Mwenyekiti wa CCM Mkoa Arusha na Katibu Mwenezi wa Mkoa Wajiuzulu na kuhamia CHADEMA

Nape ananikumbusha yule waziri wa ulinzi wa Sadam,alikuwa anapiga propaganda mpaka dakika ya mwisho Wamarekani wanaingia vitani Iraq.

Siyo wanaingia vitani Mkuu, mpaka wanateka lile jengo alilokuwa anapigia propaganda na yeye akiwemo. Nape hawezi kuwa na ujasiri kama wake! Thubutu!
 
Huyu mwenyekiti tungemshangaa kama asingemuunga mkono ENL. ENL alimsaidia sana kukaa hapo alipo. Kuna watu kwa kweli wasipomuunga mkono ENL tutawashangaa. Arusha ni mkoa wake msipomuunga mkono tutawashangaa. Lakini Mbona wanaohama ni Arusha tu jamani. Halafu M/Kiti ni mtu mmoja tu bado haina effect sana kwa CCM na bila ENL huyo Nangoro asingepita tena CCM hivyo alikuwa hana jinsi. Bado ni sanaa tu zinaendelea. Ila UKAWA kuweni macho hizi tamaa kuna siku zitawatokea puani msizoezoe. CCM inasumbuliwa na ufisadi kwa sababu ya kuzoazoa huko nyuma wafanyabiashara wenye hela , wajanja wa kuongea n.k. Wengine ni watu wa mfumo.
 
Kama ganda la mua...utamu ukiisha tunatema then kipande kingine kinafata..teh
 
Kweli! Kifo cha nyani miti yote hutereza. Hata ukijifariji. Kifo kinabaki palepale. Usijifariji kufanikiwa kwa kupata wageni wengi, kwa kauli ya MGENI njo wenyeji wapone! Utaendekea kufa tu kwan hats hao wageni wanataka chocchote.siku wakikosa wataenda pengine!!!
 
Nimelazimika kuandika baada ya kuona mwanachama mpya kutoka CCM, aliyekuwa Katibu mwenezi wa mkoa wa CCM akisema CDM ndo mpango mzima kwa sasa nikajiuliza hiki ni chama gani katika nchi gani?

Na hapa pia nimeona watu wengi wakiandika hicho kitu najiuliza CDM ni mdudu gani?

Tusiwe wajinga wa kulazimisha vifupi vya maneno ambavyo havipo?
 
Nimelazimika kuandika baada ya kuona mwanachama mpya kutoka CCM, aliyekuwa katibu mwenezi wa mkoa wa ccm akisema CDM ndo mpango mzima kwa sasa nikajiuliza hiki ni chama gani katika nchi gani?!!


Na hapa pia nimeona watu wengi wakiandika hicho kitu najiuliza CDM ni mdudu gani?!!


Tusiwe wajinga wa kulazimisha vifupi vya maneno ambavyo havipo??

Mkuu, huwa nashindwa kuelewa watu wanaofupisha neno ambalo tayari ni kifupi cha maneno. Na wako wengi sana hapa jamvini.

Kwao wao yote ni sawa/si shida.
 
Hili ni tatizo mpaka hata kwa viongozi waandamizi wa CHADEMA, wanashindwa kuelewa kuwa neno CHADEMA tayari ni kifupisho cha Chama cha Maendeleo na Demokrasia.Nimeona mabandiko kadhaa ya makada wa CHADEMA huku wakitumia CDM,hawako makini kabisa maana huwezi kufupisha neno ambalo lishafupishwa labda kama unamuandikia demu wako.
 
Ukiona huelewi kwa nini watu wanafupisha maneno hivyo ujue umri wako umesogea sasa.
 
Hili ni tatizo mpaka hata kwa viongozi waandamizi wa CHADEMA, wanashindwa kuelewa kuwa neno CHADEMA tayari ni kifupisho cha Chama cha Maendeleo na Demokrasia.Nimeona mabandiko kadhaa ya makada wa CHADEMA huku wakitumia CDM,hawako makini kabisa maana huwezi kufupisha neno ambalo lishafupishwa labda kama unamuandikia demu wako.

Halafu wateule wao katika nafasi mbalimbali za uongozi wakujaza hivo na kisha kuenguliwa wa kwanza kulalamika tumeonewa!!

Umakini sijui kutokuelewa mi hata siwaelewi mkuu
 
Back
Top Bottom