Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Mkuu, hata sie wananchi tuko hivo hivo. Angalia ziara za Kinana na Nape nchini, wakati Kinana kajikita kuongelea kwa kuiponda katiba mpya na kusema sio muarobaini wa matatizo ya wananchi, Nape hapo hapo jukwaani anaponda kuzungumzia katiba mpya eti ni ya 'wanasiasa' halafu wananchi hatuwaulizi wao kazi yao ni nini?
Wanatuambia (Kinana na Nape) kuwa wanaotaka serikali tatu wanauroho wa madaraka, hatuwaulizi wao humo CCM wamo kama akina nani na pendekezo la muundo huo ni wetu wananchi sio viongozi wa vyama!!!!!!! Tatizo ni SISI.
Nakubaliana na wewe, lakini mambo yanabadirika. Mambo hayapo kama yanavyoripotiwa na vyombo vya habari, wananchi wengi sasa hawaiamini tena CCM na serikali yake. Enzi zile ilikuwa kiongozi akitamka kitu kilikuwa kinachukuliwa kama msahafu na wananchi, mambo hayapo hivyo tena, CCM wanatumia gharama kubwa sana kuitangaza mikutano yao lakini raia wameshaijua janja yao, wanawaignore.