Mwenye uelewa anisaidie tofauti ya raia na Mwananchi

Jiulize kwenye Passport kwanini hua wanaandika

URAIA- Mtanzania
kwanini wasiandike

MWANANCHI - Mtanzania?
Hapo utapata jibu,

Kwa uelewa wangu "Mwananchi" ni RESIDENT na "Raia" ni kama mtu mwenye Passport au id kua yeye ni mtanzania "Tanzanian" in his/her Nationality

Wajuzi wataongezea zaidi,nimeelezea kwa uelewa wangu tuu.

Resident ni mkaazi, Mwananchi ni Citizen. tafsiri si si si
 
Jiulize kwenye Passport kwanini hua wanaandika

URAIA- Mtanzania
kwanini wasiandike

MWANANCHI - Mtanzania?
Hapo utapata jibu,

Kwa uelewa wangu "Mwananchi" ni RESIDENT na "Raia" ni kama mtu mwenye Passport au id kua yeye ni mtanzania "Tanzanian" in his/her Nationality

Wajuzi wataongezea zaidi,nimeelezea kwa uelewa wangu tuu.

Kinacho ni changanya ni pale wanapo sema wananchi wenye hasira kali wamewap4a majambaz na kuwa ua.Kwa hyo hao siyo wa tz wa zawa?
 
Mara nyingi maneno haya mawili yanataja watu walewale lakini inawezekana kuna tofauti. Mtazamo ni tofauti.

"Raia" inaangalia upande wa kisheria: je mtu fulani anatosheleza masharti ya kuitwa "raia" wa nchi fulani, pamoja na haki (kama kura, haki ya kusikilizwa na kulalamika, kutetewa na ubalozi wake akiwa ugenini) na wajibu (kwa mfano kwenda jeshini katika nchi nyingi, kushiriki katika wajibu fulani) za uraia.

"Mwananachi" inatazama zaidi tabia ya kuishi (kwa muda usio mfupi) katika nchi au sehemu fulani, kuwa mwenyeji wa huko.
Kwa kawaida hakuna utaratibu wa kisheria au masharti kamili ni nani anayeweza kuitwa "mwananchi", tofauti na "raia".

Unaweza kuishi katika nchi nyingine hadi umekuwa mwenyeji na kila mtu anakutazama kuwa mwananchi lakini bado hujafanya hatua ya kuomba uraia.

Mara nyingi tofauti hii si tatizo lakini kutegemeana na siasa ya nchi fulani tatizo linaweza kutokea.
Kwa mfano huko Marekani Bwana Trump anajaribu kuwaondoa watu waliokuwa wenyeji kwa muda mrefu hata kizazi cha pili kwa sababu zamani waliingia kutoka Meksiko, si raia.
Nakumbuka majadiliano sawa kuhusu Banamulenge nchini Kongo waliokuwa wenyeji na wananchi kwa vizazi lakini walinyimwa uraia na kutangazwa kuwa Warwanda kwa sababu za ukabila na siasa.
 
Jiulize kwenye Passport kwanini hua wanaandika

URAIA- Mtanzania
kwanini wasiandike

MWANANCHI - Mtanzania?
Hapo utapata jibu,

Kwa uelewa wangu "Mwananchi" ni RESIDENT na "Raia" ni kama mtu mwenye Passport au id kua yeye ni mtanzania "Tanzanian" in his/her Nationality

Wajuzi wataongezea zaidi,nimeelezea kwa uelewa wangu tuu.

Kwahiyo asiyekuwa na passport sio raia?
 
Wanajeshi wamefanya fujo URAINI.....

UTAIFA/=Mtanzania
Civilian = RAIA
Military = wanajeshi
Inhabitants = wakazi
Citizens =Wananchi
, kiswahili kimeshiba misamiati
Ni lazima kutafsiri? Basi ukipenda labda hivi:
Utaifa - nationality
raia - citizen (lakini pamoja na maneno mengine pia "mtu wa kawaida", yaani "wakristo raia - mapadre" au "watu raia" - "wanajeshi")
wakazi - inhabitants
wananchi - people of an area

Kama ni maneno yasiyotumiwa kisheria mara nyingi maana zinaingiliana.
 
Raia: mtu anaetambulika kisheria kuwa ni wa nchi fulani hata kama hakai katika nchi hiyo kwa wakati huo. Kwa mfano Mwandendeule ni Mtanzania anaeishi Norway.
Uraiani: Makazi ni ya watu wasio na kazi maalum kisheria yenye kuwatambulisha. Ni popote pale wanapokaa watu wasio katika vikosi vya ulinzi na usalama.
Mwananchi: mzawa au mhamiaji anayeishi "uraiani".
Wananchi wenye hasira kali inatoka hapo juu kwenye neno "mwananchi"
 
Hapana kwa sababu si lazima kila raia kujipatia pasipoti. Raia wengi hawana pasi kwa sababu hawakuhitaji wala kuomba bado. Lakini kila raia anaweza kuchuka pasipoti.
Ulazima hauna hiyari,tambua hilo
 
Back
Top Bottom