Mwigulu akalia kuti kavu Iramba Magharibi

Status
Not open for further replies.
Nadhani kuna uchaguzi wa Vijiji na vitongoji kadhaa jimboni Iramba mwaka huu.Nawashauri Chadema waanze na hili iwe kama Trailer kwa Mwigulu kumuonyesha vita sasa inapiganwa mlangoni mwake.

Nimeipenda strategy ya wafuasi wa Chadema wanafanya kama Wamarekani kwamba mfuate adui huko huko aliko ukamchakaze na usimpe nafasi ya kutoka nyumbani kwake.

Nawashauri viongozi wa Kanda ya Kati wachukulie maombi haya ya wafuasi wa Chadema kwa umakini na umuhimu mkubwa.Wanachotakiwa ni kuratibu zoezi husika.Kwa kweli mamilioni yatachangwa endapo wakifungua akaunti maalum kama maombi ya wanachama yanavyosema.

Pia namshauri Kitila Mkumbo apokee kwa unyenyekevu mkubwa heshima hii ya wanachama waliyoonyesha kwake.Awaongoze kuhakikisha Chadema inakuwa na nguvu Iramba kama ilivyo katika jimbo la Arusha mjini kwa Godbless Lema.
 
Last edited by a moderator:
Mwigulu hapo ndipo atajua kuwa hata sis wana ccm tumemchoka hatukumtuma bungeni kutukana na wala hapewi athabu kwa sahabu eti ni ccm,spika pia anachangia ccm kufa Mungu awape ufahamu ili wajue walau wabadilike,tumeni hiyo akaunti hat mimi mwana ccm nitachanga na 2015 hakutakuwa na viti maalumu kutokana na KATIBA.
 
Tunaisuairi kwa hamu sana hii acount ya ondoa mwigulu iramba. Ifungueni tuchangie.nyambafu sana huyu jamaa,siasa za staha yani haziwezi kabisa. Halafu na nyie wabunge wa chadema na makamanda wengine kila wiki muwe mnapiga mikutano hapo iramba,ebbo!
 
yaan thread za chadema kama kitchen part sababu mnazianzisha wenyewe mnakaa mnashe ujinga tu humu ndan
 
mimi mnyiramba haswa napenda changamoto za chadema ila ukweli lazima tuseme kwa sasa mwigulu nchemba anatisha sio iramba magharibi tu bali ni iramba nzima na hakika nina imani hata huyo kitila mkumbo ndani ya moyo wake anakiri ya kwamba jamaa ni jembe la wanyiramba hivyo basi mwigulu nchemba 2015 anapita bila kupingwa.
 
Hili wazo nimewahi kumweleza ra
fiki yangu tulipokuwa tunajadili wazo la Mwigulu kuibambikizia Kesi ya Ugaidi Rwakatare, kwamaba niko tayari kuchangia pesa kwa kiwango cha juu huyu mzinzi na muaji aondoke pale Iramba tena wajue kwamba nguvu ya umma in mkono mrefu zaidi ya policiccm, Wakubwa mimi niko tayari na ntampigia Dr mkumbo ili atakapo tangaza nia nimtumie mapesa maana namfahamu,
Sio huyu mzinzi TU msisahau Monduli na majimbo yanayokaliwa na CCM kwa ndugu zangu wamasai,
MIMI NIKIMALIZA CHUO TU BREAK YA KWANZA NI KWA WAJOMBA ZANGU MONDULI KUENEZA KAMPENI ONDOA FISADI MASAILAND MONDULI.
WANAKUBWA WA JF MUNGU AWABARIKI HIKI NI KISIMA CHA WAZALENDO.
"AIBU IWE JUU YA VIONGOZI NA WAFUASI WOTE WA CCM, WAWE SIKU ZOTE NI WATU KUPATA AIBU KWA KILA JAMBO NA WAKOSE KIBALI MACHONI PA MUNGU NA WATZ NA WATU WOTE WASEME AMEN"
 
Kampeni ya maana ni Ondoa CCM Iramba (OCI). Huyu Mwigulu amechokwa mno huku hata ndani ya CCM. Imefika mahala Dk Kitila anapewa minutes za vikao vya Kamati ya Siasa ya CCM. Kuna mjumbe mmoja kikao kilichopita ali-record kikao kizima cha Kamati ya Siasa cha Wilaya ambacho walitumia zaidi ya nusu kumsema Kitila na CHADEMA. Mkanda uliorekodiwa akapelekewa Kitila. CCM imepasuka mno Iramba kuhusu Mwigulu na kwenye kura za maoni hawezi kupita. Sasa CHADEMA watachanganyikiwa kama atapitishwa mtu mwingine, kama vile Chilolo au Kilimba. Ndio maana nasema tuhangaike na kuitoa CCM kwa sababu Mwigulu hatakuwa issue ifikapo 2015. Mie naongea haya nipo hapa Kiomboi ndani ya Halmashauri na naelewa kinachoendelea. Iramba ilikuwa ngumu sana kuingia upinzani lakini upuuzi wa Mwigulu na ujio wa Dk Kitila umebadilisha kila kitu. Achaneni na hao wajinga wanaojiita Shelui wanaojidanganya kwamba Mwigulu ni kipenzi cha wanyiramba. Haijawahi kutokea tukawa na mnyiramba wa ovyo kama huyu Mwigulu.

Nyongeza: Kuna madiwani watatu wa CCM wanajiandaa kuchomoka kuingia CHADEMA. Wote wamaeshamwambia Kitila na kuna uwezekano nao wakapokelewa hivi karibuni kama yule wiki jana. Ninafuatilia na nitawapa concrete information kuhusu hili very soon.
 
mimi mnyiramba haswa napenda changamoto za chadema ila ukweli lazima tuseme kwa sasa mwigulu nchemba anatisha sio iramba magharibi tu bali ni iramba nzima na hakika nina imani hata huyo kitila mkumbo ndani ya moyo wake anakiri ya kwamba jamaa ni jembe la wanyiramba hivyo basi mwigulu nchemba 2015 anapita bila kupingwa.

Mbona unajichanganya mkuu? Unamaanisha Mwigulu atakuwa mgombea pekee 2015? Ama hujui maana ya kupita bila kupingwa?
 
Kampeni ya maana ni Ondoa CCM Iramba (OCI). Huyu Mwigulu amechokwa mno huku hata ndani ya CCM. Imefika mahala Dk Kitila anapewa minutes za vikao vya Kamati ya Siasa ya CCM. Kuna mjumbe mmoja kikao kilichopita ali-record kikao kizima cha Kamati ya Siasa cha Wilaya ambacho walitumia zaidi ya nusu kumsema Kitila na CHADEMA. Mkanda uliorekodiwa akapelekewa Kitila. CCM imepasuka mno Iramba kuhusu Mwigulu na kwenye kura za maoni hawezi kupita. Sasa CHADEMA watachanganyikiwa kama atapitishwa mtu mwingine, kama vile Chilolo au Kilimba. Ndio maana nasema tuhangaike na kuitoa CCM kwa sababu Mwigulu hatakuwa issue ifikapo 2015. Mie naongea haya nipo hapa Kiomboi ndani ya Halmashauri na naelewa kinachoendelea. Iramba ilikuwa ngumu sana kuingia upinzani lakini upuuzi wa Mwigulu na ujio wa Dk Kitila umebadilisha kila kitu. Achaneni na hao wajinga wanaojiita Shelui wanaojidanganya kwamba Mwigulu ni kipenzi cha wanyiramba. Haijawahi kutokea tukawa na mnyiramba wa ovyo kama huyu Mwigulu.

Nyongeza: Kuna madiwani watatu wa CCM wanajiandaa kuchomoka kuingia CHADEMA. Wote wamaeshamwambia Kitila na kuna uwezekano nao wakapokelewa hivi karibuni kama yule wiki jana. Ninafuatilia na nitawapa concrete information kuhusu hili very soon.

Nimeyatambua na kuyaheshimu sana maneno yako mkuu Imebidi.

c.c Kitila Mkumbo.
 
Last edited by a moderator:
Mbona unajichanganya mkuu? Unamaanisha Mwigulu atakuwa mgombea pekee 2015? Ama hujui maana ya kupita bila kupingwa?

Mkuu wangu MOLEMO mbona kiswahili nilichoandika kinaeleweka? basi isiwe taabu nina maana atapita bila kupingwa na mtu yeyote hata huyu kitila mkumbo atamuunga mkono mhe.mwigulu nchemba kwa 100%.
 
Jamani pamoja na hayo yote, naomba mtu ambaye analifahamu vizuri jimbo hili la Iramba Magharibi atuorodheshee mambo ambayo Mwigulu Nchemba ameshayafanya kwa wananchi wake.

Naomba hata yale anayowatetea bungeni yawekwe.
 
Mkuu wangu MOLEMO mbona kiswahili nilichoandika kinaeleweka? basi isiwe taabu nina maana atapita bila kupingwa na mtu yeyote hata huyu kitila mkumbo atamuunga mkono mhe.mwigulu nchemba kwa 100%.

Mkuu wangu kwa hiyo hata yule msaidizi wake aliyekabidhiwa kadi na Dr Slaa juzi atampigia kura Mwigulu? Na pia unamaanisha Dr Kitila naye atampigia kura Mwigulu?.

Hii ni mpya kwangu mkuu lakini nakushauri endelea kuamini hivyo hivyo.
 
Fanyeni haraka kuanzisha hiyo account nichangie huyu jamaa anaitwa Mwigulu simpendi mpk nikimuona nahisi kichefuchefu
 
Naona kama 2015 ni mbali, Mwigulu hana na hakuwa na sifa ya kuwa mwakilishi wa wananchi mahali popote pale..Wananchi tukiendekeza vitamaa vya kijinga tutaendelea kuwapa watu wasiofaa usukani wa uongozi bila ya wao kujua wapi wanataka kutupeleka.
Kuna wakati naona kama tunajiadhibu kwa uamuzi wetu usiokuwa na maana wala mantiki yoyote!
 
Hali ya chuki dhidi ya CHADEMA inayoonyeshwa na mbunge wa Iramba Magharibi dhidi ya CHADEMA imesababisha wafuasi wa CHADEMA kote nchini kuungana kuhakikisha CHADEMA inamshinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu katika jimbo la Iramba 2015.

Mwigulu Nchemba anakabiliana na Msomi aliyebobea Dr Kitila Mkumbo ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Pia wafuasi wa CHADEMA wameapa kuhakikisha CHADEMA inazoa viti vyote vya udiwani Iramba Magharibi ili kumuonyesha ni nini maana ya nguvu ya umma.

Katika mahojiano na wafuasi kadhaa wa CHADEMA wa mikoa ya Mara,Kagera na Mwanza wameutaka uongozi wa CHADEMA kuanzisha Akaunti maalum ambayo itachangiwa na wanachama kuhakikisha Mwigulu harudi bungeni.

Wanachama hao wamesema chuki ya Mwigulu dhidi ya Chadema hailezeki na ameapa kutumia njia zozote kuiangamiza CHADEMA.Wamesema hata awapo bungeni hatetei chochote wanaIramba zaidi ya kutukana na kukashifu viongozi wa CHADEMA.

Hii itakuwa ni Operesheni Ondoa Mwigulu Iramba(OMI) walisema wafuasi hao wa Chadema.Pia walisema watajitolea kukaa Iramba kipindi chote cha Kampeni kuhakikisha Mgombea wa CHADEMA anapata ushindi wa 80%.

Kwa sasa Jimboni Iramba Dr Kitila Mkumbo anazungumzwa kila kona ya Jimbo hilo kama mwanasiasa makini,mpole na mtetezi wa dhati wa wananchi.Mzee mmoja katika kata ya Ndago Iramba aliwahi kusema mwaka jana kuwa kwa kawaida watu wa Iramba ni wanyenyekevu na wenye kupima maneno kabla ya kuzungumza mfano wa Dr Kitila.Mzee huyo alisema hawakuwahi kujua kama kuna siku wangekuwa na mbunge mwenye kuhamasisha chuki ndani ya jamii kiasi cha kuhatarisha amani ya nchi.

Si huyu peke bali majangili wote ukiondoa Mpinai_mtu safi,Lugola_mtu safi na Fnjombe_mtu safi ,wengineo wote lazima wang'oke kwa hali na mali.
 
Kwa hiyo mukimuondoa Mwigulu ndio mmeindoa CCM madarakani? mawazo ya kijinga haya.
 
Account please kila mwezi nikitupia tupia kwa m-pesa nadhani 2015 itakuwa na vibilioni kadhaa. OMI hand to hand with M4C.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom