Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ana maslahi gani hapa?

Sinai

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
288
47
Katika gazeti la Tanzania Daima, kuna habari inamhusu Jenister Mhagama ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge huduma za jamii. Huyu mama kama mwenyekiti, alikuwa anajaribu kuizuia kamati yake isitembelee kiwanda cha Jambo Plastics, swali langu ni je huyu mama anamaslahi gani na hiki kiwanda? Kwanini ajaribu kufanya jaribio la kuzuia wabunge wasitembelee hicho kiwanda? Au ndo yale yale ya CCM kulinda mafisadi? Naomba kutoa hoja!
 
Yeye mwenyewe ni mwenyekiti, halafu anazuia. Maslahi Binafsi, hao ndio Chama cha Mafisadi.:A S 103:
 
hapana aliyekuwa anazuia ni Waziri Gaudence Kabaka na yy jenister mhagama akakomaa hadi wakaenda kutembelea kiwanda!
 
huyu mama jamani hata kama yupo CCM ni mchapakazi wa ukweli na ana uchungu wa kweli na hii nchi.. nimejaribu kufuatilia michango yake mingi mjengoni ni ya ukweli na yenye mantiki. siamini kama anaweza kufanya kitu kama hicho
 
Katika gazeti la Tanzania Daima, kuna habari inamhusu Jenister Mhagama ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge huduma za jamii. Huyu mama kama mwenyekiti, alikuwa anajaribu kuizuia kamati yake isitembelee kiwanda cha Jambo Plastics, swali langu ni je huyu mama anamaslahi gani na hiki kiwanda? Kwanini ajaribu kufanya jaribio la kuzuia wabunge wasitembelee hicho kiwanda? Au ndo yale yale ya CCM kulinda mafisadi? Naomba kutoa hoja!

Ndugu nadhani umenukuu vibaya, Jenniste na kamati yake walikuwa WANAZUIWA na Waziri wa Kazi, Gaudencia Kabaka. Lakini Jennister na wajumbe wa kamati yake wakakomaa mpaka kikaeleka. Nadhani kuna dalili za mlungula kati ya ofisi ya waziri kabaka na wakubwa wa kampuni ya Jambo plastic.
 
Back
Top Bottom