Mwapachu waambie barrick walipe kodi

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,855
8,253
Tulisoma hivi majuzi kuwa makampuni ya migodi na simu hailipi kodi inayostahili kutokana na mapato wanayoyapata,kwa lugha nyepesi ni kuwa wanakwepa kulipa kodi,na sheria zetu ziko wazi kuhusu wakwepaji kodi.Pia nilimsikia Mwenyekiti wa Barrick Mheshimiwa sana Juma Mwapachu akisema kampuni yake imetenga mamilioni ya fedha kwa ajili ya mfuko wa jamii zinazozunguka hiyo migodi,mimi naona kwanza angejikemea mwenyewe na watendaji wake kwa kukwepa kulipa kodi kwa kampuni iliyo chini yake na inamharibia taswira yake kama kiongozi makini.Pia nashangaa TRA wameufyata angekuwa muhindi wa pale kariakoo au mimi mlalahoi siku nyingi ningeshafilisiwa,
Angalizo TRA wasiwe wanaangalia tu vidagaa kwenye ulipaji kodi bali hata mapapa au nyangumi nao washughulikiwe kwa usawa,inashangaza kwa TRA walivyoshupalia pale Break Point kuhusu mashine za malipo hadi mkurugenzi akatoa ufafanuzi lakini kwa mapapa kama makampuni ya simu na migodi hatujasikia tamko lolote.
Ingekuwa nchi za wenzetu huko majuu haya makampuni yangekuwa historia,kazi kwako Kitilya na aibu kwa TRA
 
Back
Top Bottom