KONK MASTER
JF-Expert Member
- Jan 31, 2023
- 1,225
- 511
Ninamasikitiko sana ingawa Mwanza ni Jiji la pili baada ya Dar lakini barabara ya Kenyata ni mbovu sana kuliko barabara zote kuu za Tanzania.
Serikali inatakiwa iiangalie hii barabara kwa jicho la kipekee, barabara inatakiwa ifumuliwe yote kuanzia Mwanza mjini hadi Shinyanga boarder km 104 na iijenge upya kabisa kwa viwango vikubwa.
Inatakiwa ijengwe njia sita kutoka mjini hadi Usagara, njia nne Usagara had Mwanangwa - Misungwi kupunguza foleni kubwa iliyopo na ambayo itakuja baada ya kukamilika kwa daraja la JPM.
Pia barabara za mitaa Nyegezi ni mbovu kweli hata gari kuendesha unapata shida kwani ni kweli viongozi hamlioni hili?
Barabara iendayo machinjioni ni huzuni sana na inamfikirisha kwa kuona barabara inayoelekea machinjio ya Jiji lakini imejaa makorongo na viongozi wanapita tu wala hawajali kabisa, miaka kadhaa haijengwi kwa lami wakati ni fupi kama mita 400.
Barabara ya Kishiri ni mbovu mno, sometime mvua zikizidi hatupati huduma ya magari maana barabara haipitiki na viongozi mpo tu.
Naomba viongozi mtekeleze hili maana najua mnajua sana na mnatupuuza kama vile hatulipi Kodi. 🧐