Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,495
2,740
Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kagera wametoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao kumtukana na kumbeza Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kuwa muda wao kuendelea kufanya hivyo sasa umekwisha.

Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Buruhan wakati wa ziara yake wilayani Ngara alipokutana na viongozi pamoja na wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge Aprili 16, Mwaka huu.

Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu wanaotumia mitandao kumchafua Rais Samia pamoja na viongozi wengi huku wengine wakiwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambapo amelitaka jeshi la polisi kutowatafuta watu hao pindi watakapopotezwa.

=========================​
Chairperson of UVCCM Kagera, Faris Buruhan address that the police should not bother to look for those who insult the President online incase they go missing.

The CCM youth union in the Kagera region has issued a warning to individuals using social media to insult and abuse the President Samia and her aides, stating that their time to continue doing so has come to an end.

The warning was issued by the Chairperson of UVCCM Kagera, Faris Buruhan, during his visit to Ngara district where he met with leaders and residents in the jurisdiction of the Rulenge township on April 16, this year.

He mentioned that there has been a trend of people using social media to tarnish the image of President Samia and other leaders, some of whom are within the ranks of the CCM. He urged the police not to search for these individuals should they go missing.

However, the public has reacted strongly, interpreting this statement as an attempt to suppress freedom of expression and public opinion. Many view it as a government official issuing a threat to the public, raising concerns that the government may be involved in the cases of several prominent individuals who have gone missing recently, including journalists and opposition figures.

Pia soma
- Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

- Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali
 
UVCCM mjitafakari. Hizi siasa za kupotezana sio maono ya mwenyekiti Mama Samia. Mama hana siasa za kipumbavu kama hizi.

@sirallawi
#WasafiDigital
Suala hili la kupoteza watu wanaokosoa utawala uliopo hapa Tanzania siyo kitu kigeni au kitu kipya, lipo tangu enzi na enzi. Huyu Mwenyekiti alichoongea ni kitu sahihi na cha kweli, alichofanya ni kuwakumbusha tu watu ktk nchi hii. Asilaumie yeye huyo Mwenyekiti, bali wa kulaumiwa ni kile Chama chake kilichoasisi mambo haya ya kutekana, kutesana, kuwekeana sumu, kuuana, n. k.

RIP Mchungaji Christopher Mtikila
 
Viongozi wa UVCCM Kagera wametoa Onyo Kwa watu wote wanaomtusi Rais Samia Kwa kuwataka Polisi wasijihangaishe kuwatafuta watu ambao Wanaomtukana Rais Samia endapo watapotea.

Onyo Hilo limekuja huku pia Waziri wa mambo ya Ndani akionya watu waache matusi na wafanye siasa vinginevyo hatua Kali zitachukuliwa.

UVCCM wameapa kumlinda Rais na Mwenyekiti wao Kwa gharama zozote.

My Take
Naunga mkono hoja,matusi Kwa Viongozi sio siasa, wahusika washughulikiwe.
 
Viongozi wa UVCCM Kagera wametoa Onyo Kwa watu wote wanaomtusi Rais Samia Kwa kuwataka Polisi wasijihangaishe kuwatafuta watu ambao Wanaomtukana Rais Samia endapo watapotea.

Onyo Hilo limekuja huku pia Waziri wa mambo ya Ndani akionya watu waache matusi na wafanye siasa vinginevyo hatua Kali zitachukuliwa.

My Take
Naunga mkono hoja,matusi Kwa Viongozi sio siasa, wahusika washughulikiwe.
Wao wanawapangia polisi nini cha kufanya? Hawajui mipaka yao? Kumlinda rais si kazi yao, kuna vyombo vya usalama nchini.
Kumlinda kisiasa wanaweza pambana kwa hoja lakin si kufikia mahali ku commit sucha act otherwise na wao wakianza kupotezwa wasililie mahali. Tunatengeneza bomu mbeleni
 
SOURCE WASAFI TV

Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kagera wametoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao kumtukana na kumbeza Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kuwa muda wao kuendelea kufanya hivyo sasa umekwisha.

Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Buruhan wakati wa ziara yake wilayani Ngara alipokutana na viongozi pamoja na wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge Aprili 16, Mwaka huu.

Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu wanaotumia mitandao kumchafua Rais Samia pamoja na viongozi wengi huku wengine wakiwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambapo amelitaka jeshi la polisi kutowatafuta watu hao pindi watakapopotezwa.

Pia soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Akemewe mara moja, hana mandate hiyo. Viko vyombo vya usalama. Yeye bi uvccm amabki kwenye siasa. Otherwise litainuka kundi la kumaliza ccm ndipo tutatengeneza vita vya wenyewe kwa wenyewe. Afunge domo lake mara moja
 
SOURCE WASAFI TV

Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kagera wametoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao kumtukana na kumbeza Rais Samia pamoja na wasaidizi wake kuwa muda wao kuendelea kufanya hivyo sasa umekwisha.

Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Buruhan wakati wa ziara yake wilayani Ngara alipokutana na viongozi pamoja na wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge Aprili 16, Mwaka huu.

Amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu wanaotumia mitandao kumchafua Rais Samia pamoja na viongozi wengi huku wengine wakiwa ni miongoni mwa viongozi wa CCM ambapo amelitaka jeshi la polisi kutowatafuta watu hao pindi watakapopotezwa.

Pia soma Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Kajinga kweli kwahiyo na kenyewe kakipotea polisi wasikatafute
 
Back
Top Bottom