Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,105
Mdau wa Dar amekuja DM akieleza malalamiko yako na masikitiko makubwa yanayofanya na matajiri wachache wanapotaka kufilisi mali za umma.
Mdau anasema Mradi wa mwendo kazi unaosimamiwa na watanzania umepeleka dharau na fedhea kwa mamlaka zifuatazo
1. Wamedharau kwa kiwango cha juu maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.
2. Akaenda Waziri mwenye dhamana akatoa maelekezo lakini hakuna utekelezaji
3. Awali alikwenda Waziri Mkuu naye akaongea mabadiliko yakafanyika kwa muda then kimya.
Pamoja na kukiukwa kwa maelekezo wafanyakazi wamebadili mfumo wa maisha na sasa wanajipatia kipato kwa kutotoa chenji. Asubuhi na jioni hakuna chenchi za wateja, kumbuka muda watu wanaotumia kupanga foleni.
Lakini ukifanya uchambuzi mdogo Mradi huu unaonekana una rasilimali kubwa ya watu wasiofanya kazi. Wanaripoti kazini asubuhi hadi jioni bila kazi yoyote. Mchanganuo wa wafanyakazi kwa kituo cha gerezani
1. Kuna askari kumi na mbili kwa shifti
2. Wakata tiketi 4 per shift
3. Wachanja tiketi 7 per shift
4. Wanaoratibu kupanda magari wapo 8
5. Wanaosimamia matangazo wapo 5
Kwa muktadha huu kuna zaidi ya watu 32 wanaotamatisha huduma ya mteja kupanda gari kwenye kituo kimoja.
Swali
1. Askari 12 wanafanya kazi gani vituoni endapo huduma imeboreshwa? Mbona vituo vya daladala hakuna kampuni za ulinzi? Tunadhani mwenye kampuni ya ulinzi ataruhusu huduma za kielektroniki katika mazingira haya? Akiruhusu waajiriwa wake watapata wapi pakujustfy mikataba?
2. Kituo cha gerezani kina abiria wengi kwanini madirisha ya huduma yawe manne tu?
3. Wanaoajiriwa kukata tiketi walikuwa na ulazima wakuwepo kwenye vituo?
4. Waajiriwa wengi kwenye huu Mradi ni watoto wa vigogo na ndugu zao. Akili zao zinaweza kufanya mabadiliko?
Tukumbuke Hiki ni kituo kimoja, sijachambua madereva wanaolipwa mshahara bila kufanya kazi, mameneja na viongozi waliokaa ofisini, wapo watu wameajiriwa kutafuta chenchi nk...
Kufeli huku na kiburi hiki nani yupo nyuma yake? Magu alitumbua wala deal wa mwanzo, je waliokabidhiwa lini watajifunza kwamba utawala ukibadilika watajikuta jela?