Mwenyekiti wa CCM huko Usangi (Mwanga) ameamua kujiuzulu

Waache waende zao. CCM ina hazina ya watu wasafi na waadilifu.
hakika unachokesema ni ukweli mtupu.
ila tu zingatia yafuatayo:biashara ya dawa za kulevya nchini,biashara haramu ya meno ya tembo,ufisadi na machafu mengine mengi yanayoliingiza taifa ktk hasara kubwa na kulipatia aibu,yanafanyika chini ya himaya ya watendaji wa serikali ya CCM.

embu jikumbushe kwanza na taarifa hii,i hope kingereza kinapanda : Corrupt officials and Chinese gangs destroy Tanzania's elephant population.
 
Tatizo ni kuwa; Walilikoroga wenyewe. Kuweka majina mfukoni halafu unapelekea watu kuwa taka msitake majina ni haya hapa.
Watu wakamtaarifu mapema kuwa ; Tuna imani naye. Akakataa, akidhani bado watu ni wale waleee wa zidumu fikra sahihi. Sasa, ayapokee mafuriko au ayazuie tu yamfurikie.
Lowasa ni Top. Ikulu ataingia saa 2 asubuhiiii 25 Oktoba
 
Hao wajiuzuru tu yakhe, CCM inajua kinachoendelea/kitachoendelea kwa ccm mikoa ya kilimanjaro na arusha. wakitaka wajuizuru wote kwa pamoja au wapangiane ratiba mmojammoja kila siku sawa tu. Lakini mwenyeakili anajua kwamba hadi sasa ccm haijapoteza hata wanachama 1000 kati ya wanachama zaidi ya milioni 6 nchi nzima.

Ndiyo mkuu CCM yetu haijatetereka hata chembe maana mbinu tunazo na lile bao la mkono tulilozoea litahusika!! Kwi! Kwi! Kwi! Ila Mkuu tujipe moyo tu ila khali sio nzuri
 
Naomba nichangie post hii iwekwe kwenye kumbukumbu! Silaha ya mwisho kabisa ya CCM ni Kama ifuatavyo; wameshajipanga vilivyo kuanzisha fujo kubwa sana , na kupindua matokeo , then fujo itaanza kutoka wafuasi wa ukawa; fujo itaongezwa chumvi na media ; Jeshi la Wananchi na Polisi litapiga sana watu , itatangazwa hali ya hatari siku 3 , ndani ya siku 3 alieshindwa ataapishwa!!sijui nini kitafuata!!
 
Nape anasingizia eti wana sababu zao, nakudai eti ni marafiki wa Lowasa,yaani hataki kuhamini
kama chama kinawafia mikononi!!!!
 
Hao wajiuzuru tu yakhe, CCM inajua kinachoendelea/kitachoendelea kwa ccm mikoa ya kilimanjaro na arusha. wakitaka wajuizuru wote kwa pamoja au wapangiane ratiba mmojammoja kila siku sawa tu. Lakini mwenyeakili anajua kwamba hadi sasa ccm haijapoteza hata wanachama 1000 kati ya wanachama zaidi ya milioni 6 nchi nzima.

Kwa hiyo kwa akili zako ukiambiwa mwenyekiti kaondoka unadhani ataondoka mwenyewe??? Na pia kati ya wanachama 6m.
Wa Ccm wakitoka 1000 bado wanatabaki 6million tu???? TAFAKARI
 
Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Kighare, Usangi, wilaya ya Mwanga huko mkoani Kilimanjaro Abdallah Kiluvia ameamua kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa CCM wa eneo hilo kwa madai ya kuchoshwa na siasa chafu za CCM na Ukandamizaji wa hali ya juu ndani ya CCM kuanzia ngazi ya juu mpaka ya chini kabisa.

Tayari katibu wa CCM wa eneo hilo Mr.Gaga amethibitisha hilo kwa kukiri kupokea barua ya kujiuzulu mwenyekiti wake.
Mpaka sasa haijafahamika anataka kuhamia chama gani ila tetesi zinasema siku ya Jumatatu atasema Chama anachotaka kuhamia mara atakapofanya kikao na wazee wa huko Usangi.

Mwenyekiti huyo alikuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana kisiasa katika wilaya ya Mwanga, na kujiuzuru kwake huenda kukachangia kwa sehemu kubwa sana CCM kupoteza viti vya udiwani na ubunge katika jimbo la Mwanga kwa mara ya kwanza toka kupata uhuru

Eneo la Usangi ndio mahali ambako wanasiasa wengi wa siku nyingi wa TANU na CCM katika mkoa wa Kilimanjaro wanatokea akiwemo Marehemu Peter Kisumo alizaliwa, kuisha na kuzikwa jana. Pia mbunge wa sasa wa Mwanga, Professa Maghembe anatokea eneo hilo na Pia hata Waziri mkuu mstaafu Cleopa Msuya anatokea pia hapo Usangi.
Na David Mathayo, Rose Migiro nk
 
Back
Top Bottom