Mwigulu Nchemba auvuruga upinzani Morogoro. Awaasa wananchi kuachana na viongozi wabaguzi, wabinafsi

Ulishawahi kumpa kura Lipumba akakulaghai !? UNAMAWAZO MGANDO TENA YAKUAMBIWA. Mlaghai na mshenzi ni yule tunaempa kura zetu then anaishia kutukandamiza na kutuibia hatuna sababu ya kuita vyama vingine vya ulaghai

By principle siasa ni ulaghai, with no exceptions.
 
Kwa mfano, akija Lipumba Morogoro akapata wasikilizaji wake wengi tu, basi hapo tayari AMEIVURUGA CCM, au CHADEMA? Neno lililotumika siyo sahihi kwa muktadha huo.
 
Watajaribu lakini hawataweza mwigulu ni mwanasiasa anayejua anachokifanya katika kuwatumikia watanzania.

kasoro jimboni kwake tu kashindwa kutatua kero za wapiga kura kama vile maji,barabara afya nk.tofauti na sugu kwake maji kila kona barabara kila chocho .kumbuka charity begins at home.
 
Kama katika mikutano CCM wing wa watu si hoja kwa nini yanatumika mpaka malori kusomba watu toka sehemu mbalimbali ili kuhudhuria mikutano?(ushahidi ni mwingi mno)
Juzi tumeonyeshwa nyama zikichomwa SAUT na aliyetoa ngo'ombe ni kiongozi wa CCM,nia yake ilkuwa nini kama sio kupata maximum attendance kwenye mikutano yake?
Nimeandika nilichokiona kuwa na ilkuwa busara upinge hoja kwa hoja,je eneo ni tofauti na nililoandika,boundaries nilizoeleza ni tofauti na hali halisi,as simpl as that then tunaendelea kujadiliana.
Hata hivyo,Good morning!

Mkuu juzi nyama zilichomwa SAUT kwenye promotion ya "Airtel UNI 255" usijechanganya na siasa.Inaonekana una hasira sana na CCM.
 
10373748_257515377784031_4207639000960800927_n.jpg

10354938_257515181117384_2114189522674244736_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba akiwasili Viwanja vya Fire Mjini Morogoro kwa ajili ya Mkutano wa Hadhara.
10364067_257521834450052_1645358639771839629_n.jpg

10441376_257521804450055_2083361314415593058_n.jpg

10390513_257515171117385_3853575915649676680_n.jpg

Umati wa wananchi kwenye mkutano
10425116_257515611117341_2554898552966715760_n.jpg

10437429_257515594450676_7410177323600367412_n.jpg

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, wakitoa burudani katika mkutano.
10394586_257515127784056_2860286074744922326_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba akihutubia umati wa wananchi Katika mwenedelezo wa Mikutano ya CCM kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Mchakato wa Katiba Mpya na Kujipanga kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba amewataka wananchi na wakazi wa Mkoa wa Morogoro kujiandaa na uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa nchini ili waweze kuwachagua viongozi watakaoendelea kutekeleza sera na Ilani ya Uchaguzi wa CCM kama inavyoendelea kutekelezwa nchi nzima kwa sasa.
10388136_257515441117358_5624545377277498264_n.jpg

Mwigulu Nchemba akifurahia jambo na Mbunge wa Morogoro Vijijini kwenye Mkutano huo
10388086_257521697783399_1167165729248483950_n.jpg

Mwenyekiti wa vijana wa wilaya ya Morogoro Mjini akisema machache na kuwasalimia wananchi
10314035_257521764450059_8875052421158788255_n.jpg

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mzumbe akizungumza kuhusu Ubora wa muundo wa Serikali mbili na namna yeye na Wasomi wengine Nchini wamepanga kuhakikisha Serikali mbili zinapita kwenye katiba Mpya itakapofika hatua ya Kura ya maoni ya Wananchi.
10464317_257521757783393_8922937963484951502_n.jpg

Katibu wa Mkoa wa Vyuo Vikuu Nchini, Ndugu Ndubi Hagai akishangiliwa na wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi kutoka Vyuo vya Mzumbe,SUA n.k
10342889_257521704450065_1989884167855255186_n.jpg

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris akiwasalimia wananchi.
10462465_257521761116726_2760389045629854801_n.jpg

Mbunge wa Morogoro Mjini, Mh. Abdulaziz Abood akiwashukuru Wananchi wake kwa Kumuunga mkono kwenye Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na amesisitiza Morogoro ni Ngome ya CCM kutokana na kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi inavyofanikiwa na kwa maana hiyo, kamwe Jimbo la haitakwenda Upinzani.
10460780_257515327784036_5364424900293531326_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu (Bara), Nchemba akiwaaga wananchi baada ya mkutano kumalizika.

mnàtumia vibaya neno"wananchi" yaani watu wapo kumi unasema wànanchi,kwani ungesema wanachama ungekufa?
 
Ndugu, naona umepita sehemu ambayo siyo. CCM haina sera za uwingi wa watu kwenye mikutano yake.

Wewe umeweza kwenda kwenye mkutano halafu unakuja hapa kuanza kusema watu walikuwa ni wachache. Wewe kilikuvutia nini mpaka ukaenda kwenye mkutano wa watu wachache ambao wengine hawakuvutiwa na kile kilichokupeleka.

Kupambana na ukweli na kushinda kunahitaji ujasili ambao haupo kwa binadamu walioko hapa duniani.

Pamoja na kwmba wewe ni gamba,nimependa comment yako.Wingi wa watu si hoja.
 
Mkuu juzi nyama zilichomwa SAUT kwenye promotion ya "Airtel UNI 255" usijechanganya na siasa.Inaonekana una hasira sana na CCM.
CCM ni chama changu ila nataka kichapwe kiboko ili kkiweze ku deliver what is expected.
Unawajua sharehlder wa Airtel?
 
10373748_257515377784031_4207639000960800927_n.jpg

10354938_257515181117384_2114189522674244736_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba akiwasili Viwanja vya Fire Mjini Morogoro kwa ajili ya Mkutano wa Hadhara.
10364067_257521834450052_1645358639771839629_n.jpg

10441376_257521804450055_2083361314415593058_n.jpg

10390513_257515171117385_3853575915649676680_n.jpg

Umati wa wananchi kwenye mkutano
10425116_257515611117341_2554898552966715760_n.jpg

10437429_257515594450676_7410177323600367412_n.jpg

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, wakitoa burudani katika mkutano.
10394586_257515127784056_2860286074744922326_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba akihutubia umati wa wananchi Katika mwenedelezo wa Mikutano ya CCM kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Mchakato wa Katiba Mpya na Kujipanga kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba amewataka wananchi na wakazi wa Mkoa wa Morogoro kujiandaa na uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa nchini ili waweze kuwachagua viongozi watakaoendelea kutekeleza sera na Ilani ya Uchaguzi wa CCM kama inavyoendelea kutekelezwa nchi nzima kwa sasa.
10388136_257515441117358_5624545377277498264_n.jpg

Mwigulu Nchemba akifurahia jambo na Mbunge wa Morogoro Vijijini kwenye Mkutano huo
10388086_257521697783399_1167165729248483950_n.jpg

Mwenyekiti wa vijana wa wilaya ya Morogoro Mjini akisema machache na kuwasalimia wananchi
10314035_257521764450059_8875052421158788255_n.jpg

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mzumbe akizungumza kuhusu Ubora wa muundo wa Serikali mbili na namna yeye na Wasomi wengine Nchini wamepanga kuhakikisha Serikali mbili zinapita kwenye katiba Mpya itakapofika hatua ya Kura ya maoni ya Wananchi.
10464317_257521757783393_8922937963484951502_n.jpg

Katibu wa Mkoa wa Vyuo Vikuu Nchini, Ndugu Ndubi Hagai akishangiliwa na wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi kutoka Vyuo vya Mzumbe,SUA n.k
10342889_257521704450065_1989884167855255186_n.jpg

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris akiwasalimia wananchi.
10462465_257521761116726_2760389045629854801_n.jpg

Mbunge wa Morogoro Mjini, Mh. Abdulaziz Abood akiwashukuru Wananchi wake kwa Kumuunga mkono kwenye Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na amesisitiza Morogoro ni Ngome ya CCM kutokana na kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi inavyofanikiwa na kwa maana hiyo, kamwe Jimbo la haitakwenda Upinzani.
10460780_257515327784036_5364424900293531326_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu (Bara), Nchemba akiwaaga wananchi baada ya mkutano kumalizika.

Hii ndio tofauti ya CCM na vyama vya kitapeli.
 
Jana nilikuwepo.Ulikuwa ni mkutano mdogo mno.
Mnaojua morogoro,mkutani ulikuwa kwenye enro opposite na fire station ktk kona ya kwenda tumbaku ukitokea masika.Palikuwa na soko upande wa magharibi.Picha zimepigwa kimkakati

Ok! Watu walikuwa kidogo. Je jiulize, mna madiwani wangapi morogoro mjini? Mna wabunge wangapi mkoa mzima wa morogoro? Angalizo tu.!
Binafsi mimi ni mwanachama hai wa CCM ila kila mkutano uwe wa CDM,CUF na CCM huwa nahudhulia. Na tupo wengi tu wa nanma hii.
 
Hizo ni parapanda tu zinapigwa! Kwanza kofia mbili zinamfanya asijue aongee nini na kwa wakati gani.

Wenye uwezo wa kufikiri miaka 50 chini ya CCM maisha bora ya mTZ yanazidi kudidimia ndio tunaambiwa tuichague CCM itatuletea maendeleo? Kwani huko nyuma kiliwanyima nini kutuboreshea maisha yetu? Sasa hivi wamepata nini cha ziada? wakati wanauza gesi yetu, tembo na twiga wetu, madini yetu pasenti wanazopata wanaficha Uswisi huku machinga ni kufukuzwa kila siku mijini!

Dini la laki sita kwa kila mTZ mbona Mwigulu hawaambii wananchi?
 
  • Naibu katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi
  • Naibu Waziri wa fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Si nilisikia kwamba mtumishi wa Umma hatakiwi kuwa kiongozi mwandamizi wa chama cha siasa!! hii sheria inawahusU wale wa vyama vya upinzani pekee? niwekeni sawa wakuu kwenye hili, HIVI Waziri si mtumishi wa umma?
 
Mie bado nashangaa sana uwezo wa hawa wanaoitwa viongozi wa CCM. Hivi hii rasimu wanayogombana nayo kwa maneno makali sana imeletwa kwenye Bunge maalumu na wapinzani? Hii rasimu sii imeletwa na tume ya katiba ambayo imeundwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM tena wajumbe wote waliteuliwa kwa utashi wake mwenyewe?
Tume imeleta maoni ya wananchi, UKAWA wameamua kuheshimu hayo maoni ya wananchi tabu iko wapi? Sasa utashangaa ugomvi wa CCM na wapinzani wao kuhusu katiba utadhani ile rasimu ni ya Chadema,CUF au NCCR.
Ninacho jiuliza hawa watu kama Mwigulu, Nape au Kinana wanajua wanachokiongea au wanajitia uchizi tuu kwa vile wameshaamua kuwadharau Watz? Maomba msaada hapo.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Kweli leo nimeamini kuwa mti mbaya kamwe hauwezi kuzaa matunda mazuri. Unaposema kuwa UKAWA wanasaka madaraka na sisiem kung'ang'a madaraka zaidi ya nusu karne madarakani ni nini? Sisiem wamekomba kila kitu, kila mtu yuko hoi kwa ukombaji wao. Hebu wawe wakweli katika chaguzi zote zilizofanyika ni kwa kuwa chaguzi zetu haziko huru. Ona nchi zilizo na tume huru uchaguzi ukianyika hakuna mwendelezo wa mtu fulani kushinda ni kwa Tanzania pekee. Hesabu ni watawala wangapi wamepita baada ya kuruhusiwa mfumo wa vyama vingi hapa Malawi na Zambia. Wakombaji wa sisiem hawataki kuachia. Huyo jamaa yenu kapora jina la mtu kwa hiyo sisiem wote ni waporaji na wakombaji Sisiem kama si wakombaji wasingeruhusu huyo mporaji wa jina la mtu awe katibu mkuu.
 
Mwigulu anatapatapa kwani hâta awalishe maneno kwa nguvu wananchi waliojitambua,hawatayameza.
 
Angetumia huo muda kuchangisha fedha kwa ajili ya kupeleka maji Singida ambako watu huchota maji kwa kutumia punda zaidi ya kilometa kumi toka makazi ya watu.Siasa za kujifurahisha.Wabaguzi ni chama cha majambazi
 
mwigulu nchemba: Achaneni na viongozi wabaguzi na wabinafsi.

katika mwenedelezo wa mikutano ya ccm kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi, mchakato wa katiba mpya na kujipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015, naibu katibu mkuu wa ccm (bara), mwigulu nchemba amewataka wananchi na wakazi wa mkoa wa morogoro kujiandaa na uchaguzi ujao wa serikali za mitaa nchini ili waweze kuwachagua viongozi watakaoendelea kutekeleza sera na ilani ya uchaguzi wa ccm kama inavyoendelea kutekelezwa nchi nzima kwa sasa.

Nchemba pia amewaasa wananchi kuwasikiliza na kuwapima wale wote wanaokuja na agenda za mchakato wa katiba wakati kiuhalisia wako kwenye mchakato wa kugawana madaraka kwa ajili ya kuzitumikia nafsi zao. Naibu katibu mkuu ccm(bara) ametumia sehemu kubwa ya hotuba yake kwa wakazi wa morogoro kuwaelimisha kuhusu mchakato wa katiba mpya ulipofikia na kile kinachozungumzwa na wanaojiita ukawa kwenye mikutano yao,

nchemba akizungumza kwa msisitizo wa hali ya juu amesema, "ukawa ni genge la watu wachache waliodhamiria kusaka madaraka kwa njia zozote kupitia idadi ya serikali. Kikundi cha ukawa kinazunguka nchi nzima kudanganya na kuwagawa watanzania kuhusu serikali tatu wakati historia pia inatuonyesha hawajawahi kutumia gharama kubwa kutekeleza miradi ya maendeleo au kuwaelimisha watanzania kuhusu kujiajiri".

Aliendelea kusema, 'baadhi ya wana kikundi wanatumia fedha za misaada na ruzuku kuzunguka angani kuwahadaa watanzania kuwa serikali tatu ni suruhisho la matatizo wakati serikali ya tatu haitajishughulisha hata na afya, elimu, nishati, barabara na maji.

Wanataka tutengeneze serikali ambayo kazi yake ni kukusanya kodi tu za watanzania na kuzitumia kulipa mishahara na marupurupu ya viongozi pekee badala ya kutumika kwenye mambo muhimu sana kwa watanzania kama afya, elimu, nishati, barabara na maji.

Watanzania lazima waelewe kuwa, hakuna serikali inayoendeshwa kwa gharama ndogo. Serikali ya tatu ikija kuna uwezekano wa kodi kupanda lakini vile vile kuna uwezekano mkubwa wa sehemu moja ya muungano kushindwa kuchangia serikali hiyo ya tatu na matokeo yake ni kuligawa taifa katika misingi ya utanganyika na uzanzibari kitu ambacho ni dhambi kubwa sana na haitatuacha salama.

Kuhusu uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, mh. Mwigulu nchemba amewaomba watanzania kuwa na imani na chama cha mapinduzi na waendelee kuichagua ccm kama ilivyofanyika kwenye chaguzi za nyuma na hata hizi za karibuni katika kata 27 na majimbo ya kalenga na chalinze.

Nchemba alisema, mkataba wa ccm na watanzania ni maendeleo na sio kuzunguka na helkopta angani kwa gharama kubwa ili kuitukana serikali na viongozi waasisi wa taifa letu.

Mwisho, mh, nchemba alisisitiza na kusema kuwa "kitendo cha wabunge wa upinzani kutoka nje ya bunge la jamuhuri wa muungano au la katiba ni kudhihirisha wazi kuwa hawafai hata kidogo kupewa uongozi. Hatuwezi kuwa na kiongozi anayesusa kuwatumikia wananchi wake. Wanasusia bajeti ya nishati na madini wakati wananchi wao wamewatuma bungeni kwenda kujenga hoja kwa ajili ya maendeleo yao. Wananchi wananyimwa fursa ya kujengewa hoja bungeni ili wapate nishati. Inasikitisha kuona kambi ya upinzani nchini yenye viongozi wabovu. Viongozi wasiokuwa na mboni ya kitaifa kuhusu taifa lao. Akili na mawazo yao wameelekeza kwenye ubinafsi na upotoshaji kwa watanzania kwa manufaa ya siasa zao za kibaguzi na kibinafsi.

nyie ccm hata mfiche aibu kwa kutumia viti ili watu waonekane wengi kwenye mikutano lazima ile kwenu. Kama na morogoro ndio mmepoteza mvuto hivi mmekwisha kaeni chini mfikirie.hivyo viti mnavyoleta kwenye mikutano mnavilipia? Maaana inaweza kuwa mmekopa halafu viingizwe kwenye deni la taifa watanzania masikini tuanze kudaiwa. Nassari anapeleka ,madawati shuleni watoto wasikae chini ccm kwa akili zenu mnayakataa. Mnawaza kuvuna tembo, mnataka watanzania waendelee kuwa maskini ili muendelee kuwadanganya na ahadi za maisha bora
 
Back
Top Bottom