Mwanasheria na Mbunge Wa Chadema Tundu Lissu Atuombe Radhi Taifa Amemdhalilisha Baba Wa Taifa!!

Pindi baba wa taifa anatafuta uhuru wa taifa hili tundu lissu alikua wapi! Pindi baba wa taifa anaacha kazi iliyokuwa inmpatia kipato kwa ajili ya watanzania, huyu tundu lissu Leo anaishi vizuri na kukesha bar kw sababu ya mwalimu
 
mbona mtikila alimwita mzoga na kesi akashinda? kwani alikuwa malaika? na sina hakika kama hayo maneno ya akina massawe na wenzake alitaja. ayo umeongeza wewe.
 
- ha! ha! ha! unaongelea Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais, kwanza tuambie baba yako alifikia cheo gani kwenye seirkali mkuu wangu hoja za baba hapa hazina mashiko u know!! ha! ha! ha!

Le Mutuz System

Pamoja na ustaafu huo wananchi wa Mtera walimkataa na kumpa nafasi kijana mdogo Livingstone Lusinde... Imebaki historia Tu. Mi nakwambia kila kiti, katika umri wako wa miaka 56 siasa za majitaka hazikufai, jitahidi kufanya kazi kwa bidii kufidia pale ulipopoteza muda wakati unazima Moto na kuendesha malori mamtoni, hata kama itatulazimu kukutuma kutundika mabango huku tunakutafunia Sinta wako.
 
- Yaaani unahoji katiba kwa kumtukana baba wa Taifa ambaye kila wakati Chadema mnaenda kwenye kaburi lake? Sasa huwa mnaenda kufanya nini kwenye lile kaburi halafu mnajifanya kumheshimu mke wake Mama Maria halafu mnaenda bungeni mkurushia matusi mazito mazito namna hii?

Le Mutuz System

halaf we malecela ni snitch,unaongea kiumbea umbea ili utusikie tutasema nini, ni bora ukae kimya mikono ya baba yako imejaa dhambi na ufisadi wa wizi wa mali za umma, we mwenyewe ulikua mlevi na fuska mkubwa huko marekani ulikua una wahonga makahaba wa kizungu fedha za wavuja jasho ambazo baba yako fisadi aliesilimu kimy AAA kimya huko arabuni ili awe rais alikua anakutumia, nyie ndio maadui wa nchi hii, wazalendo ndio kama akina lissu ambao hawaogopi kuongea ukweli wenye tija na ustawi wa jamii. pole sana tunakujua huwezi kutudanganya.
 
Kaka yangu pole.Kwa vijana wa mwaka 47 mmeona amemdhalilisha lakini kumbuka kizazi cha leo kina hoji na kinataka majibu yanayothibitika kisheria kama halali.Hajamtukana wala kumdhalilisha sababu ameongea kwa nafsi yake na hata Mwl.Nyerere kwenye moja ya hotuba zake amesema tuwasamehe kama viongozi kuna mengi waliyokosea na mazuri waliyofanya,na akaomba mazuri yaendelezwe mabaya yaachwe.

Lakini viongozi wetu wameacha MAZURI wanafanya MABAYA.Kama kweli mnataka kumuenzi baba wa TAIFA anzeni na kurudisha mali za TAIFA kwa waliojilimbikizia mali kwa wizi,rushwa kubwa na hata madawa ya kulevya,uuzaji wa madini na maliasili zetu na hata kuwanyang'anya wanyonge(Watanzania) ardhi zao kwa kisingizio cha uwekezaji.

Leo mnamuenzi kwa Muungano mengine je?Hakuna kiongozi ndani ya CCM mwenye uwezo wa kusema tunamuenzi Mwl.Nyerere ,hawa viongozi ndiyo wanamdhalilisha Mwalimu kwa tabia na maovu wanayoyafanya ndani ya TAIFA letu.Wizi,udanganyifu,Rushwa,Ufisadi,uuzazji wa wanyama wetu,tembo maliasili zetu na madini.

Kwa hiyo kaka si Lissu wenye makosa ni nyinyi wenyewe.Kwa nini msubiri mpaka watu wa hoji ndiyo mtoe hiyo hati?Msimsingizie Lissu,mnaogopa ukweli tu.

Siku atakapo kutukana wewe ndio utajuwa kuwa yupo sahii. Mwana -------- ni chukizo kwa mamaye
 
Nikweli kuwa baba wa Taifa amelifanyia Taifa hili mambo mengi sana ya maana, Binafsi namheshimu sana kwa umoja wetu na uwezo wake wa kuzuia rasilimali zetu kukwapuliwa kama ilivyo sasa! Namkubali zaidi kwa yeye kukiri kuwa kuna MAMBO YA KIPUMBAVU mengi aliyafanya katika utawala wake! JKN alikuwa na mapungufu mengi yeye kama yeye MFANO! Alihakikisha Uchagani watoto hawafaulu hata kama wanaakili kiasi gani! Shule zilizokuwa na Waalimu, mazingira mazuri watoto wenye akili walikuwa wanafelishwa kwa zaidi ya miaka 20 plus bila ya kufaulisha hata mwanafunzi mmoja! AJABU ya Musa watoto hao hao walikuwa wakienda kurudia kwenye shule za Dodoma, singida, shinyanga, mwanza, moro, pwani nk Walikuwa wanafaulu sana! Leo hii utakuta akina masanja wengi ambao ni wachagga! Technocrats wengi wa nchi hii ni wachagga !!! Itoshe kusema JKN alikuwa na mapungufu mengi ikiwemo kuwabania mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kwa saana

Kwa hiyo ndo maana mmemtuma huyo kichaa wenu amtukane ili kuonesha hasira zenu. Hakika mmeanza safari ya kuenjoy laana yake na mtakwisha tu.
 
malecela wengine tunaona hao ndo wakombozi wetu.....wengine si washiba na wanazidi kulimbikiza.....na ndo maana lissu anaonekana amefedhehesha mtu. alikuwa sahihi kwa wakati huo na muda huo.
 
- Yaaani unahoji katiba kwa kumtukana baba wa Taifa ambaye kila wakati Chadema mnaenda kwenye kaburi lake? Sasa huwa mnaenda kufanya nini kwenye lile kaburi halafu mnajifanya kumheshimu mke wake Mama Maria halafu mnaenda bungeni mkurushia matusi mazito mazito namna hii?

Le Mutuz System

Umekuwa mkali bila sababu,kama Ikulu ingetoa hiyo Document hoja hiyo isingekuwepo na hata kama ingekuwepo ingekuwa nyepesi hata kuijibu,leo wananchi wameanza kuhoji hata saini ya Mwalimu kama kweli ni yake au umegushiwa?

Hivi aliyemtusi Mwalimu ni Lissu kweli au CCM?Hebu jiangalieni maisha mnayoishi nyie mnaotoka au mlioko kwenye familia za viongozi,watoto wenu hawasomi shule zetu,hatibiwi hospitali zetu haishi mazingira yetu.Kuna mlala hoi na mlala hai,kwa hilo tu ni TUSI tosha kwa Mwalimu aliyewapenda watu wake!

Leo Mama Maria huyo huyo mnayemtumia kwenye suala la Maendeleo hamumpi heshima stahili.Je hakunyimwa Kitambulisho wakati wa uzinduzi wa Vitambulisho mpaka aende kupewa Zanzibar?Ndiyo heshima hiyo?Basi kum-recognise tu ilikuwa shida,lakini pale pakutafuta mtelezo haraka mmeenda kumtafuta.

Mkiacha unafiki,ulaji,uzembe,uonevu,rushwa,ufisadi,madawa ya kulevya,kuuza raslimali za nchi ndipo tutasema CCM na viongozi wake mnamuenzi Mwalimu,lakini kwa sasa mnamtusi sana tu,kwa tabia zenu za kujilimbikizia mali.

Kwa kukueleza tu kwa ufupi kuna watu au familia nyingi za watanzania zilizoathirika na uongozi wa Mwalimu lakini hatukumlaumu wala kumlaani kwani alidanganywa sana na Viongozi aliowaamini wanatekeleza filosofi yake,lakini kumbe walikuwa wauaji wakubwa wakuiba halafu kesi anapelekewa mtumishi mdogo,na tukianza kueleza yote siyo tu familia ya Mwalimu bali hata wale wanaomuenzi kwa falsafa yake wataumia na kujiuliza maswali kwa nini hakujua yote,lakini sababu alikuwa binadamu na ameomba asehewe yale yameachwa.

Kwa hiyo aliyosema Lissu yametokana na utafiti wake,tatizo inawezekana Lugha tu aliyotumia ilikuwa kali mno ambayo wengi wa vijana wa miaka 47 mmeshindwa kuipokea,lakini ni nafuu yeye amesema kinachomuuma kuliko nyie mnaowaumiza watanzania wake aliowapenda mpaka dakika ya mwisho,ndiyo mnaomtusi sana tu,ukizingatia ndiyo wale waliolelewa katika falsafa yake ndiyo wale wale viongozi hadi leo.Product ya mwalimu ndiyo wala rushwa,mafisadi,wauza nhci yetu wakubwa ,ndiyo hawa wanaomtukana Mwalimu matusi ya nguoni .
 
- Yaani mimi Celebrity kupiga picha na Macelebrity wengine unasema ni sawa na Tundu Lissu kusimama mbele ya bunge na kumtukana matusi ya nguoni baba wa Taifa? Are u serious au unatania?

Le Mutuz System

Tanzania hamna maceleb bali tunao maceleb wanna be. Disabuse your mind kaka.
 
- Yaaani unahoji katiba kwa kumtukana baba wa Taifa ambaye kila wakati Chadema mnaenda kwenye kaburi lake? Sasa huwa mnaenda kufanya nini kwenye lile kaburi halafu mnajifanya kumheshimu mke wake Mama Maria halafu mnaenda bungeni mkurushia matusi mazito mazito namna hii?

Le Mutuz System

Umenena vyema mkuu, tatizo la CDM hawapendi kukosolewa na hilo ndio linalowapeleka shimoni. Wanakubali kuwa Nyerere alikuwa na mapungufu lakini hawataki kukubali kuwa Lissu amekosea! Kwa wao Lissu ni malaika, hakosei. Nawashangaa wabunge wawili wa CDM ambao ni wa ukoo wa Nyerere akiwemo mtoto wa Nyerere kama na wao wameukubali upuuzi alioufanya Lissu.
 
Pindi baba wa taifa anatafuta uhuru wa taifa hili tundu lissu alikua wapi! Pindi baba wa taifa anaacha kazi iliyokuwa inmpatia kipato kwa ajili ya watanzania, huyu tundu lissu Leo anaishi vizuri na kukesha bar kw sababu ya mwalimu

Uhuru wa Tanganyika haukuletwa na mtu mmoja. Usitake kutuaminisha kuwa kama Mwl Nyerere asingezaliwa Leo hii wakoloni bado wangekuwepo na mtu ukitaka kuingia bar kupata Kinana ya baridi wakoloni wanakuzuia, hayo ni mawazo ya hovyo. Jifariji na mzee mwenzio Le Mutuz System
 
Kuna mashriti nane (8) chadema wamepewa ili waingie madarakani. Kwanza nitaanza mawili kadri muda unavyokwenda nitayataja yote!
Kikao kilochofanyika nchini wingereeza mwishoni mwa mwaka 2013 na wadhamin wa chadema mmoja anatoka ujerumani na mwingine Denmark (majina tunayaifadhi).ili waendeleh kupokea misaada kutoka kwao walipewa mashriti!
1. Kuakikisha nchi ya Tanzania inakosa amani muda wote kwa kutumia vijana ambao wengi hawana kazi yaan ajira.
2. Kwakujua kuwa umma wa watanzania wanaiamin serikali yao! Inabidi kuwe na propaganda nchi nzima itakayowabadilisha watanzania mtazamo wa kutokuihamin dola!

Hoja: ndugu zangu wanzania mimi shishangai hata kidogo kwa upotoshaji unaoendelea kwenye bunge la katiba na nje ya bunge hilo co icho ndicho kinachoifanya chadema ipate misaada toka kwa wafadhili wao. Tunachotakiwa kukijua sisi kama wananchi ni kuwa macho na uzandiki na ufirauni huu unaofanywa na chadema kwa ajir ya maslah tu,Taifa hili ni letu sote leo tukilihalibu tutakimbilia wapi? Chadema imewafanya wananchi wengi wa Tanzania vilema, wajane na wengine kupoteza maisha kwa maslah ya viongozi wachache! Chukua hatua kuanzia sasa upotoshaji huu ukome Tanzania
 
Tundu Lissu amewashika pabaya na bado! Safi sana.eti kamtukana mwalimu , ivi nyie nani kawaloga? Au pesa za ufisadi.tumewachoka tunataka serikali tatu
 
Hivi kwani hawezi kushtakiwa kwa uhaini? Bunge Maalum la Katiba halina kinga inayomiwezesha mjumbe wake asishtakiwe. Feleshi hulioni hilo.
 
Umenena vyema mkuu, tatizo la CDM hawapendi kukosolewa na hilo ndio linalowapeleka shimoni. Wanakubali kuwa Nyerere alikuwa na mapungufu lakini hawataki kukubali kuwa Lissu amekosea! Kwa wao Lissu ni malaika, hakosei. Nawashangaa wabunge wawili wa CDM ambao ni wa ukoo wa Nyerere akiwemo mtoto wa Nyerere kama na wao wameukubali upuuzi alioufanya Lissu.
Nyie maCCM mmewadhalilisha hawa kuwa sio ndugu za Nyerere, Leo mnakosa hoja mnaanza kuwakumbuka.

The more hii ishu inajadiliwa na ukweli kuwekwa wazi ndivyo madudu ya Nyerere yatazidi kujulikana, hilo haliepukiki. Lissu ni agent tu wa kuweka ukweli hadharani, kubalini kuwa muungano una makosa, ruhusuni mjadala wa uhuru wananchi wachague kama serikali 1,2,3 au hata nne sio kutafuta sympathy
 
Mwalimu Nyerere alifanya yake kwa Wakati ule, miaka ile na kwa rasilimali zilizokiwepo Wakati ule, alijitahidi kwa uwezo wake kutokana na Wakati huo kulingana na changamoto zilizokuwepo kipindi hicho. Sasa Leo tuko Wakati mwingine na mambo yalivyokuwa kipindi chake si sawa na sasa ila CCM inataka tuzidi baki Kwenye kipindi kile kile cha Wakati wa Mw Nyerere wakati kuna baadhi ya mambo wamefanya kinyume Cha aliyoleta Mw Nyerere wazi wazi ikiwa ubadhilifu wa Mali za Umma,Uongozi dhaifu,Rushwa,Uchu wa Madaraka,Mihadarati etc. Na sasa wanaficha kwa kuleta kisingizio cha kumwenzi Mw Nyerere kwa kuleta UHURU na kusahau mengine. Hawataki Kusibitisha udhaifu wao ila wanangangania zisivyofaa kwa Wakati huu. Na ndio maana unaona kila Wakati wakisisitiza kumwenzi Mwalimu Nyerere hata kwa visivyostahili. Huo ni utumwa wa fikra kichama. Kuna Mazuri alifanya tutayaendeleza Mabaya tutaweka pembeni hivyo ndio ilivyo Na ndio maana tumeona serekali 2 au muungano uliopo hazifai Na sababu tumeweka kungekuwa hakuna shida tusengekuwa na sababu, ukiona sababu Kwenye Jambo lolote basi jua kitu hicho kinamapungufu. So Mr Lissu kafanya yake kwa Wakati wake na ni Haki yake, katiba ni uti wa mgongo wa nchi tuache kuleta maneno ya kupotosha ili tuone kakosea.
 
I don't know Tanganyika, I have never seen Tanganyika, I don't want Tanganyika I am a Tanzanian.

I am a Tanzanian. Of blood cleaned by fresh waters of the lakes and the rivers and the streams of my great nation. A vision from the top of mount Kilimanjaro and honesty as clear as The Serengeti savannah. Pure as virgin beaches of Zanzibar. Hopeful as a product of Azimio. Sparkling as Tanzanite stone out of the Land of Maasai.

I am a Tanzanian. Born of the peoples of Africa, of Tanzania. The Pains of the struggle of African liberation. The pains of The Revolution. Whatever the setbacks of the moment, nothing can stop me from being a Tanzanian, an African. The land of Kambarage. The state of our own creation. Whatever the difficulties, Tanzania shall remain ONE, Strong and UNITED. However improbable it may sound, Tanzania shall prevail. Amongst nations of the world. We are The United Republic of Tanzania. I am a Tanzanian.
 
- Baba wa Taifa hakumtukana anybody na hata kama tunamsamehe ni mapungufu ya kibiandam na uzee kidogo, lakini kijana mdogo kama Tundu Lissu kusimama mbele ya Bunge la Jamhuri na kuanza kumporomoshea matusi mazito mazito Baba wa Taifa hili na anajua kabisa kwamba mke wa marehemu masikini Mama Maria Nyerere, anayeheshimiwa mpaka na kina Zuma leo amekaa anaangalia Mume wake aliyelala macho kuliokoa hili Taifa kwa wakoloni anatukanwa kama vile hakulifanyia mema hili Taifa, jamani kweli shida yenu ni katiba tu au kuna mengine jamani?

Le Mutuz System

Ndo maana sishangai kila siku watu wanapotilia shaka uwezo wako wa kupambanua mambo.Hivi kwako wewe matusi ni nini?Naona hujielewi coz nimesoma ulichoandika hapo juu sijaona tusi na ambalo hata linafikia nusu ya kashfa ulizommwagia baba yako kupitia kwa ile akaunti yako nyingine ya JF.Probably una definition ya kivyako ya matusi au unajaribu kuvumbua matusi mapya mzee wa Wabebzz
 
I don't know Tanganyika, I have never seen Tanganyika, I don't want Tanganyika I am a Tanzanian.

I am a Tanzanian. Of blood cleaned by fresh waters of the lakes and the rivers and the streams of my great nation. A vision from the top of mount Kilimanjaro and honesty as clear as The Serengeti savannah. Pure as virgin beaches of Zanzibar. Hopeful as a product of Azimio. Sparkling as Tanzanite stone out of the Land of Maasai.

I am a Tanzanian. Born of the peoples of Africa, of Tanzania. The Pains of the struggle of African liberation. The pains of The Revolution. Whatever the setbacks of the moment, nothing can stop me from being a Tanzanian, an African. The land of Kambarage. The state of our own creation. Whatever the difficulties, Tanzania shall remain ONE, Strong and UNITED. However improbable it may sound, Tanzania shall prevail. Amongst nations of the world. We are The United Republic of Tanzania. I am a Tanzanian.

Wenye Zanzibar yao wanaitaka kwa namna yoyote ile sasa wewe utabakia wapi?Misimamo mingine ni kujaribu kuonyesha udhaifu wako wa kupambanua mambo tu.Wenye Zanzibar yao wakiichukua utajiua au utaenda uhamishoni manake hujazaliwa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom