Mwembe Yanga is dead!!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
View attachment 59865Kwa wale wenzangu, waswahili wa Temeke/Tandika mtaukumbuka sana mwembe huu.
Umekuwapo hata kabla ya uhuru, na mikutano mingi tu ya kisiasa imefanyika katika uwanja karibu na hapo, including ule wa Dr Slaa wa "List of Shame".
Mtakumbuka vile vile katika mwembe huu bendera ya Yanga ilikuwa ikitawala kwa miaka mingi sana , karibu miongo mitatu au minne iliyopita.
RIP Mwembe Yanga
 
Nasikia Dar kuna eneo linaitwa chai juu ya mwembe liko karibu na barabara ya morogoro, huwa najiuliza ni nani hasa mpishi wa hiyo chai.
 
Nasikia Dar kuna eneo linaitwa chai juu ya mwembe liko karibu na barabara ya morogoro, huwa najiuliza ni nani hasa mpishi wa hiyo chai.
Mbona unaharibu jina la maeneo yangu? unaitwa Muembe chai karibu na nyumbani kwa Marehemu RIP. Sheikh Yahaya Husein. Na Kuna Msikiti mkubwa unaitwa Msikiti wa Muembe Chai Mwaka 2003 Polisi waliwapiga Waislam wa huo Msikiti wa muembe chai kulikuwa na vita kati ya Waislam wa huo msikiti na Serikali unakumbuka mkuu Asante?
 
Last edited by a moderator:
Ili kuendeleza Historia ya mwembe Yanga, ni vizuri WanaYanga tupande mwembe mwingine, tuutunze ili uchukue nafasi ya huu unaokauka. Kwa kufanya hivyo Historia ya mwembe huo maarufu na alama muhimu hapa Dar haitopotea
 
Kwa kweli huu mwembe umezeeka mno! Ila kwa kuuenzi naungana na kimondo upandwe mwembe mwingine na usiwe hii miembe ya kisasa!
 
Ili kuendeleza Historia ya mwembe Yanga, ni vizuri WanaYanga tupande mwembe mwingine, tuutunze ili uchukue nafasi ya huu unaokauka. Kwa kufanya hivyo Historia ya mwembe huo maarufu na alama muhimu hapa Dar haitopotea

Kwa wanaoujua Mwembe Yanga watatofautiana sana na huyu mleta mada maana picha aliyoitoa si wenyewe. Wenyewe upo karibu na kanisa na si kwenye kona kama unavyoonekana huu kwenye picha
 
Back
Top Bottom