Kwa kuwa umejitahidi kuthubutu, nakupa maswali machache uyajibu. Majibu yake yanaweza kusaidia kupata wajasiliamali wengine kama wewe kwenye forum. Na hapo utaweza kuonekanan umefaulu zaidi.
1. Gharama ya green houce moja ni kiasi gani, na kwa uzoefu wako msimu mmoja unachukua siku ngapi? Mavuna unapata kiasi gani kwa green house.
2. Unaonekana kyumia drip irrigation. Gharama za kuingiza drip irrigation in kiasi gani?
3. Tafadhalii baada ya hapo piga gharama za uzalishaji ili uone profit, return on capital kama vipo poa
Miaka mitatu ilopita nilinunua nusu eka pale mlandizi,nikaweka pilipili kali na kuhakikisha hazitegemei mvua, mwaka uliofuatia nikaweza kununua eka nne hukohuko mlandizi, nililima nyanya nusu ya eneo na lililobaki nikaendelea na pilipili, nyanya zinahitaji maji mengi sana kwa hiyo niliziacha zitegemee mvua, pilipili maji lita kwa wiki yanatosha, Mungu kasaidia mwaka huu nimefanikiwa kujenga greenhouse, nashukuru Mungu malengo yangu yameanza kutimia. Starehe napenda lkn nilijitahidi kuzizuia zisiingilie mipango yangu
attachment ni mfano wa vitu vyenyewe
Hizo picha zina tarehe 8/2/2011.Mungu kasaidia mwaka huu nimefanikiwa kujenga greenhouse, nashukuru Mungu malengo yangu yameanza kutimia.
Mkuu ngosha naomba tuwasiliane walau nije kutembelea shamba lako nijifunze kwa utekelezaji zaidi. Please if you can PM me your contacts I would be appreciative
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
hiyo green house mbona ni kama niliwahi kuitembelea.. huo mradi unafadhiliwa na serikali ya japan.. na mbele ya hiyo house naona pia bendera ya marekani.. ujawaibia vijana
Ngoshas kama ni kweli nakupa big up sana. Ni wachache wenye uthubutu kama wako. Ila kwenye hiyo green house pamoja na maeneo yanayoizunguka inaonekana kama kwenye maonyesho fulani hivi!! Naona vibao vinavyoonyesha aina ya mimea iliyooteshwa pamoja na bango kwenye hiyo GH, au ulikuwa na ugeni?? Nikupe hongera, ila usisahau kujibu maswali ya wadau kwa faida ya wengi, mimi mmojawapo.
Hongera sana !