Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,385
- 27,604
Uchaguzi umekwisha na matokeo yaneshatoka (yawe halali au sio hilo sio dhumuni la post hii).
Lakini kuna maeneo bado kuna manung'uniko makubwa, na hapa ntazungunzia kwa sehemu nilisikia na kuona. Siku moja kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi nilikuwa Mwanza.
Na nisewe wazi nilijumuika na wana mwanza kwenye kushauriana kupata viongozi bora. Upepo wa John Pambalu ambaye alikuwa anagombea jimbo la nyamagana haukuwa mbaya sana, ila ndio kama tunavyojua mambo ya uchaguzi yalivyo.
Lakini kubwa zaidi lililonisikitisha ni hili la mawakala kutokupata pesa zao baada ya uchaguzi hapa nazungumzia kwa wale ambao nina ushahidi nao, huko kwingine sijui.
John Pambalu nakuomba upokee simu za hawa mawakala na umalizane nao, uwalipe pesa zao maisha yaendelee. Hili jambo linataka kukutia doa, kwa kuwa wapo waliopanga kwenda kulalamika kwa waandishi wa habari.
Lakini pia unaweza puuzia hili jambo na kukanusha na watu wa mitandaoni wakakuelewa, ila wale vijana utawaumiza sana mioyoni mwao kwa kuwa ukweli unaujua.
Ninakuomba sana kwa unyenyekevu mkubwa watafute umalizane nao, najua kwenye kampeni umetumia pesa nyingi lakini jitahidi kuongea nao na kumalizana nao kwa kuwa wale wana ndugu, jamaa na marafiki na wakisikia habari hizi unaweza kupoteza credibility uliyonayo.
Kwa nini nimekuja humu sababu hata simu zao hutaki kupokea na wakipiga kwa katibu wanaishia kuzungushwa tu wanaambiwa warudi kwako, leo ni siku ya 6 na bado muafaka wa pesa zao haujapatikana.
Nawasilisha