Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa DSM amtolea Uvivu Zakaria Kakobe

Naona mnatoleana povu tu! Hapa dini hapa siasa basi kila moja apambane na hali yake kiki zingine muache tu
 
Nakumbuka Nchimbi alimuita Kibwetere...Dr Nchimbi alikuwa na sifa zote za kuwa raisi..ni zao halisi la UVCCM..laana ya Askofu kila anachofanya anapwaya
 
Chama hiki siku hizi kinaokota kila mtu na kumpa cheo.
Mpuuzi huyu hata hajui anachozungumza wala hajui Kakobe kasema nini kadandia treni.
Ohh mara anayejiita Askofu. Mpuuzi huyu kwani hajui Kakobe ni askofu?
Wamezoea kusifiwa na akina Pengo ambao wao akiingia rais Mwisilamu umkosoa asubuhi na jioni lakini akiingia mkatoliki wanayefanya bidii yote awe mkatoliki, umtumia kama remote.
Tuachieni Kakobe. Kasema rais atubu. Period. Hiyo ndio kazi ya nabii yeyote. Kupeleka meseji kwa kiongozi akatae, akute ya kumkuta. Asilaumiwe mtu.
 
Amesema, Aende akatubu apate utakaso.
Sheria ya unabii haulembwi humwelekea mhusika. Aliyeambiwa atubu ni rais sasa nyie endeleeni na siasa midomoni mwenu mpuuzie kauli hii ya Kakobe kwa kiongozi wa nchi ndipo mtakapoona mziki wa Mungu.
Pharaoh alipewa ujumbe mfupi tu "Waachie wana wa Israel waende wakanitumikie " akakaidi mziki aliuona.
Mungu anapotoa ujumbe kwa kiongozi mkuu mfalme wa nchi huwa hahitaji mzaha wala kebehi. Ninyi endeleeni kumshambulia huyo kakobe majibu mtayasikia. Uwanja uko wazi. Ikibidi kila kiongozi wa ccm amshambulie itapendeza.
 
Ndiyo ni kweli kuwa kila kila mamlaka zimetolewa na Mungu, lakini sio kweli kwamba kila mamlaka zimeletwa ili kuwa baraka kwa watawaliwa bali ana zileta ili mpate funzo la kumchagua yule ambaye kwake halikuwa chaguo Mungu bali limekuwa chaguo lenu wanadamu. Kwa wale wasomaji wa maandiko someni kwenye kitabu cha Samweli mtakuta watawala ambao Mungu ali wakubali watawale ili wanadamu wajutie ku ukataa uchaguzi wa Mungu na kujifanyia chaguzi zao kama wanadamu. Kwa ufupi tu ni kwamba muasisi wa demokrasia wa kweli ni Mungu, yeye alazinishi umkubali bali amekuachia uhuru umkubali kwake ni vema na pia ukimkataa hakufanyii lolote lilo baya bali bado ataendelea ataendelea kukupatia pumzi ili uendelee kuishi.
 
Nabiii Eliya ali simama mbele ya mfalme na kumueleza makosa yake na kwamba kutokana na makosa hayo mvua haita nyesha juu wa nchi kwa miaka kadhaa na ndivyo ilivyo kuwa. Ni jukumu la watumishi wa Mungu kuwaeleza viongozi wetu ukweli kama wanaona kuwa kuna mapungufu yoyote yale kutoka kwa hao Viongozi. Kakobe amesimamia majukumu yake kama kiongozi wa dini.
 
Sawa kakobe lakini usishangae labda unatafuta waumini
Maskini humjui Kakobe wewe . Ana makanisa nchi nzima na yote yana waumini wa kutosha.. hana shida na waumini. Pale anakemea dhambi. Akiona hata mshirika ametenda dhambi ya uasherati anatimua hana double standard. Nenda kanisani kwake uvae tu kwa adabu halafu ukashuhudie chunguza mambo kwanza halafu uje useme pumba zako hapa...
 
Lkn hayahusu kutaja majina ya viongozi wa kisiasa na kuwaamrisha wafanye jambo fulani.

Imani za kikristo ni pamoja na kutubu/kuungama je anajuaje km hajaungama au mpk akafanye hivyo kanisani kwake?

Magufuli sio muumini wa kanisa lake kwanini amtake kutubu hadharani kn kwamba ni muumini wake?
Hehee ndugu unajua kiswahili wewe?? Kakobe amesema kwamba atubu hajamwambia atubu kanisani kwake wala hadharani. Kutubu kunaambatana n kujuta n kuacha.. Sio unatubu n kurudia yaleyale.. LUGHA NYEPESI HAIHITAJI HATA KWENDA SHULE...
 
Mkuu kwa upande wangu gwajima sijawahi hesabu kama ni mchungaji,samahani ka ww ni muumini wake.Wanachokifanya akina gwajima,pengo,shoo,kakobe na mashehe wanaojifanya kuunga au kupinga vitu flani ktk nchi hii wengi ni SIASA.Hakuna cha Mungu anayetumika hapo na wanakufuru kutumia madhabau zao kufanyia siasa huku wakinukuu maandiko matakatifu na Kumtaja Mungu.Hao akina kakobe na gwajima ni timu ukawa na rangi zao zilionekana 2015 na akina pengo and co hao ni CCM.Hawa wote wanatetea pande zao kwa kutumia maandiko kitu ambacho sio sahihi.

Tanzania tuna viongoz wa dini fake,wanasiasa fake Yani kila kitu fake.Na ukifuatilia kwa karibu,atakachoongea gwajima au kakobe huwa sahihi kwa chadema na atakachoongea pengo huwa sahihi kwa CCM lkn ubaya wake wote wanajifanya wanawasemea watanzania kwa kuwapa maandiko ya kimungu
Nonsense
 
Back
Top Bottom