MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,090
- 22,373
Mambo mengi sana yamezungumzwa kuhusu mapenzi na ndoa kwa ujumla. Hata hili ninaloandika ni kama kukazia tu. Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema ni kuwa mwanaume yeyote kama kichwa cha familia ndo huamua familia yake iweje. Mwanaume ndo kabeba taswira nzima ya familia yake. Mimi leo nakumbusha jambo muhimu sana. Ishu za imani.
Kabla hujaingia kwenye ndoa hakikisha unajua unasimamia wapi. Uwe mkristo, mwislamu au mwabudu mizimu hakikisha unasimama na hiyo imani na ili familia yako ifuate unachofanya. Sijamaanisha ndo uwe mfia dini... nimemaanisha uonyeshe mwelekeo kwa vitendo kwamba familia yako ni waamini wa imani hii na sio vinginevyo. Mke na watoto wajue kabisa HILO NI SUALA LISILOHOJIKA.
Hii nimesema kwasababu siku hizi hasa kwa sisi wakristo kumekuwa na udhaifu mkubwa katika hili hadi kupelekea ndoa nyingi kuvunjika. Kina mama wamebeba hili jukumu na kuishia kuleta mambo ya kiwaki mengi sana. Wanawake wengi wana hawa wanaoitwa mababa wa kiroho. Huwa wanasikilizwa kuliko waume zao. Mwanaume usiposimama imara katika hili utaivuruga familia.