Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, tajiri wa Singida United anagawa rushwa kufuru

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
335
495
Tajiri na mfadhili wa Timu ya Singida United ambaye ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Yusuf Mwandami anafanya kufuru ya kugawa Rushwa kubwa kubwa kuhakikisha anashinda uenyekiti wa CCM mkoa wa Singida. Uchaguzi wa kumpata mwenyekiti Mpya wa Mkoa huo unatarajiwa kufanyika tarehe 5/12/2017 mjini Singida.

Mwandami ambaye anafahamika Kwa jina la Musukuma na mwenye ukwasi wa kutisha ndiye mfadhili mkuu wa Timu ya Singida united na Tajiri wa mgodi wa madini wilayani Ikungi.

Taarifa za Mwandami kucheza rafu za Rushwa zimelalamikiwa na wanachama wa CCM wakihoji matumizi hayo makubwa ya fedha ni sawa na mtu kukinunua Chama na Kutokana na uwezo wake wa kifedha. Mwandami anadaiwa kuwaita makatibu wa CCM wa kila wilaya na kuwapa Sh Milioni Tano kila mmoja kuhakikisha anashinda uchaguzi huo Kwa gharama yeyote.

Taarifa za uhakika toka mkoani Singida ni kwamba jana Jumatatu Majira ya mchana Mwandami aliitwa na Uongozi wa CCM Mkoa wa Singida kuhojiwa baada ya TAKUKURU kupeleka taarifa kwamba kuna mgombea Anagawa Rushwa Kwa Viongozi wa wilaya na Kata ambao ndiyo wapiga kura wa uchaguzi huo. Jana hiyo mchana Mwandami akiwa ndani ya gari ya kifahari aina ya JEEP nyekundu alifika ofisi za CCM Mkoa na kuhojiwa Kwa Saa1 , haijajulikana yaliyozungumzwa ndani ya kikao hicho kilichohudhuriwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa, katibu wa CCM Mkoa na baadhi ya Viongozi wa TAKUKURU. Baadaye Mwandami alitoka na kuendelea na mipango yake.

Katika hali isiyo ya kawaida Mwandami alikamatwa Tena na TAKUKURU Majira ya usiku baada ya kunaswa Tena akigawa Rushwa na wapambe wake Kwenye nyumba za kulala wageni mjini Singida. Inadaiwa Viongozi wengi wa kata kuanzia Makatibu, wenyeviti na makatibu wenezi wa kata waliitwa waje kulala mjini na kulipwa gharama zote Kwa ajili ya mipango ya usiku kuamkia siku ya uchaguzi. Taarifa za uhakika Kambi ya Viongozi wa kata ilikuwa maeneo ya KIRIMA BAR na wajumbe walitawanywa kulala maeneo ya karibu karibu na KIRIMA Kwa ajili kufanikisha miadi yao.

Baada ya Mwandami kushikiliwa nyakati za usiku inadaiwa alihojiwa Kwa saa 2 na maafisa wa TAKUKURU na baadaye kuachiwa, haijajulikana nini kilitokea katika mahojiano hayo.

Baadhi ya wagombea ambao hawana fedha wamebaki wanyonge wakisubiri kudra za Mwenyezi Mungu Kwenye Ukumbi wa kupiga kura. Wagombea wenzake wamekata tamaa Kutokana na ukweli kwamba wajumbe Hawana muda kumsikiliza mgombea asiye na fedha na wengi anakimbilia Kwa Mwandami mwenye rutuba mfukoni. Moja ya wagombea ambaye ameonekana akitembea Kwa miguu na kupanda Bajaji ili kufanya harakati za kampeni amejikatia tamaa huku akijipa matumaini kwamba CCM ya Magufuli haiwezi kuwekwa mfukoni na Mwandami.

Rushwa za yusuf Mwandami zinajulikana Kwa wajumbe wengi na wanasema kweli jamaa anautaka uenyekiti wa Mkoa Kwa nguvu zote na amejipanga kisawasawa.

Taarifa za uchaguzi zitakazojiri huko Singida tutashea hapahapa, ila ukweli Boss wa Singida united ameshashinda Kabla ya kura kupigwa.
 
Huyu Msukuma kwa uendeshaji kule wa Sngida Utd ataisaidia Ccm na Singida yake..karibu mawazo mapya jaribu Mamii..
 
Inaitwa expansion joint
Ipi kati ya hizi?
1.
e7cf4865de23df51e9100c1055b3f120.jpg


2.
2d290a67c9574c3647969aea00c74546.jpg
 
Safi sana, CCM=Chama cha Manunuzi.

Kama Baba kabisa anatamka kwa wengine kwamba "nakutaka kwa gharama yeyote, sema unachotaka nitakupa ili uje huku" unategemea watoto wataiga nini?

Hakuna msafi CCM.
Hebu tuwekee hiyo clip mkuu nasi tuione.!
 
Hii inashangaza mtoa RUSHWA badala ya kukamatwa wahusika wanaenda kumlalamikia kwa uongozi wa Ccm!!
 
Fedha ndo rasilimali muhim kwenye SIASA.
Nao wasake pesa sio kulialia.
Unadhan bila pesa JPM angeshinda?Mikutano yake ilikuwa Live,sasa si gharama hizo?
 
Back
Top Bottom