Mwanaume usijichukulie poa

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,962
6,896
Habari zenu wakuu,

Neno "WAKUU" kwangu namaanisha hapa nimelenga wanaume so, popote ukiona uzi wangu umeanza na hiyo salamu basi kama wewe ni mwanaume hakikisha unaupitia maana huo uzi unaongeza nguvu za kiume.

Katika miaka yangu ishirini na kitu niliyonayo nashukuru Mungu kwa maarifa kiasi ya kuchanganua mambo ambayo ninayo, kwani nimekaa na wenzangu wengi wa rika langu ila kiufahamu kuhusu maisha kiujumla nakuwaga nyota wa mchezo.

Ipo hivi kuna ule usemi unasemaga "Nyuma ya mwanaume aliefanikiwa kuna mwanamke" na huu usemi umekuwa maarufu sana na wengi wetu tunauamini sana. Huo usemi umebeba maana kwamba eti ili mwanaume afanikiwe lazima mwanamke awepo nyuma kumsupport, Na ubaya wa huu usemi hawajauweka kuonesha ni kwa kiasi gani bali wameuweka in general kuonesha kwamba mwanaume hawezi kufanikiwa bila kuwa na mwanamke. Wote nadhani tunafahamu kwamba kufanikiwa ni maana kwamba ni kiuchumi.

Lakini sasa huo usemi wakuu hivi ninyi mkiutazama hamuoni kama una lengo fulani la kumfanya mwanaume akose kujiamini yeye mwenyewe? Yaani ni sawa na mtu akuambie kwamba wewe bila fulani hufanikiwi na ukitazama wote ni wanadamu, ndiyo kufanikiwa kwangu pengine napaswa kukutana na fulani ili nifanikiwe ila sio kweli kwamba kama sitokutana nae basi sitofanikiwa maana mafanikio ya mtu yanachangiwa na juhudi na bahati pia, Haya basi tuachane na hilo twende kwenye point sasa... Hivi tuongee ukweli ebu fikiria tu kwenye suala la kufanikiwa kimaisha kati ya mwanamke na mwanaume ni nani ambae anamuhitaji sana mwenzake?

Nimeishi mazingira tofautitofauti nimeona washkaji kibao wanaishi magheto hawajaoa na maisha yanasonga na wanamudu bills zao bila stress wala kisirani, Na pia nimeishi mazingira nikaona wanawake waliojaribu kuishi gheto na kujitegemea ila in deep nilipochunguza walikuwa na backup either za wazazi au mwanaume yeyote yule awe Baba,Kaka,Mjomba au Danga, Na ikiwa walikosa backup kabisa basi hawakukosa visirani, Ni mara chache niliona ambao walifanikiwa hilo ila bado walikuwa na hisani ya mwanaume fulani au wanaume.

Mwanaume hujenga nyumba yake akaimaliza hata shilingi isitoke kwa mwanamke ila amini usiamini Nyumba aliyojenga mwanamke Shahidi yake msingi, ni lazima tu kuna mwanaume amechangia kama sio Baba yake mzazi, Sio mtu alienae kwenye mahusiano, basi hata nafasi ya kazi anayofanya inayomlipa hela ya kutosha kujenga ilikuwa ni hisani ya mwanaume fulani.

Huo usemi wa nyuma ya mwanaume aliefanikiwa kuna mwanamke nyuma ni vice versa na najua tu aliegeuza alikuwa na lengo la kumfanya wanaume duniani kutokujiamini na akafanikiwa kwa asilimia kubwa maana hiyo slogan kwa wana waishi nayo kwwnye vichwa vyao jambo ambalo limewafanya kuwasujudia wanawake, Ila Mimi siku zote naamini kwamba Mwanaume anaweza kufanikiwa hata bila mwanamke, Ila mwanamke anahitaji zaidi hisani ya mwanaume ili yeye kufanikiwa.

Wakuu pambaneni na maisha kufanikiwa ni juhudi zako wewe mwenyewe na bahati yako ila asitokee mtu akakuambia bila mwanamke hufanikiwi, Wewe Mungu amekuumba ni mwanadamu na nusu... Wewe ndo Controler wa kila kitu, Wewe unaweza kuishi popote bila chochote na ukatoboa, Wewe hufai kujilinganisha na mwanamke hata kidogo.... Wewe kabla ya huyo mwanamke ulishaishi sana peke yako hapa duniani, Mungu aliona umekuwa tu mpweke akaona akuletee msaidizi ila upweke haukumaanisha kwamba ungeshindwa kuishi bila yeye.

Nakasirika sana nikiona mwanaume anaeteseka kwaajili ya mwanamke alafu mwanamke mwenyewe anamchukulia poa anamuona sio kitu oya asee ningekuwa na uwezo ninyi ambao mnafumaniwaga mnapigwa ningekuwa na kazi ya kuwaongezea.

Oya Malume usijichukulie poa malume.
 
Ipo hivi kuna ule usemi unasemaga "Nyuma ya mwanaume aliefanikiwa kuna mwanamke" na huu usemi umekuwa maarufu sana na wengi wetu tunauamini sana. Huo usemi umebeba maana kwamba eti ili mwanaume afanikiwe lazima mwanamke awepo nyuma kumsupport,
Hujamaliza sentensi mkuu

NYUMA YA MWANAUME ALIEHARIBIKIWA AU ASIEKUA NA MAFANIKIO KUNA WANAWAKE WENGI WALIOCHANGIA KUMFANYA AWE HIVYO

Ili mwanaume afanikiwe anahitaji mwanamke mmoja tu sio lundo la wanawake, hio ndio maana halisi ya huo msemo
 
ila ni uhakika mara 3 zaidi mtu akisema nyuma ya mafanikio ya mwanamke kuna mwanaume..
Ili mwanaume ufanikiwe unahitaji kitulizo kitulizo Cha Nafsi, usiwe kibolodinda tulia na mwanamke mmoja songa mbele hata km utakua na wa nje Ila mmoja mzingatie
 
Na ubaya wa huu usemi hawajauweka kuonesha ni kwa kiasi gani bali wameuweka in general kuonesha kwamba mwanaume hawezi kufanikiwa bila kuwa na mwanamke.
Hawakumaanisha hivyo maana yake ili ufanikiwe usiwe na lundo la wanawake kua na mwanamke mmoja tu anaekuzingatia na kukuonyesha njia ya kupita kuyafikia mafanikio,
 
Ipo hivi kuna ule usemi unasemaga "Nyuma ya mwanaume aliefanikiwa kuna mwanamke" na huu usemi umekuwa maarufu sana na wengi wetu tunauamini sana.
Labda iwe hivi. “Nyuma ya mwanaume alie fanikiwa kuna mwanamke mbinafsi”.
 
Ni kweli kabisa hii

Nyuma ya mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke, huu msemo umekaa kifeministi kuendana na ajenda za mambo ya wazungu... ila ni uhakika mara 3 zaidi mtu akisema nyuma ya mafanikio ya mwanamke kuna mwanaume..
🤝
 
Habari zenu wakuu,
Neno "WAKUU" kwangu namaanisha hapa nimelenga wanaume so, popote ukiona uzi wangu umeanza na hiyo salamu basi kama wewe ni mwanaume hakikisha unaupitia maana huo uzi unaongeza nguvu za kiume.

Katika miaka yangu ishirini na kitu niliyonayo nashukuru Mungu kwa maarifa kiasi ya kuchanganua mambo ambayo ninayo, kwani nimekaa na wenzangu wengi wa rika langu ila kiufahamu kuhusu maisha kiujumla nakuwaga nyota wa mchezo.

Ipo hivi kuna ule usemi unasemaga "Nyuma ya mwanaume aliefanikiwa kuna mwanamke" na huu usemi umekuwa maarufu sana na wengi wetu tunauamini sana. Huo usemi umebeba maana kwamba eti ili mwanaume afanikiwe lazima mwanamke awepo nyuma kumsupport, Na ubaya wa huu usemi hawajauweka kuonesha ni kwa kiasi gani bali wameuweka in general kuonesha kwamba mwanaume hawezi kufanikiwa bila kuwa na mwanamke. Wote nadhani tunafahamu kwamba kufanikiwa ni maana kwamba ni kiuchumi.

Lakini sasa huo usemi wakuu hivi ninyi mkiutazama hamuoni kama una lengo fulani la kumfanya mwanaume akose kujiamini yeye mwenyewe? Yaani ni sawa na mtu akuambie kwamba wewe bila fulani hufanikiwi na ukitazama wote ni wanadamu, ndiyo kufanikiwa kwangu pengine napaswa kukutana na fulani ili nifanikiwe ila sio kweli kwamba kama sitokutana nae basi sitofanikiwa maana mafanikio ya mtu yanachangiwa na juhudi na bahati pia, Haya basi tuachane na hilo twende kwenye point sasa... Hivi tuongee ukweli ebu fikiria tu kwenye suala la kufanikiwa kimaisha kati ya mwanamke na mwanaume ni nani ambae anamuhitaji sana mwenzake?

Nimeishi mazingira tofautitofauti nimeona washkaji kibao wanaishi magheto hawajaoa na maisha yanasonga na wanamudu bills zao bila stress wala kisirani, Na pia nimeishi mazingira nikaona wanawake waliojaribu kuishi gheto na kujitegemea ila in deep nilipochunguza walikuwa na backup either za wazazi au mwanaume yeyote yule awe Baba,Kaka,Mjomba au Danga, Na ikiwa walikosa backup kabisa basi hawakukosa visirani, Ni mara chache niliona ambao walifanikiwa hilo ila bado walikuwa na hisani ya mwanaume fulani au wanaume.

Mwanaume hujenga nyumba yake akaimaliza hata shilingi isitoke kwa mwanamke ila amini usiamini Nyumba aliyojenga mwanamke Shahidi yake msingi... ni lazima tu kuna mwanaume amechangia kama sio Baba yake mzazi, Sio mtu alienae kwenye mahusiano, basi hata nafasi ya kazi anayofanya inayomlipa hela ya kutosha kujenga ilikuwa ni hisani ya mwanaume fulani.

Huo usemi wa nyuma ya mwanaume aliefanikiwa kuna mwanamke nyuma ni vice versa na najua tu aliegeuza alikuwa na lengo la kumfanya wanaume duniani kutokujiamini na akafanikiwa kwa asilimia kubwa maana hiyo slogan kwa wana waishi nayo kwwnye vichwa vyao jambo ambalo limewafanya kuwasujudia wanawake, Ila Mimi siku zote naamini kwamba Mwanaume anaweza kufanikiwa hata bila mwanamke, Ila mwanamke anahitaji zaidi hisani ya mwanaume ili yeye kufanikiwa.

Wakuu pambaneni na maisha kufanikiwa ni juhudi zako wewe mwenyewe na bahati yako ila asitokee mtu akakuambia bila mwanamke hufanikiwi, Wewe Mungu amekuumba ni mwanadamu na nusu... Wewe ndo Controler wa kila kitu, Wewe unaweza kuishi popote bila chochote na ukatoboa, Wewe hufai kujilinganisha na mwanamke hata kidogo.... Wewe kabla ya huyo mwanamke ulishaishi sana peke yako hapa duniani, Mungu aliona umekuwa tu mpweke akaona akuletee msaidizi ila upweke haukumaanisha kwamba ungeshindwa kuishi bila yeye.

Nakasirika sana nikiona mwanaume anaeteseka kwaajili ya mwanamke alafu mwanamke mwenyewe anamchukulia poa anamuona sio kitu oya asee ningekuwa na uwezo ninyi ambao mnafumaniwaga mnapigwa ningekuwa na kazi ya kuwaongezea.

Oya Malume usijichukulie poa malume.
Mafanikio yangu kwa asilimia 98.9% yanatokana na mke wangu na ninamuenzi kila sekunde. Sidhani kama ningekuwa na mwanamke mwingine zaidi ya huyu niliyenaye ningepata haya mafanikio niliyonayo. Mwanamke mnayeendana naye ni mali sana maishani. Tuwaheshimu wake zetu wanaume wenzangu.
 
Unamaanisha bila huyo mwanamke wewe sio kitu?
 
Wewe bado ni mdogo na bado una mengi unatakiwa ujifunze usijifanye unajua.

Ulitumia vigezo gani kujikuta nyota wa mchezo unapojilinganisha na vijana wenzako?

Yaani kulipa Kodi, na kununua sub woofer ghetto ndio unaona umefanikiwa?

Umuhimu wa mwanamke kwenye maisha ya mwanaume hauna mbadala ,shupaza shingo yako ivunjike.
 
Ni kweli kabisa hii

Nyuma ya mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke, huu msemo umekaa kifeministi kuendana na ajenda za mambo ya wazungu... ila ni uhakika mara 3 zaidi mtu akisema nyuma ya mafanikio ya mwanamke kuna mwanaume..
Haha 😂 huyo mwanamke ni Mama Yako (mzazi/mlezi) ndio maana yake, sio Hawa kausha damu Mpwa, akina Hadija ndala ndefu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom