Mwenyekiti wangu, Mfukuze Nape Uanachama Mara Moja

Mkuu mimi sina mahaba na ccm na hasa rais huyu... Ila anachokifanyA Nape ni Man to Man show...

Yani kifupi anatunishana mabavu na Magufuli live. Hili mimi sijawahi ona.

Laxima anatumwa na nafikiri tayari ana plan B.

Katamka maneno mankali sanaaa... Kifupi anamtuma Na kumfundisha Magufuli kazi.
Thubutu!!
Hata kidogo hawezi cheza mziki wa Magufuli.

Hizo plan alizo nazo zitamtokea puani!!
Hii ni CCM bhanaa,
Ebooo!!
 
kama serikali inafanya mambo yake vizur, y muhangaike na nape acha unafiki .
 
Ewe Mwenyekiti wangu wa chama Chetu pendwa CCM Dk John Magufuli tunaomba kwa kulinda heshima yetu ya serikali na chama tunaomba umfukuze Uanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mbunge wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Mnauye.

Tunashuhudia kijana huyu akikukosea heshima wewe, serikali na chama chetu.
Nape sio mtu wa kwanza kuondolewa kwenye Baraza la Mawaziri.
Walisha ondolewa Mawaziri wengi ambao mimi nimeshuhudia nikiijua siasa kipindi cha JK lakini sijawahi shuhudia Waziri aliye enguliwa kuendelea kuiandama serikali.

Juzi Kitwanga ulimtumbua lakini kwa heshima ya serikali na Chama Kitwanga alikaa kimya, na hakuzungumza chochote.

Tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa wakiondolewa lkn hakuna hata mmoja aliye lalamika na kupiga makelele.

Kwa sasa Nidhamu yaa Nape ktk serikali yako na hata Chama imepungua, ni wazi kwamba huyu ni Mwanachama asiye mtiifu, asiye weza tunza siri za Chama na hata serikali.

Kwa heshima ya chama Chetu na hasa sisi wanachama ambao hatupendezwi na mambo anayofanya Nape tunaomba umvue uanachama.

Nakuomba Mwenyekiti wangu uwe jasiri katika hili, usiogope!!
Kukaa na nyoka ndani ipo siku atakuuma!!

Asante!!

General Mangi
Sasa unamchongea kwa jpm au?
 
Nape mnafiki sana na ni mchumia tumbo. CCM kuweni naye makini. Yaani saivi ndo anajidai anauchungu wakati sio siku zote alikua ccm na matukio yalikua yakifanyika kama kawaida.
 
Naendelea kuwa wa kwanza kutoa comment...

Mengi mtajua wenyewe ccm huko ila nikukumbushe kuna Uzi wako wa juzi humu unaigiza kuhama cdm kwenda ccm afu Maelezo yako yanaonesha we ni mwanachama wa Muda mrefu.
Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu!
hahaha chikuntentema
 
Mkuu katiba imamruhusu, lakini yeye alikuwa Waziri na mjumbe wa baraza la mawaziri ambapo siri kubwa za taifa hujadiliwa.

Lakini kitenda cha yeye kuendelea kuinanga serikali sio nidhamu.

Nina hakika hata wewe pale nyumbani Mzee wako akikosea huwezi simama na kumnanga mbele za wadogo zako, kuna njia za kumfikishia ujumbe.
Ni sawa mkuu mangi lkn kwani kwa hali ilivyokuwa Nape alikuwa sahihi kwa alichofanya. Kilichotakiwa nikwamba Mzee angepokea ripoti ya Nape nakupiga kimya bila kutolea maamuzi hata kwa miaka kadhaa kusingekuwepo na wakumuliza. Sasa watu wengi wamekuwa wakimtetea Nape kulingana na hali halisi kwani haingii akilini aliyekuwa akimkimbiza mwizi nakumkamata kisha kumfikisha kwenye vyombo vya usalama halafu yeye ndio akaswekwa rumande kisha mwizi akaachiwa huru. Inauma sana.
 
Back
Top Bottom