Obama wa Bongo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 5,416
- 4,872
he deserve to be a next president! tatizo nchii hii uswahili mwingi sana hatapita NEC
Mwigulu amebeba dhamira ya kweli tatizo ni mfumo uliopo ndani ya chama chake ataweza kuufuta.
Wanabodi,
Tuweke ushabiki pembeni, kati ya watangaza nia watatu kati ya jana na leo, Mwigulu Lameck Nchemba is the most bonafide genuine mgombea so far, ukimuangalia huku unamsikiliza, utaiona his genuinety kutoka moyoni mwake 'to practice what he preach' kwa aliyoyasema yanaonekana kabisa yametoka moyoni mwake, tofauti na hawa wengine wawili waliyoyatamka yametoka tuu midoni mwao, hivyo kiukweli kabisa wa nafsi yangu, nadhani kwa kati ya hawa watangaza nia watatu so far, naamini Mwigulu can make the best president this country has e has ever had tangu Mwalimu Nyerere!.
Jee wewe mwenzangu ulibahatika kumsikia, unamuonaje?!.
NB: Ku make the best president ni jambo moja, lakini kuchaguliwa na chama kuwa mgombea ni jambo jingine!.
Kati wa watangaza nia hawa watatu, kuna mgombea anayependwa sana na watu na huyu sii mwingine bali ni ni Edward Lowassa, jee ni kwa nini Edward Lowassa anapendwa sana, sababu zinajulikana!, ila kama urais ni kupendwa basi rais wetu ni Lowassa!.
Kuna mgombea ambaye ni the most experieced so far, huyu ni Stephen Wasira, yeye ana uzoefu toka enzi za Nyerere alikuwa mbunge wa CCM, akahama CCM na kuwa mbunge wa upinzani, na kisha kurejea CCM, hivyo kama urais ni uzoefuu, then rais wetu ni Wasira.
Kati ya hawa watangaza nia watatu wa mwanzo wa CCM, Mwigulu Nchemba kwenye aspect ya originality na genuinety, Mwigulu ndio the most real, the most original na the most genuine!.
Mwigulu ameonyesha yuko real and down to earth kwa kuonyesha ametoka familia masikini, sio mtu wa makuu ya kujionyesha ili just to impress people kwa mbwembwe zozote kwenye uzinduzi, set yake ilikuwa simple, ameongelea background yake ya kimasikini na kuthibitisha kuwa yeye ni best brain tangu alikopita mpaka hapa alipo lakini kamwe hajasahau alikotoka!, hivyo huyu ndio mfano halisi wa Mtanzania wa kawaida, anaonyesha anawajua Watanzania, anaijua Tanzania, anawajua Watanzania wanataka nini, na anaijua Tanzania inatakiwa ifanye nini kutoka hapa tulipo twende kwenye the next level!.
Ukiangalia speech za wengine ni za kuandikiwa wa na mtu akisoma speech ya kwake mwenyewe aliyoiandika mwenyewe, utamjua, mtu akisoma speech aliyoandikiwa kisha aka kremu na kuja kusoma utamjua, na mtu akiandika speech yake mwenyewe na kuisoma mwenyewe, utamjua!, Mwingulu ndio was the most original, amekuja na talking notes too kama Nyerere na vitu vyote kutoka kichwani!.
Hivyo kwa maoni yangu, so far, ni Mwigulu ndio can make the best president this country can ever had, ila kwa sababu watia nia wanaendelea nitaendelea kuwapatia uchambuzi wangu kidogo kidogo kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa!.
Wakati tukielekea kumpata rais wetu wa 2015, kwa vile CCM ndio chama tawala, hatuwezi kukwepa kuuzungumzia mtindo wa uchaguzi wa kumpata mgombea wa CCM kwa sababu za kihistoria ya hii miaka 50 ya uhuru wetu, mgombea wa CCM ndie rais wa nchi, unless kama mwaka huu historia itabadilika!.
Tukiuchukulia mchakato wa 2005 wakati JK alipochaguliwa, kama reference, assuming hawa watatu ndio wameingia tatu bora, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakipewa choice ya kuchagua between "the most loved", "the most experienced" and the "the best president", watachagua mtu 'anayependwa na watu', mtu 'atakayechagulika' kwa urais kwa lengo la kuwapatia ushindi, na baada ya kumpitisha mbinu nyingine zote safi na chafu hutumika kwa sababu lengo ni ushindi, na ukiishapatikana zile mbinu zilizotumika zinakuwa justified na the end results.
Hivi ndivyo JK alivyochaguliwa ile 2005 kwa sababu kwenye the finalist watatu, JK was never the best, kulikuwa na "the most experienced" Dr. Salim, "The best Brain", Prof. Mwandosya, na "the good looking" Jakaya Kikwete, akapitishwa JK kwa hoja kuwa 'ni mwenzetu' ndiye 'anayependwa na watu', as if mapenzi ya watu ndio uongozi wa nchi!. Matokeo ya kumchagua rais 'mwenzetu' na sifu kuu ni 'kupendwa na watu' ili kukiletea chama ushindi wa kishindo, ndio haya ya kuunda serikali ya kishikaji yenye madudu kibao!, watu wakiboronga ni kuhamishia tuu, kwa sababu ni 'wenzetu', jee kwa 2015 Watanzania wanahitaji rais 'mwenzetu' tena, au this time tunahitaji the best?!.
JF has a role to play kupitia ma great thinkers wa jf, tutangulize mbele maslahi ya taifa kwa kuyaweka pembeni mahaba niue ya wapendwa wetu, na kujitolea kuwaelimisha wananchi wetu nchi hii inahitaji nini na kuongozwa na mtu wa aina gani, ili waweze kufanya informed decisions kwenye choice of president, ili ifike mahali chaguo la mgombea wa CCM sio lazima ndio automatikally awe rais wa nchi, kama CCM wakituletea ule ujinga ujinga kama wa 2005, tunapiga tuu chini CCM only if huko kungine kuna the better alternative!.
Ushauri wangu wa kwanza kwa wana JF, huyu Mwingulu Nchemba sio mtu wa kubezwa hata kidogo, he is a man to keep a close watch seriously, if the best is what we are looking for!.
NB. Kwa walionidhania mimi Pasco wa jf, niko kambi fulani, naomba tena kuwathibitishia kuwa Pasco wa jf, hana chama, hana kambi, hana mtu, ila kuna watu anawakubali akiwemo yule 'jamaa yetu', lakini linapokuja suala la kuchagua kati ya mapenzi binafsi kwa watu na maslahi ya taifa, nitatanguliza maslahi ya taifa mbele!, hivyo sitarajii kuulizwa kama nimehama kambi kwa sababu sijawahi kuwepo kambi yoyote!.
Hivyo kati ya hawa watatu wa mwanzo, kiukweli mimi Pasco wa jf, nimeguswa na Mwigulu Nchemba!.
Vipi wewe?.
Pasco
NB. Kutokana na kuwa bize na mambo mengi, sitaweza kuchangia uzi huu, wala kujibu hoja au swali lolote hivyo nitakushukuru kama utasoma tuu bila kuniuliza chochote!.
ANAFAA KUWA RAIS LAKINI MUDA BADO STILL 2 YOUNG/ asubirie 2025
apate uzoefu ndani ya serekali kwanza!!!
Red Giant latu huwezimlinganisha Nyererr na Mwigulu.... uthubutu wao ni tofauti kabisa. Nyerere aliyethubutu kuwaface wakoloni na masilaha yao... na huyu ambaye hata kutamka atawashughulikiaje watuhumiwa wa Escrow, EPA na mafisadi wengine ndani ya chama chake ameshindwa ndio tumlinganishe na Nyerere wa wakati ule?hivi 1961 nyerere alikuwa na umri gani?
kuna theory ya history make the man. inasema mwigulu angekuwepo 1961 angepambana na wakooloni na Nyerere angekuwepo leo asingeweza pambana na mafisadi.Red Giant latu huwezimlinganisha Nyererr na Mwigulu.... uthubutu wao ni tofauti kabisa. Nyerere aliyethubutu kuwaface wakoloni na masilaha yao... na huyu ambaye hata kutamka atawashughulikiaje watuhumiwa wa Escrow, EPA na mafisadi wengine ndani ya chama chake ameshindwa ndio tumlinganishe na Nyerere wa wakati ule?
I am glad someone else could see through Mwigulu, Mwigulu uses the people agenda as his main speech, however he needs to stay consistent and tell us his strategy, so far he has only been telling us ACTION PLANS, well you cant make president if you talk of action plan, that level is not for presidents, that's for DIWANI NA MBUNGE, lets talk US politics, when Obama went out to the mass with his message, it was CHANGE, , he stayed consistent with his message, but it was not built on action plans, rather long term strategies , I will await for others to see , we need to be able to draw a line between.............................1. STRATEGIES 2. INITIATIVES 3. ACTION PLANSMwigulu ni opportunistic populist tu.
nimewaeleza watu wakabisha sana. mimi nimekaa pale Idara ya Uchumi, UDSM. najua mtu akisomeshwa masters na BoT (yeye amesomeshwa masters baada ya kuongoza GPA), anapata ajira moja-kwa-moja hata kabla hajamaliza. lakini cha kushangaza eti anasema alibeba zege. watu nao wanakubali, wanampigia makofi.