Mwenye uelewa gari langu linapandisha temperature katika engine

Thermostat laweza kuwa tatizo. Cheki na fundi aifungue aangalie kwa maji moto kama inafungua ama siyo.
 
Kuna kitu kinaitwa cylinder head katika engine ndani yake kuna gasket hiyo inaweza ikawa imeungua au hiyo cylinder head njia zake zimeliwa na maji ya chumvi
 
Yapata miezi mi3 sasa gari langu linatatizo ya engine kupandisha joto, ni Toyota spacio hii ilitokea baada ya kubadilisha rejeta ikawa unapotembea kama umbali wa 45 au 40km unaona inatokea alarm ya high temperature ktk dash board. Nikaipeleka kwa fundi tena akasema tubadilishe mfuniko wa rejeta ok tukabadilisha tatizo likawa linaendelea, nikampelekea tena akasema tubadilishe sensor ya temperature ok tukabadilisha lakni tatizo bado linaendelea sasa je mwenye ujuzi gari langu lina tatizo gani?
Je inasumbuwa kuwaka tofauti na awali kabla ya tatizo au inawaka kawaida ?
 
Pole sana mkuu.huna haja ya kuhangaika na kutafuta tiba hapo kwa uelewa wangu kulingana na maelezo yako shida au utatuzi upo sehem mbili tuu.

Kwanza kwenye upande wa rejeta.

Hapo yaweza kuwa rejeta iliyoweka ni kimeo.
Inaweza ikawa baadhi ya njia zimeziba,au rejeta yenyewe chafu kwa nje so inazuia hewa kupita vizuri,au imepukutika kwa nje.


Fan ya kupooza.kwa kuwa hiyo gari inatumia fen ya umeme na umesema kuwa chanzo cha rejera kutoboka ni baada ya panga la fen kukatika ndio likatoboa rejeta hivyo ulibadilisha kuna mambo haya ya kuzingatia.

Aidha kama ni panga peke yake ndio ulibadili unaweza ukawa umeweka tofauti au lina panga chache??.

Au mota yenyewe ni tofauti na ya mwanzo hapo kama ulibadilisha na mota.

Mwisho angalia kama ulibadili mota usije ukawa umeiinga kinyume. Baada ya kuvuta hewa nje kutoka mbele ya gari kuingiza ndani yenyewe inatoa hewa ya joto ndani na kuipuliza nje hivyo hewa ya joto badala ya kuyapooza maji inayapasha moto.

Ukitaka kufaham juu ya mzunguko wa feni kama upo sahihi basi.washa gari feni ikiwa inazunguka chukua kipande cha karatasi weka mbele ya rejeta or condeser ya ac hapo inatakiwa karatasi ivutiwe ndani itanasa ukiona inadondoka ujue fen inazunguka kinyume.
Hapo tatizo lisipoisha badilisha fundi.
 
Back
Top Bottom