Time will tell hawa jamaaa wamenunua mgodi kwa bei chee tena wanalipwa capacity charge wanatakiwa wanyang'anywe mali ya watanzania halafu waende jela
Habari zinazoingia mida hii zinasema kuwa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini na mbia mkubwa wa Mgodi wa Kiwira Bw. Daniel Yona amejitokeza na hatimaye kuzungumzia madai kuwa yeye pamoja na Rais wake walijigawia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira kwa njia za kinyemela.
Imeripotiwa katika mojawapo ya magazeti kuwa Bw. Yona anadai kuwa haki iko upande wake na hajatisikika.
Bw. Yona anasema kuwa aliposikia kuwa kuna mbunge toka Kilimanjaro ameleta hoja ya Kiwira alidhania ni Bw. Ndesamburo wa Chadema. Lakini alipogundua kuwa ni Kimaro wa Vunjo (CCM) Bw. Yona alibakia kusema "Haya bwana".
hivi sheria za nchi zinaruhusu bunge kufungua mashtaka?
Yona pole sana kakyangu,ila ujue umefuta historia njema ya wanao, siku zote kizazi chako kitadharaulika na hata kutengwa, fanya maarifa uturudishie hayo mapesa yetu, siku zote watanzania ni wapole ila siku wakicharuka, sijui itakuaje.
.........Bandugu,
hii kitu CAPACITY CHARGE!!!..........ina maana gani hasa na ni ya nini
Capacity charge -- An element in a two-part pricing method used in capacity transactions (energy charge is the other element). The capacity charge, sometimes called Demand Charge, is assessed on the amount of capacity being purchased.
Kwa ninavyoelewa ni kama vile service fee. Kwa hiyo kama unanunua umeme, pia unalipa gharama ya kukuuzia huo umeme. Mwenye kujua zaidi anaweza iweka sawa.
Kwa ninavyoelewa ni kama vile service fee. Kwa hiyo kama unanunua umeme, pia unalipa gharama ya kukuuzia huo umeme. Mwenye kujua zaidi anaweza iweka sawa.
Mzuzu,
..... angalia quatation hii:
``Kama yupo mwenye ubavu na nia ya kwenda mahakamani sawa ni haki yake, sitishiki kwa vile pia nina haki zangu. Tutakutana huko,`` alisema.
HIKI NI KIBURI CHA KUTISHA
Jamani mbona MKAPA haongei kitu??? waandishi wa habari mnamsuburi huyu jamaa mpaka awaite???? nendeni wenywe mkamuombe mahojiano nae, msumbueni mpaka atamke neno jama, na naahidi siku atakayo fungua mdomo ataongea madudu kama haya "ooo ni magazeti ya udaku tuu, am going to grant their wish am resigning".... "ni vijisenti tu na sitajiuzulu"