Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Kuna watu katika nahusiano wanaamini jatika kuagana. Wengine hawaamini katika hilo. Siyo katika kuaga tu bali pia katika kuulizana. Kwa mfano, mtu akitaka kutoka anaweza kukuuliza "unakwenda wapi" au kama anarudi unaweza kumuuliza "unatoka wapi au ulienda wapi". Na upande mwingine wa hilo unajisikiaje kama mwenzio anakuuliza hivyo. Anakuona unajiandaa na anajua utamwambia lakini anashindwa kujizuia "unakwenda wapi tena?" anauliza.
Au kuna kiwango gani cha kuulizana kinaruhusiwa? Kwa mfano, kama unaenda "dukani mara moja" unahaja ya kumwambia mwenzio? Ni mipaka gani ipo kwenye suala la kuagana na kuulizana kabla halijawa kero na kuanza kuleta kisirani?