Mwenye ubavu anishtaki! - Yona

Waheshimiwa Wajumbe!
Nimekaa kimya weee lakini mwishowe naona bora nami nijumuike ilikuongezea nguvu mapambano zidi ya mafisadi viburi!

Kuna baadhi ya Waheshimiwa waliotangulia wanadai hawa mafisadi hawajui kusoma alama za nyakati..lakini mimi kwa mtizamo wangu, nafikiri ni watu waliosoma alama za nyakati, huenda tukizubaa tu! wanachomoa mashambulizi yetu yote.

Maana walishajua haya yatatokea kwa siku zijazo nao wakaanza kujipanga mapema; Kwa mujibu wa Mh.Nyama Hatari; Nicholas Mkapa ni DPP..je anaweza akamfungulia Kesi Mkapa?

...Itakuwa ni naive and stupid kusubiri DPP (Director of Public Prosecutions) wawachunguze achilia mbali kuwafungulia mashitaka kwa vile Nicholas Mkapa hivi tayari sasa ni afisa wa DPP.

Nyingine ni hii: Nimaruku kutangaza mali za Viongozi..iliandaliwa na Fisadi Chenge kwa kusoma alama za nyakati.

"Kwa mujibu wa Ofisa Habari Mkuu wa sekretariati, Bw. Augustus Kariya, sheria ya maadili ya viongozi inaruhusu kuperuzi majalada ya mali zao lakini inakataza kutangaza kwa namna yoyote taarifa za `utajiri` au`umaskini` wao.

``Mtu atatutumia vibaya taarifa alizozipata kwenye daftari endapo atatumia sehemu tu kutangaza kwenye vyombo vya habari au kuzitoa bayana kwa umma.``

Akinukuu kanuni ya saba kifungu cha 2(b) Bw. Kariya alisema na kuwataka waandishi kusoma masharti ya sheria ya sekretariati hiyo ili waone jinsi ambavyo kanuni na taratibu zisivyoruhusu utoaji wa taarifa.

Ofisa huyo aliambatanisha nakala ya kanuni hizo akieleza kuwa adhabu kwa atakayekiuka sheria inapatikana katika kipengele namba tatu kinachoeleza:

``Yeyote atakayetangaza mali za viongozi anapatikana na hatia na adhabu yake ni faini Sh. 10,000 au kifungo cha miaka miwili au vyote kwa pamoja.``

Source: Mh. kitia wa JF

Sheria hiyo ilipitishwa wakati Fisadi Chenge akiwa Wiziri huko Sheriani. Je hapo tutasema walikuwa hawajasoma alama za nyakati?

Kitu ambacho pia kwa mtizamo wangu, nahisi hawa washirika wa BWM waliambizana kwamba huko tuendako mambo yanaweza kuwa moto hivyo... ukishutumiwa wewe nyamaza kimya wala usijibu mapigo kwani ukiwajibu utawasha moto..ndiyo maana unaona Sumaye kimya!!! Mkapa kimya!!! Hapa ninauhakika waliambizana..ndiyo maana akishajiuzuru tu ananyamaza kimyaa!!! wameshagundua kuwa kelele zetu huwa ni moto wa kifuu...kisha tunazimika na kuwaacha wakiendelea kuvinjali na "vijisenti" walivyo tunyonya.

Kwani kwa Balali kinaendelea nini waheshimiwa?..labda mimi niko nyuma ya mstari! Hivi hatua za awali zilishaanza kuchukuliwa dhidi yake?

Kwa wale wanavijiji wenzangu tunaoishi kwenye mabonde yanalimwayo mpunga' kuna kile kipindi cha kuwania ndege..kama ndicho kiswahili chake ama la! naomba BAKITA watanisaidia hapo. Mkulima huweka vijisanamu kama watu ilikuwatisha wale ndege wasije shambulia mpunga wake, mwanzoni ndege wanaogopa kweli hawatui shambani wakiamini hivyo vijisanamu ni watu, lakini kila siku wanapita pale shambani wanaona kile kijisanamu hakitikisiki wala hakibadili nguo, hivyo wanakizoea wanaanza kutua na kuendelea kushambuli mpunga.

Baadae mkulima huamua kwenda kushinda shambani mwenyewe akikabiliana nao kila wakitaka kutua anawapigia kelele, wanapitiliza hawatui pale. Hapo ndipo ugumu wa kilimo cha mpunga ulipo.

Je, sisi tunawapigia kelele tu hawa mafisadi kisha wakishajiuzuru tunawaacha waendelee kufaudu walivyotuibia! ama sisi wananchi na wabunge tunaopiga kelele ni kama vile vijisanamu vya shambani kwa hiyo walishatuzoea, wanaendelea kutushambulia tu pamoja na kelele zetu!

Kazi kwetu sote ipo, tupeane mbinu za kuwashambulia na wala siyo kuwawekea vijisanamu...Asanteni Waheshimwa Wajumbe..nisamehewe pale nilipotumia lugha isitokuwa ya kiungwana!
 
hapa ndio hua namuona Sheikh Yahaya tapeli maana haya yote alishindwa kuyatabiri....""Mwaka wa kuchukua vyetu kwa wezi"" Mkapa hata iweje lazima uonje utam wa sheria
 
Back
Top Bottom