Mwigulu: Naombwa nigombee urais 2015

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,687
2,238
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema makundi mbalimbali ya kijamii yameomuomba agombee urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Nchemba, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, aliyataja makundi hayo kuwa ni pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo, wanafunzi wa vyuo vikuu, Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wakulima na hadi watu wa vijiweni.

"Hata hivi karibuni nilipoenda Mwanza nilikuta bango kubwa limeandikwa ‘Mwigulu ni wewe unayekuja, au tumsubiri mwingine?" alisema wakati akihojiwa na kituo cha redio cha jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

"Ujumbe kama huu wa ‘ni wewe unayekuja, au tumsubiri mwingine' alipewa bwana mkubwa Yesu zama hizo. Aliulizwa na watu wake, akawajibu ‘mkiona neema zinakuja mjue ndivyo'."

Hata hivyo, Mwigulu alipotakiwa kutoa kauli yake kama atagombea, hakutaka kukubali wala kukataa na badala yake akachukua fursa hiyo kuwashukuru wale wote ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa kumtaka agombee.

Na alipobanwa zaidi, alisema: "Tutajua kama tutavuka mto tutakapofika mtoni."

Hata hivyo, akizungumza jana mchana na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mwananyamala, alisema kwa sasa hawezi kusema kama atagombea ama la kutokana na majukumu aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete.

Alisema jukumu la kwanza alilopewa ni kusimamia Wizara ya Fedha ambayo jukumu kubwa ni kuhakikisha kodi zote zinakusanywa na kuwafikia Watanzania kwa usawa.

Alisema jukumu lingine ni la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni Naibu Katibu Mkuu Bara na kwamba anategemewa kutimiza majukumu aliyopewa ya kichama.

Nchemba hata hivyo, alisema kuwa atatoa maamuzi yake ya kugombea ama la kipenga kitakapopulizwa akimaanisha muda rasmi CCM kitakapotangaza kuanza mchakato wa uteuzi wa mgombea.

Kwa miezi kadhaa sasa, Mwigulu amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa makada wa CCM watakaojitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho tawala ili kurithi nafasi itakayoachwa wazi na Rais Kikwete anayetarajiwa kumaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka 10 mwishoni mwa mwaka huu.

Wengine wanaohusishwa na harakati za kuwania nafasi hiyo ni mawaziri wakuu wastaafu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja; Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro.

Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangalah, walishatangaza nia ya kujitosa kwenye mbio za kuwania urais wakiwa ziarani nchini Uingereza huku Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akitangaza nia hiyo mwezi uliopita wakati akihutubia mkutano wa hadhara jimboni kwake. Dk.

Kigwangalah, alitangaza nia yake ya kujitosa kwenye mbio za urais wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

WAKWEPA KODI
Katika hatua nyingine, Mwigulu alisema anataka kuona watu ambao wanakwepa kulipa kodi na wakathibitika kutolipa kodi wanafungwa gerezani ili iwe somo kwa wengine.

Alisema anayekwepa kulipa kodi ni muuaji kwa sababu kuna watu wanakosa dawa na wanakufa kwa sababu ya ukwepaji wake huo.

"Kama mtu amekwepa kulipa kodi na ikathibitika kwamba amekwepa afungwe gerezani. Hapaswi kuwapo nje kwa sababu akiwa nje atahonga.
Anatakiwa alipe kodi na kisha akakae gerezani.

"Hatuwezi kufukuzana na mama mjane, huyu ambaye anauza karanga ili amsomeshe mwanaye ili tupate kodi ya senti chache wakati tunawaachia watu ambao wanakwepa kulipa mabilioni ya kodi," alisema.

Aliongeza kuwa hakubaliani na utaratibu wa kuwaondoa kwenye nafasi zao watu wasio na uzalendo wa nchi yao na kuwaacha huru hata baada ya kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha (kama bilioni 30); na badala yake akasema anataka watu hao wapelekwe gerezani kwani kutochukua hatua kali dhidi yao kunawapa nafasi ya kwenda kutumia vizuri fedha nyingi walizohujumu.

"Inapotokea kodi inayopaswa kulipwa ni dola milioni 45, halafu afisa wa kodi anaandika kiasi kinachotakiwa kulipwa kuwa ni Sh. milioni 45, huyu lazima ashughulikiwe kwa sababu lazima kuna tatizo. Haiwezekani afisa wa mamlaka ya kodi awe hajui kutofautisha kati ya Dola na Shilingi. Lazima ashughulikiwe. Na kama ni kweli kwamba hajui kutofautisha dola na shilingi, hafai kuwapo ofisini," alisema.

Aidha Mwigulu alisema hivi sasa anaendelea na mapambano dhidi ya watumishi wa umma wanaolipa mishahara hewa.

"Nilipata upinzani kidogo hapa kutoka kwa watu wanaonufaika na jambo hili, wakitoa sababu nyepesi kwamba ni ngumu kujua viwango vya michango yao katika mifuko mbalimbali na madeni mengine yanayowakabili. Lakini nasema kwamba mwajiri atakata michango yote kisha mishahara ndiyo italipwa kwa wahusika halali tu," alisema.

Chanzo:Nipashe

Ccm ndiyo imetengeneza na inalilnda kwa gharama yoyote majanga yote ya taifa hili.

Hakuna raisi atatawala Tanzania kutoka ccm. Mkifanya umafia wenu kama mlivyofanya serikali za mitaa, niwaambie mapema, mtakuwa marehemu wote. Mtauawa na wananchi na hamtaishi!.

Sasa ni muda wa wananchi kujilinda. Kwanza majengo yenu yote yatalipuliwa. Hakuna ofisi mtakayokaa haitakuwa majivu.

Tumechoka na upum.bavu wenu!. Nyie jipangeni lakini muandae hamtazikwa. Mtatupwa baharini na wengine mtaachwa porini muwe chakula cha fisi na ndege. Jidanganyeni.

MH Mwigulu Nchemba amenukuliwa katika gazeti moja leo akidai makundi mbalimbali yamemuomba agombee Urais mwaka 2015.

Ameyataja makundi hayo kwamba ni makundi ya dini wakiwemo waislamu na wakristo, vijana wa vyuo vikuu na makundi mengine.

Amesema alipotembelea Mwanza hivi karibuni akikutana na mabango makubwa yakisema hivi kweli wewe ndio Mwigulu unakuja kutembelea kuonyesha kwamba jambo hilo ni bahati kubwa kwa wanaMWANZA!!?.

Maoni yangu: Mwigulu pamoja na kuheshimu mchango wako mkubwa katika kukijenga chama na kupambana na mafisadi ndani ya nchi na hasa wizara ya fedha lakini nakuomba uwe mvumilivu bado hujawa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za nchi hii. Ni wakati mzee wa maamuzi magumu au kijana bright January wa Makamba au MwanaCCM mwingine aliyekomaa katika siasa za nchi hii.
 
Maoni yangu: Mwigulu pamoja na kuheshimu mchango wako mkubwa katika kukijenga chama na kupambana na mafisadi ndani ya nchi na hasa wizara ya fedha lakini nakuomba uwe mvumilivu bado hujawa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za nchi hii. Ni wakati mzee wa maamuzi magumu kuongoza au kijana bright January wa Makamba au MwanaCCM mwingine aliyekomaa katika siasa za nchi hii.
 
Iliwahi semwasemwa kwa matamko makali kwamba wapinzani ni waroho wa madaraka .Naomba kujuzwa kinachotokea Leo CCM kila MTU anautaka uraisi nano mroho wa madaraka?
 
Wote mwigulu na makamba wasubiri halafu Lowasa hafai ni fisadi mkubwa.
 
MH Mwigulu Nchemba amenukuliwa katika gazeti moja leo akidai makundi mbalimbali yamemuomba agombee Urais mwaka 2015.

Ameyataja makundi hayo kwamba ni makundi ya dini wakiwemo waislamu na wakristo, vijana wa vyuo vikuu na makundi mengine.

Amesema alipotembelea Mwanza hivi karibuni akikutana na mabango makubwa yakisema hivi kweli wewe ndio Mwigulu unakuja kutembelea kuonyesha kwamba jambo hilo ni bahati kubwa kwa wanaMWANZA!!?.

Maoni yangu: Mwigulu pamoja na kuheshimu mchango wako mkubwa katika kukijenga chama na kupambana na mafisadi ndani ya nchi na hasa wizara ya fedha lakini nakuomba uwe mvumilivu bado hujawa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za nchi hii. Ni wakati mzee wa maamuzi magumu au kijana bright January wa Makamba au MwanaCCM mwingine aliyekomaa katika siasa za nchi hii.

Makamba kijana bright?how?
 
Ccm ndiyo imetengeneza na inalilnda kwa gharama yoyote majanga yote ya taifa hili.

Hakuna raisi atatawala Tanzania kutoka ccm. Mkifanya umafia wenu kama mlivyofanya serikali za mitaa, niwaambie mapema, mtakuwa marehemu wote. Mtauawa na wananchi na hamtaishi!.

Sasa ni muda wa wananchi kujilinda. Kwanza majengo yenu yote yatalipuliwa. Hakuna ofisi mtakayokaa haitakuwa majivu.

Tumechoka na upum.bavu wenu!. Nyie jipangeni lakini muandae hamtazikwa. Mtatupwa baharini na wengine mtaachwa porini muwe chakula cha fisi na ndege. Jidanganyeni.
umetumwa wewe sio bure!
 
Mbona unatishia watu wazima mkuu? Watanzania wana akili wala hawapo tayari kuona amani ya nchi yao inapotea kwasababu ya watu wenye njaa ya madaraka.
 
Iliwahi semwasemwa kwa matamko makali kwamba wapinzani ni waroho wa madaraka .Naomba kujuzwa kinachotokea Leo CCM kila MTU anautaka uraisi nano mroho wa madaraka?

Nani asiepende kuwa kiongozi tena wa ngazi ya juu popote duniani? Ni haki ya kila mwanasiasa kutamani kufikia kiwango cha juu katika ngazi za uongozi.
 
Sasa mbona CCM haichezi kitimu sio watajeruhiana sana kiasi kwamba mpaka madonda yapone watakuwa wamejiumiza sana
 
Kiongozi siwatishii. Ninawapa tahadhari ili wanaposhaurian ujinga, wajue nini kipo mbele yao. Wangekuwa wanajali amani wasingeendeleza umafia huu wa wazi kama walivyofanya serikali za mitaa. Hawa wanachokifanya ni matusi kwa wantanzania na kuwaibia.

Muda wao umekwisha. Wakubali kuondolewa wakiwa hai (kwa kukubali matokeo sahihi ya chaguzi), ama waondolewe wakiwa wafu!. (Kwa kulazimisha utawala kimafia). Hakuna lugha laini wala mbadala. Huu ndio ukweli kiongozi.

Mimi hata wakiniua, ikiwa maccm yatakuwa hayapo, wala sijuti. wanangu na wajukuu watakuwa wanaishi ndani ya nchi yao.

Mbona unatishia watu wazima mkuu? Watanzania wana akili wala hawapo tayari kuona amani ya nchi yao inapotea kwasababu ya watu wenye njaa ya madaraka.
 
Promotion zinaendelea, kaeni chonjo. Jisomee mwenyewe gazeti Nipashe la leo.
 
siyo kila akupigiae makofi anakupongeza wengine wanakuchora,mwigulu kuwa makini na mabango ya kukudhihaki hatukutaki
TEAM lowassa
 
Last edited by a moderator:
Mimi hata sihangaiki kutafuta gazeti la mengi gazeti lenyewe la kiminga hata hoja yenyewe ya kijinga kwanii kujisumbua.
 
Back
Top Bottom