwa wake hawezi mdanganya hivi.
 
Ahadi yake ile Migulu kuwa CHADEMA itakufa kabla ya 2015 anaikumbuka?


Hicho kibabu chenu kitafute kazi nyingine ya kufanya Urais tutampa Mtanzania mwenzetu mzalendo wa kweli.Ninyi si huwa mnasema watu Wajiajiri?

Hicho kibabu chenu hakijapata tuu mtaji?Kinaogopa nini kwenda kujiajiri? Huyo babu alitwambia alijaribu tuu kuomba Urais akasukuziwamo humo humo na matokeo yake yakawa raia kuuwa, kutekwa, ukatili wa kutisha dhidi ya binaadamu na kubinywa kwa uhuru.

Hicho kibabu kitulie kilee wajukuu hakina jipya ni kishamba sana. Kisubirie kuitwa I.C.C.
Uonevu sasa baathi.
 
Ahsante kwa kutukaribisha ndugu yangu. Kwangu mimi hizi mbinu za kuwaita watu wenye mawazo tofauti na uongozi vibaraka wa mabeberu na kuwa wameuza nchi, zilitumiwa sana na viongozi wa nchi za Afrika kwenye miaka ya 1965 mpaka 1980.


Kipindi hicho kiongozi yoyote mwenye maoni na maono tofauti na watawala wa kiafrika aliitwa kibaraka wa mabeberu. Matokeo yake watawala waliwaua watu wengi na wengine wakakimbilia uhamishoni.

Lakini mpaka sasa Afrika ndiyo hii unavyoiona bado iko nyuma hata bajeti zetu zinatushinda. Viongozi wengi wa kiafrika sasa hivi wameshagundua watawala wa wakati ule walifanya makosa na walitumia mbinu ya ukibaraka ili tu kuficha udhaifu na kushindwa kwao.

Inasikitisha kuona sisi bado viongozi wetu wanatumia hii mbinu ya kizamani kabisa. Nakuhakikishia kuwa tunarudishwa nyuma badala ya kwenda mbele.
 
Wewe na Mwigulu wote mnafanana akili (kama mnazo lakini).

Kwa mtu ambaye kakaa darasani muda mrefu sikutegemea kama angekuwa mropokaji, azungumze vitu bila ushahidi na kama anao ushahidi basi auweke hadharani.

Tunatukanwa sana wanaCcm kila kona kwa sababu ya wapuuzi wachache ambao hawawezi kuacha nguvu ya hoja ikafanya kazi na badala yake kutegemea hoja ya nguvu, shame on you and the likes!!!

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
Chadema pamoja na tuhama zenu zote za Kijinga mmewahi kuweka ushahidi hadharani ?
 
Back
Top Bottom