Mwenyekiti wa shirikisho LA Vyuo vikuu nchini na ambaye pia ni Rais wa Kitivo cha Elimu (college of Education) chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Leo ameponea chupuchupu baada ya kuonekana maeneo ya maandamano na huku akijulikana kuwa ni msaliti kwa kukaa kimya muda mrefu bila kutolea tamko suala la vyuo vikuu kutopelekewa pesa za malazi na chakula ukizingatia kuwa yeye ndiye anapaswa kuzungumza kwa niaba ya chuo na vyuo vyote Tanzania kama Rais. Suala lingine ni kufanya ufisadi wa pesa ya serikali ya Wanafunzi na kununua magari mawili. Amekimbizwa na kushambuliwa kwa mawe ambapo alinusuriwa kwa kufungiwa chumbani na baadae kuondolewa maeneo ya chuo chini ya ulinzi mkali wa polisi. maandamano yanaendelea kesho baada ya majibu kutoka kwa Waziri mkuu kutoridhisha