Mwigulu, IGP Mangu, mkuu wa TISS watumbuliwe

Anaandika mdude chadema!

MAWAZO YA MDUDE NYAGALI KUHUSU TUHUMA ZA MBOWE NA MADAWA YA KULEVYA.

Sakata la mbowe na dawa za kulevya viongozi wafuatao wanapaswa kuachia madaraka haraka sana.

1.Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba.
2.Mkurugenzi wa usalama wa taifa TISS
3.Mkuu wa jeshi la polisi tanzania IGP

Haiwezekani mbowe mabaye ni kiongozi mkuu wa upinzani ambaye kila siku anapishana na serikali,anakosoa serikali anahujumiwa uchumi wake na serikali anaingiza madawa ya kulevya nchini na kufanya biashara,IGP hajui,usalama wa taifa hawajui,waziri wa mambo ya ndani hajui anakuja kujua makonda mabaye ni RC tu.

Kama mbowe anaweza kuingiza madawa nchini bila vyombo vya usalama kujua basi kumbe mbowe anaweza kuingiza silaha nchini vilevile bila vyombo vya usalama kujua na akapindua serikali tukufu ya mheshimiwa mtukufu rais.

Kwa hili kwa kweli nchi yetu haipo salama kama kiongozi wa upinzani mpinzani mkuu wa serikali anaingiza dawa vyombo vya usalama mpaka waziri hajui,Kumbe wanaweza kuiingia al-shabaab na magaidi wengine bila vyombo vya usalama kujua.

Nina muomba mtukufu rais awatumbue IGP,mkurugenzi wa TISS na waziri wa mambo ya ndani kwa kukosa umakini kwa kuhatarisha nchi yetu kiusalama kisha kumpandisha cheo RC wa dar es salaam Paul C. Makonda kwa umakini wake wa kufanya kazi nzuri ususani ya kugundua kiongozi wa upinzani kuingiza madawa,

Ikiwezekana makonda ateuliwe ubunge kisha apewe uwaziri wa mambo ya ndani kwa kuwa inaonyesha ana interejensia kuliko IGP na jeshi lake,Lakini pia kazi ya makonda imemvua nguo waziri wa mambo ya ndani mwigulu nchemba kana kwamba hatoshi kuwa waziri kabisa

Mdude nyagali
Sumu ya nyigu
AKILI yako ndipo ilipoishia kufikiri hapo...unafikiri wanatumbuliwa kirahisirahisi hivyo kwa mihemko iliyopo..si kama unavyofikiri DOGO.
 
Vipi ile list yenu ya mafisadi mahakama iliwathibitisha?
Akili zako sasa unadhani kwa sababu nimeandika hilo basi Mimi ni mwanasiasa?
Subiri Ccm wenzako sijui Chadema wenzio waje mrumbane Mimi sio mwanasiasa.
Nimeandika utaratibu unaotakiwa kuwepo ili mtu aitwe mkosaji.
 
siasa zimetulevya sana, yaani kuna watu wana amini upinzani na serikali ni watu tofauti. huku kwetu wanaigiza kusumbuana ila kiundani lao moja. wanajuana kupiga kwao madili, wanalindana sana unashangaa mbowe kutuhumiwa madawa na kudhani wahusika hawafahamu.

rejea mtafaruku kidogo wa mbowe na kundi lake vs zitto walianza umbuana madili wanayopiga na serikali. zzk alimsema lissu kupiga dili, lissu pia alianika yake.

hawa wanajuana wakuu si wenzetu.wanalindana na kuigiza ugomvi mbele yetu
 
halafu hii agenda mngeitumia ingewapa credity sana kama ile ya list of Shem ya mafisadi kwa nini upinzani hawakuwahi kuitumia agenda hii ya madawa y kulevya ili kujienrich kisiasa!?
 
Daaaah.....Kuna watu wana AKILI ...na unaona fahari kutoa credits , Hongera sana kwa upembuzi huu...Natamani hii makala iwekwe kwenye gazeti LABDA itawafanya watu wafikiri. LABDA
Jamaa ni genious!!mwenye akili ameelewa
 
mheshimiwa RAIS hongera kwa juhudi kubwa unazofanya ....Sasa WATU ndo wameanza kukuelewa kua VITA HII umeivalia MKANDA NA KWAMBA UPO TAYARI KUMLINDA NA KUMTETEA MAKONDA ..

Ni IMANI yangu kua WAZIRI MWIGULU hafai na Anakuzunguka ....Haiwezekani RAIS Wanchi umefanya Juhudi kwa upande wako .....Umemthibitishia kua "" Hata kama ni mke wako àkamatwe""" nabado Leo "" umemwongezea watendaji KATIKA kupambana na janga hili """"

Chakushangaza amekula BUYUUUU ..AMEUCHUNA KAMA HASIKII ....

MHESHIMIWA RAIS NAJUA MWIGULU NI MWANACCM ILA NAKUOMBA KATIKA VITA HII HAWEZI KUIONGOZA .

NATUMAIN MAKONDA MUDA MFUPI UTAMPA UWAZIRI WA MAMBO YA NDANI AU UKISHINDWA NAOMBA UUANZISHE WIZARA MPYA YA MAMBO YA KIZARURA AMBAYO WAZIRI WAKE ATAKUA MAKONDA ...AU UKISHINDWA NAOMBA UWABADILISHE ..HUYU NWIGULU MPELEKE WIZARA NYINGNE NA HII WIZARA YA MAMBO YA NDANI UUMPE MH PAUL MAKONDA ..

MH RAIS ..NIMATUMAIN YANGU KWA KUFANYA HATUA HII VITA TUTAISHINDA LKN KAMA MAPAMBANO YATAENDELEA NA MWIGULU YUPO KATKA WIZARA HII HATUTOFIKA .
7192f3b7a68b84d21adb5c4d215b7bf5.jpg
 
Anaandika mdude chadema!

MAWAZO YA MDUDE NYAGALI KUHUSU TUHUMA ZA MBOWE NA MADAWA YA KULEVYA.

Sakata la mbowe na dawa za kulevya viongozi wafuatao wanapaswa kuachia madaraka haraka sana.

1.Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba.
2.Mkurugenzi wa usalama wa taifa TISS
3.Mkuu wa jeshi la polisi tanzania IGP

Haiwezekani mbowe mabaye ni kiongozi mkuu wa upinzani ambaye kila siku anapishana na serikali,anakosoa serikali anahujumiwa uchumi wake na serikali anaingiza madawa ya kulevya nchini na kufanya biashara,IGP hajui,usalama wa taifa hawajui,waziri wa mambo ya ndani hajui anakuja kujua makonda mabaye ni RC tu.

Kama mbowe anaweza kuingiza madawa nchini bila vyombo vya usalama kujua basi kumbe mbowe anaweza kuingiza silaha nchini vilevile bila vyombo vya usalama kujua na akapindua serikali tukufu ya mheshimiwa mtukufu rais.

Kwa hili kwa kweli nchi yetu haipo salama kama kiongozi wa upinzani mpinzani mkuu wa serikali anaingiza dawa vyombo vya usalama mpaka waziri hajui,Kumbe wanaweza kuiingia al-shabaab na magaidi wengine bila vyombo vya usalama kujua.

Nina muomba mtukufu rais awatumbue IGP,mkurugenzi wa TISS na waziri wa mambo ya ndani kwa kukosa umakini kwa kuhatarisha nchi yetu kiusalama kisha kumpandisha cheo RC wa dar es salaam Paul C. Makonda kwa umakini wake wa kufanya kazi nzuri ususani ya kugundua kiongozi wa upinzani kuingiza madawa,

Ikiwezekana makonda ateuliwe ubunge kisha apewe uwaziri wa mambo ya ndani kwa kuwa inaonyesha ana interejensia kuliko IGP na jeshi lake,Lakini pia kazi ya makonda imemvua nguo waziri wa mambo ya ndani mwigulu nchemba kana kwamba hatoshi kuwa waziri kabisa

Mdude nyagali
Sumu ya nyigu
Kesho unaitwa central kwa kuandika habari za uchochezi
 
Ni mawazo ya ovyo kabisa yaliyoletwa na mleta post, ni upofu wa uelewa. Hivi TISS, IGP na Waziri alitaka wajue lini kwamba Mbowe ni mtuhumiwa kati ya ma-Drug dealers? Huu ni upofu wa mahaba uliopitiliza. Kama anadhani hawa watu hawajui kazi yao, yeye ajaribu kuingiza hizo siraha zake.

Mbowe ni Mr. Ziro, alifeli kidato cha VI ndiyo maana hata mawazo yake ni ya ovyo ovyo tu. Hata huyu aliyeleta post ndiyo wale wale ambao siku zote wao hudhani makisa yoyote au tuhuma zozote zinazomlenga kiongozi wa upinzani huwa ni kusingiziwa, na kwamba ni njama za kusiasa.

Ila tuhuma hizo hizo zikielekezwa kwa CCM huwa ni sahihi kabisa. Huu ni upumbavu ambao haufai hata kuletwa mitandaoni na sijui kwanini moderator anaruhusu upuuzi huu.
Povu LA nini hadi matusi?
Wafaaaaaaaaa
 
Anyway hatujajua yeye ni mwingizaji ama mtumiaji ama anasaidia kuingiza kwa kutumia watu wake. Tusubiri
 
Mkuu unaongea kama unaushahidi vile, ukiitwa kusaidia polisi utakwenda kweli
 
Daaaah.....Kuna watu wana AKILI ...na unaona fahari kutoa credits , Hongera sana kwa upembuzi huu...Natamani hii makala iwekwe kwenye gazeti LABDA itawafanya watu wafikiri. LABDA
Uandishi wa mleta mada, kuna wengi hawajagundua assadsyria3 anamaanisha nini.
 
Makusudically Wewe ulifaulu kidato cha Sita? Kwani kufeli kidato cha sita ni ajabu kwa nchi yetu? Kwani wewe unafikiri kufeli kidato cha sita ndio mwisho wa maisha? Kama kweli Mbowe alifeli kidato cha sita na sasa hupo hapo alipo basi ni mfano bora kwa wengine wanaofikiri kufeli mtihani wa darasani ni kufeli maisha. Hongera Mbowe kuionyesha dunia na akina
Makusudically kuwa kufaulu maishani ni zaidi ya kufaulu darasani.
 
Ni mawazo ya ovyo kabisa yaliyoletwa na mleta post, ni upofu wa uelewa. Hivi TISS, IGP na Waziri alitaka wajue lini kwamba Mbowe ni mtuhumiwa kati ya ma-Drug dealers? Huu ni upofu wa mahaba uliopitiliza. Kama anadhani hawa watu hawajui kazi yao, yeye ajaribu kuingiza hizo siraha zake.

Mbowe ni Mr. Ziro, alifeli kidato cha VI ndiyo maana hata mawazo yake ni ya ovyo ovyo tu. Hata huyu aliyeleta post ndiyo wale wale ambao siku zote wao hudhani makisa yoyote au tuhuma zozote zinazomlenga kiongozi wa upinzani huwa ni kusingiziwa, na kwamba ni njama za kusiasa.

Ila tuhuma hizo hizo zikielekezwa kwa CCM huwa ni sahihi kabisa.
Wewe una akili kweli? Hoja hapa ni Makonda kuwazidi kete IGP,TISS na Waziri wa Mambo ya ndani.Mbowe (pamoja na ziro yake) ana wafuasi wengi na hivyo nyendo zake lazima zijulikane kwa TISS,IGP na MMN kwanza kuliko kwa RC.Rais ampandishe Makonda cheo ili amsaidie kwa karibu zaidi kuliko hao!!
 
Back
Top Bottom