Mwandishi Munga Tehenan: YUPO WAPI?

Nami nilikuwa mpenzi mkubwa wa gazeti la JITAMBUE,nilijifunza mengi sana jinsi ya kuishi na watu,na hasa kuwasaidia usiowajua,kupitia kwake nilijifunza kuwa wema unalipa,wema ni akiba.niliumizwa sana na kifo chake,kama sikosei JITAMBUE lilikuwa linatoka siku ya alhamis,nilikuwa naweka order kabisa,nakumbuka siku naenda kuchukua gazeti,nikaambiwa mtunzi amefariki,nafsi yangu iliugua sana.hata hivyo ameniachia hazina kubwa ya mafundisho yake.RIP MUNGA TEHENAN.
 
Wadau naomba kujuwa alipo mwandishi maarufu wa makala, na one time mhariri na mmiliki wa gazeti la JITAMBUE.

Ameandika vitabu vingi vya lugha na hadithi, na kuna wakati alikuwa na TALK SHOW pale TBC1 Wakati ikiwa TVT. Pia amewahi kuwa Majira Publishers, nadhani mhariri wa vitabu among other things...

MHARIRI, MUNGA TEHENAN!
Namkumbuka sana kwa gazeti lake la jitambue
 
Mungu aliaga dunia kitambo,kitu kama 2007 hivi na aliswaliwa pale msikiti wa kibo.Alipokufa na shughuli zake zote ziliishia hapo.Kuna umuhimu wa kujenga mfumo wa kitaasisi kuliko kusimama mtu kama mtu.
Mkuu, ulichoongea ni ugonjwa mkubwa sana kwenye familia nyingi sana...
Either wenye shughuri hawataki kushirikisha wengine AU wanaotakiwa kushirikishwa hawajuonyeshi kutaka kushiriki
 
Mi nilikuwa nafatilia makala zake kwenye magazeti ya Jitambue tu. Tena kipindi hicho nilikuwa bado mdogo sana kiasi kwamba binafsi sikuwa na hela hata ya kununua gazeti hivyo kama baba hakuleta hilo gazeti basi siku hiyo nilikuwa nakosa raha.
Pia nimekuja kupata video zake mwaka huu huu ila kumbe tayari ameshaucha mwili
Nahitaji kupata hizi video, unanisaidiaje ndugu?
Ni kweli alitutoka kimwili kama mwenyewe alivyopendelea kusema.

Mojawapo ya makala zake ambayo ilichukuliwa kama ilikuwa ikitabiri kifo chake ni hii ambayo nitaiweka hapa chini.

Na ni kweli hayao yote aliyo yaandika yalitokea kwenye msiba wake, nadhani waliohudhuria watakumbuka zaidi.
 
Kwa Comments Hizi inaonekana Munga Tehenan alikuwa na Cha Ziada... Aliitendea vema Dunia alimokuwa..
Remember ...."Who Will Cry When You Die???"
 
Back
Top Bottom