Mwigamba has said it all "Wimbo wa kasi mpya umefia wapi?"

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Wimbo wa kasi mpya umefia wapi?

Samson Mwigamba

MHESHIMIWA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwanza nakupa hongera kwa kutimiza miaka sita ndani ya Ikulu ya Magogoni. Lakini napenda kuwa muwazi kwamba nakupa hiyo hongera kwa desturi ya kitanzania tu lakini kiuhalisia hakuna bado una safari ndefu ya kuleta maisha bora kwa Mtanzania kwani kwa sasa hali ni mabaya sana.


Mheshimiwa rais naomba nikukumbushe kwamba ahadi kubwa mbili ulizoingia nazo kwenye madaraka mwaka 2005 yaani maisha bora kwa kila mtanzania na uongozi wa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, zote zimeyeyuka.Miaka sita ya wewe kuwa madarakani imeshuhudia maisha duni kwa kila mtanzania na kwa kweli Serikali yako imekuwa legelege kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.


Wakati umeingia madarakani mwaka 2005 mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 5, leo tunapoongea uko kwenye asilimia 19 ambazo kimsingi mimi nasema ni asilimia za wataalam wa uchumi. Kwangu mimi raia wa kawaida ambaye si mchumi ninauangalia mfumko wa bei katika jicho hili:Kwamba wakati unaingia madarakani mwaka 2005 tulikuwa tunanunua kilo ya mchele kwa shilingi 800 lakini leo tunaununua mchele huo huo kwa shilingi 2300. Mfumko huu wa bei ni asilimia 150.Vivyo hivyo kama sukari ilikuwa shilingi 600 na leo tunainunua shilingi 2,500 na mahali pengine mpaka shilingi 2,700, mfumko wa bei hapo ni asilimia 230. Vivyo hivyo lita ya mafuta ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi zisizozidi 1,100. Leo tunainunua lita hiyo hiyo kwa shilingi 2,050.Mfumko wa bei hapo ni asilimia 105. Masikini wa kupindukia wasio na uhakika wa mlo mmoja kwa siku walikuwa milioni 11 wakati Kikwete anaingia madarakani 2005, lakini leo wako takriban milioni 13.


Hayo ni machache sana yaliyojiri wakati wa utawala wako wa miaka sita. Hapo sijagusia akiba ya fedha za kigeni ilivyopukutika, sijazungumzia jinsi mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ilivyochakachuliwa, sijazungumzia jinsi uzembe ulivyopoteza maisha ya watanzania wenzetu kupitia mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto, sijazungumzia ombwe la uongozi uliosababishwa kushindwa kuchukua maamuzi, sijagusa ufisadi wa Richmond, Dowans, Stimulus package na mengineyo mengi.


Naomba nikuulize tena mheshimiwa rais, nikupongeze kwa lipi katika miaka yako sita? Mpaka sasa hatujaona barabara za juu ulizoziahidi mwaka 2005.


Mheshimiwa, bado hatujaonyeshwa bayana ajira milioni moja zaidi ya kuona vijana wanaookota chupa za maji zilizotumika mitaani wakiongezeka mithili ya vichaa.Hatujaona shule moja ya kitaifa katika kila wilaya ambayo itachukua wanafunzi kutoka pande mbalimbali za nchi yetu katika jitihada za kukuza uzalendo na umoja wa kitaifa.


Katika hali hii najaribu kutafakari utakapoachia madaraka hapo 2015 ni nini utakumbukwa nacho! Kwa maoni yangu huwezi kwa muda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama ulivyoahidi mwaka jana. Sioni pia uwezekano wa wewe kuweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa huko Mwanza na Bukoba katika muda uliobaki. Sioni uwezekano wa kuhakikisha kila mwanafunzi ana kompyuta yake kabla ya 2015 kama ulivyoahidi, sijaona uwezekano wa kumnunulia bajaj kila mwanamke mjamzito wa nchi hii, na kadhalika. Naona anguko unalokiachia chama chako kama nilivyotabiri mwaka 2007, miaka miwili tu toka ulipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza. Katika utabiri wangu nilisema, mwishoni mwa uongozi wake wa awamu ya nne wananchi watashtuka wataikataa CCM yote kwa kuwa waliaminishwa kwamba hakuna aliyebaki ndani ya CCM anayeweza kuikoa nchi hii zaidi ya Kikwete. Lakini wale tunaokupenda (ambao wewe unadhani ndio tunaokuchukia), hatukuachi hivi hivi. Tunakupa ushauri ili ukichemsha ujilaumu mwenyewe

Sasa nakupa ushauri wa mwisho. Ushauri wangu kwako ni kwamba jiegemeze kwenye katiba mpya. Yule unayemwita Mzee Mkapa, alipoona anaondoka bila cha maana cha kukumbukwa nacho, aliamua kujenga Uwanja mpya wa Taifa wa kisasa. Wewe tengeneza Katiba mpya.

Ninaposema hivyo simaanishi kwamba hauko katika mchakato wa kuandaa katiba mpya. Naelewa sana hilo lakini najua kwamba hiyo unayoitengeneza kwa sasa si katiba mpya bali itakuwa katiba ya zamani za kale katika jina jipya. Ukitaka kuwa na katiba mpya fanya hivi; Katika bunge lijalo peleka bungeni muswaada wa marekebisho ya sheria ya mchakato wa katiba mpya. Katika marekebisho hayo, jiondolee kabisa mamlaka ya kufanya uteuzi wa tume wewe mwenyewe, sekretarieti ya tume wewe mwenyewe, bunge la katiba wewe mwenyewe, hadidu za rejea unawapa tume wewe mwenyewe, ripoti ya tume unaipokea wewe mwenyewe na mchakato wa katiba unafuata utaratibu wa kawaida wa kupeleka miswaada ya sheria bungeni kwa maana kwamba itapitia baraza la mawaziri na kadhalika. Hapa unataka kuleta vurugu isiyo na maana nap engine kuhatarisha amani. Watu wataandamana kupinga mchakato huo na wewe kwa jeuri ya utawala utaagiza askari wako wakawapige. Badala ya kukumbukwa kama Mkapa anavyokumbukwa leo na kila mtanzania anayeingia ndani ya ule uwanja wa taifa wa kisasa, utajikuta unazungumzwa vibaya ndani na nje ya Tanzania.


Kubali wananchi watengeneze katiba yao wenyewe. Mimi si mtaalamu wa sheria lakini natambua kwamba kuna mapendekezo mazuri tu ya Jukwaa la Katiba na vyama vya siasa kama CHADEMA, CUF na NCCR ambao wanajiandaa kukuona.
Achana na jamaa zako kina Wassira, kina Nchimbi, na wenzao wa kwenye chama chako cha mapinduzi. Hao wanakudanganya na wanakutumia kwa maslahi yao ya binafsi.
Hao ni kama wale waliokuwa karibu na rais wa zamani wa Ivory Coast, Laura Gbagbo. Huyu bwana alikuwa anadanganywa na watu wa karibu naye akawa anakomaa na kung’ang’ania Ikulu matokeo yake leo yuko ICC peke yake na hakuna msaidizi wake hata mmoja aliyejitolea kushitakiwa naye.


Hivi sasa una wasaidizi na washauri wengi sana walio karibu nawe kiasi kwamba sisi tulio huku nje unatuona hatuna maana bali ni wachochezi tusioitakia mema serikali “halali iliyoko madarakani”. Lakini wakati unakuja ambapo utatukumbuka wale uliotudharau kama utaendelea kutudharau na ushauri wetu. Hatuna la kufanya zaidi ya kukutakia kila la heri katika maandalizi yako ya kuja kuwa rais mstaafu atakayekuwa anazungumzwa vibaya.Utajikuta hakuna cha maana unachokumbukwa nacho na Watanzania katika utawala wako. Hukujenga uchumi, hukudhibiti ufisadi, hukufanya maamuzi ya mazito kama anavyoagiza, Edward Lowassa.

Kete pekee ambayo ulitaka kujiibulia ujiko ni katiba mpya, lakini kama utakoroga mchakato wake na mchakato wa katiba mpya ukazusha vurugu, utakuwa umeharibu kila kitu. Hakuna atakayekumbuka hata vitu vizuri vichache ulivyovifanya kama kumleta kocha wa timu ya taifa ya mpira, ama kuongeza majengo pale kwenye jingo la Chimwaga na kutengeneza chuo kikuu cha Dodoma.

Jaribu kutafakari lakini Waswahili walisema kama unaona elimu ni ghali jaribu ujinga. Na wewe kama unaona ushauri wetu wachochezi ni mbaya sana, jaribu ushawishi wa wanaojikomba kwako halafu utaona matokeo yake. Kila la heri unaposherehekea miaka sita Ikulu.
Source: Tanzania Daima
 
hiyo kauli mbiu ya zamani imepitwa na wakati kwa sasa kuna tumethubutu, tumeweza, tusonge mbele.
 
Jaribu kutafari kauli mbiu ikichukua muda mrefu sana inachosha ni sawa na matangazo ya biashara ni lazima kubadilisha mara kwa mara ili kuwavutia wateja CCM wako sawa kupunguza kuitumia kauli mbiu hiyo
 
Na ikiwezekana ni vema sana katika siasa kila uchaguzi mkuu kuwa na kauli mbiu yake ili kuwavutia wapiga kura kutokana na mahitaji ya wakati
 
Tanzania ni nchi iliyoshindwa kabisa serikali na chama chake ni mfu nbado kuzikwa ushahidi huu hapa

Mwekezaji Rorya ambaye wananchi hawamjui ,hawakushirikisha anafahamiana na mkuu wa mkoa anachimba dhahabu mpaka amebomoa shule bila kujenga nyingine wala kuwapa usalama watoto wanaoweza kutumbukia kwenye mashimo
Wafungwa 100 keko wanalala selo moja

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amenyang'anya viwanja vya wananchi akawapa wananchi wengine wahanga wa mafuriko
Wachimba kokoto wana mahandaki zaidi ya 25 yenye urefu wa mita sitini yanoyopita chini kwa chini kuvuka barabara ya Bagamoyo Road serikali haijui ,Wanajeshi Kambi ya Kunduchi walipokuwa wakitahadharisha hatari wanasiasa wakazuga matokeo ni hayo

Meatu kunawananchi wameliwa na Simba baada ya nyumba zao kuchomwa moto ili wampishe mwekezaji
Nyamongo Maiti zimetupwa barabarani

Watoto wa shule ya Msingi elfu 9 na ushee wamefutiwa matokeo vinginevyo warudie mwaka kama hawataki huo ndio mwisho wao hakuna cheti cha darasa la saba

Waziri wa Afya anadnganya kwamba madaktari walio kura kiapo kwamba sio madaktari ila ni wanafunzi kwa sababu tuu ni maitern
Serikali ya DARUSO imefutwa na chuo UDSM
Watoto wa mitaani wanafanyiwa kila ajizi toka kulawitiwa,kunajisiwa,kutumiwa kama watumwa mpaka kuhusishwa kwenye ujambazi serikali imelala
Mwigamba unampigia Gita Mbuzi,KIKWETE ni kokotwa hajiwezi hafai ni wakumuondoa leo kabla ya kiama chetu
 
kuna kauli mbiu moja inafanyiwa editing inaingia sokoni very soon.

nyie endeleeni na hiyo zilipendwa.

haiwezekani chama na serikali zizidiwe hata na diamond kwenye kutoa single.
 
kabla ya uchaguzi wa 2005 kauli mbiu ya ccm na jei kei ilikuwa ari mpya ,nguvu mpya na kasi mpya...2010 ikawa ari zaidi,kasi zaidi na nguvu zaidi .....kauli mbiu hii imekufa ,hii ya tumethubutu tumeweza na tunasonga mbele si ya ccm na ya taifa kwa hivyo jei kei anaona soo kuisema hadharani maana hata nafsi yake inamsuta
 
Mbona kila kitu kimeonekana kwani maisha tunayoishi ndo maisha bora aliyokuwa ameahidi na Kasi waliyo nayo ndo waliyomaanisha sema waliompigia kura ndo wakulaumiwa kwa kushindwa kujua uwezo wake na serikali yake kabla ya kumpa nafasi
 
Back
Top Bottom