Mwanza: Mtoto ateketea kwa moto wakati wa operesheni ya Kiserikali

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,889
35,901
Habari hii ni kutoka Kaliua, Tabora ambako wale jamaa wasiokuwa na chembe ya utu walikuwa wametia timu kwenda kufanya yao.

Unachoma vipi nyumba ambayo wanaweza kuwemo ndani watoto wadogo, wazee au wasiojiweza?

Piga picha kumwona mtoto wa miaka 4 yuko je.

Eeh mola wetu umrehemu malaika wako huyu aliyetangulizwa kifedhuli kwako. Ukawakirimu majahili hawa ujira sawa sawa na matendo yao:

(Picha za tukio hili haziwekeki hapa katika hali yoyote).

=====

Mwanza. Mtoto Nyanzore Ng'wandu (4) amefariki dunia kwa kuteketea kwa moto wakati wa operesheni ya kuwaondoa wananchi waliovamia eneo tengefu ndani ya Hifadhi ya jamii Isawimo inayoundwa na vijiji 11 vya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana Ijumaa Juni 18, 2021 mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Abel Busalama amethibitisha kifo cha mtoto huyo kilichotokea wakati wa operesheni iliyofanyika Juni 16, 2021.

Mtoto aliyetekea kwa moto ni mjukuu wa mzee Ng'ombeikungire Ng'wandu, mkazi wa kijiji cha Kombe wilayani Kaliua.

"Serikali imesikitishwa na kifo cha mtoto huyo na vyombo vya dola vimeanza uchunguzi wa kuhusu tukio hilo. Mimi binafsi nimefika eneo hilo nikiongozana na kamati ya usalama ya wilaya."

"Kuna maswali na hoja nyingi kuhusu kifo cha mtoto yule, kwanza wana familia wanasema aliteketea baada ya kuanguka mlangoni katika jitihada za kujiokoa. Lakini eneo mwili upokutwa ni karibia hatua mbili kutoka mlangoni," amesema.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, kuna hisia kuwa kifo cha mtoto huyo ni tukio la kutengenezwa kwa nia ya kukwamisha operesheni ya kuwaondoa waliovamia eneo la hifadhi na kuendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo makazi, kilimo, uvuvi na ufugaji.

"Siwezi kusema kwa uhakika ni nani ametengeneza tukio hilo lakini mazingira yanatia shaka na ndio maana vyombo vinafanya uchunguzi wa kina," amesema mkuu huyo wa wilaya

Akizungumzia tukio hilo, diwani wa Usinge, Titus Kavura amelaani kitendo cha askari Mamlaka ya Wanyamapori na Jeshi la Polisi walioshiriki operesheni hiyo kutumia nguvu na mabavu badala ya busara kiasi cha kuteketeza nyumba bila kutoa fursa kwa wananchi kujiokoa na kuokoa mali.

"Walichokuwa wanafanya askari wale ni kufika na kutia moto nyumba bila kujali ndani kuna watu wala mgonjwa, hii ndio maana wazazi walitimua mbio kujiokoa na kumsahau mtoto aliyekuwa amelala ndani," amesema diwani Kavura.

Mwanachi
 
mkuu wa wilaya anasema anahisi ni tukio la kutengeneza?! hivi ana akili kweli watu wamchome mtoto Moto ili kikwamisha operation? huyu kiongozi hayuko sawa asimamishwe kazi inaonekana yeye ndiye aliyetoa order ya Kuchoma Moto nyumba.
 
Ninasapoti hoja yako mkuu.

Operesheni ya kuondoa 'wavamizi' huwa haifanyiki bila usimamizi ama baraka za mkuu wa wilaya ama mkoa husika.

Hawezi akaanzisha sakata halafu arudi kujichunguza mwenyewe na kutoa maoni, kimsingi huyo ni mtuhumiwa na anataka kupotosha ukweli kwa ajili ya kulinda kitumbua chake.

Anajua fika ni hatua gani za kisheria zinazoanza kumnyemelea.

Anyamaze na aache achunguzwe kama wanavyochunguzwa watuhumiwa wengine na sheria ifuate mkondo.

Mara zote viongozi katili hutenda mabaya huku wakitabasamu kuonesha kama ni waungwana na wazalendo safi.

Serikali iwajibike na kubeba lawama zote kwenye kadhia hii.
 
Hawa watu haijulikani wanatuona je.
 
DC amefeli sana hapo mtu anateketezaje mtoto ili kukwamisha operation? Tena anayasema hayo mbele ya Camera??? Yeye anatoa wapi guts za kusema tukio limetengenezwa ili hali hata uchunguzi rasmi haujaanza?
 
mkuu wa wilaya anasema anahisi ni tukio la kutengeneza?! hivi ana akili kweli watu wamchome mtoto Moto ili kikwamisha operation? huyu kiongozi hayuko sawa asimamishwe kazi inaonekana yeye ndiye aliyetoa order ya Kuchoma Moto nyumba.
Kingine moto ni lazima?Maana ni kama anautetea....kwamba mtoto angefia mlangoni,hapo ni Sawa!!
 
DC amefeli sana hapo mtu anateketezaje mtoto ili kukwamisha operation? Tena anayasema hayo mbele ya Camera??? Yeye anatoa wapi guts za kusema tukio limetengenezwa ili hali hata uchunguzi rasmi haujaanza?
Halafu mtoto hajafia mlangoni...kafia mitaa kadhaa...kumbe kutumia moto kwenye zoezi hilo ni Sheria ya Nchi/Wilaya?!!!She.....z _-Ake huyo DC
 
Kwanini nyumba zichomwe? Hakuna hekima wala busara katika kuhamisha raia? Tuna safari ndefu sana....
Wakitumbuliwa, wanalalamika...Mama anasema kila Leo njia zipo nyingi tu,kwanini tujifiche kwenye Mabavu?REJEA tena ..Machinga kule Morogoro
 
Back
Top Bottom