Mwenye taarifa yoyote ya ajali ya gari maeneo ya Iringa, awasilishe

Sijui hata nisemeje, nikitoka mm anafata yeye, yeye ndio was mwisho, bado mdogo, dah inaniuma sana, maisha haya
"Kila nafsi itaonja mauti, na hakika mambo yalivyo mtapewa ujira wenu kamili siku ya kiama, na yeyote atakaye epushwa na moto na akaingizwa peponi basi huyo amefaulu, na hayakuwa maisha ya dunia isipokuwa ni starehe ya udanganyifu."

Qur'an 3:185

Mkuu BrownRange maneno yangu machache sana katika wakati huu mgumu kwako ni haya:

Siku ya mdogo wako ilikuwa imefika na hakuna tena budget ya rizki yake hapa duniani, hakuna tena maji, chakula, pumzi wala makazi ya kumfanya aendelee kuwa hai, hivyo shukuru kwa hilo na sisi tuliobakia tuendelee na maandalizi kusubiri wakati wetu.

Jikaze kama mwanaume na umfanyie ndugu yako yale anayopaswa kufanyiwa maiti, na uliharakishe hilo kwani kukaa hapa duniani akiwa na hali hiyo ni udhalili kwake, na ujitahidi uwe na subra na ujasiri.

Kama ambavyo hakuwepo kabla basi aliyemleta kwenu akamfanya sehemu ya familia yenu, ndiye huyohuyo alieamua aondoke leo na awaache peke yenu, ridhikeni na hilo na mshukuru kwa maisha yake ijapokuwa ni muda mfupi, na hayakuwa maisha yetu haya ya dunia isipokuwa ni starehe tu yenye kudanganya.

.إنّا لله و إنّا إليه راجعون
 
Mkuu pole sana kwa msiba ulioupata.
Mungu akupe wewe na wafiwa wote roho ya ustahmilivu katika kipindi hichi kigumu.

Japo taarifa rasmi ya ajali haijatoka mpaka sasa ila itakapotoka tutajua mbivu na mbichi
 
Mkuu pole sana kwa msiba ulioupata.
Mungu akupe wewe na wafiwa wote roho ya ustahmilivu katika kipindi hichi kigumu.

Japo taarifa rasmi ya ajali haijatoka mpaka sasa ila itakapotoka tutajua mbivu na mbichi
Mimi nasoma tu ila comment yako nimeisoma kiundani.
 
Back
Top Bottom