Mwanza walia na mgao wa umeme. Dodoma, Kagera wachekelea!!!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Mkoa wa mwanza umekumbwa na adha kubwa ya mgao wa umeme hali ambayo imepelekea mbunge wa nyamagana kuliomba bunge liahirishe mjadala wa bajeti ya wizara ya maliasili na utalii ili kujadili hoja ya dharura ya mgao uliokithiri wa umeme ulioukumba mkoa wa mwanza pamoja na maeneo ya Arusha, Mbeya, Kigoma na Dar es Salaam.

Nimeongea na mdau mmoja kutoka mwanza anasema tangu jumapili hawajaona mwanga wa umeme si mchana wala usiku. Watu wenye majenereta wamegeuza adha hiyo kuwa mtaji na baadhi yao hasa kwenye vibanda vya biashara wanachajisha simu kwa shilingi elfu moja (1000).

Wakati watu wa mwanza wakisota gizani hali ni tofauti katika mkoa wa dodoma ambako hakuna hata chembe ya mgao wa umeme licha ya mkoa huo kutumia umeme wa gridi ya taifa. Hali kama hiyo imeripotiwa pia katika mkoa wa Kagera.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom