Mwanasheria na Mbunge Wa Chadema Tundu Lissu Atuombe Radhi Taifa Amemdhalilisha Baba Wa Taifa!!

Ukiwa na watu wasomi lakin wanatumia itikadi kufikiri ni kitu cha ajabu sana uwezi ukatoka ulikotoka ukatunga uongo na unafiki juu ya taifa alafu ukaenda kulielezea taifa na kuaminisha watu kuwa unachokisema ni chakweli huu ni upumbavu na utumiaji wa elimu vibaya! Leo hii sisi watanzania tunaona bado hamjapata nchi mshaanza uwongo tukiwapa nchi itakuwaje? Imefikia hatua uwongo na unafiki ukae pembeni tuseme ukweli kuwa chadema ni janga la Taifa tena hasa Tindu lissu! Ni lazima hatua kali zichukuliwe na serikali na watanzania kukomesha huu unafiki. Mwizo Tindu lissu omba radhi Taifa.
 
- Jamani kweli kijana Mtanzania unasimama mbele ya bunge unamuita Baba wa Taifa ni mnafiki kisa na mkasa ni nini hasa jamani katiba tu? haiwezekani lazima kuna mengine nyuma ya pazia he!! khaaaa!!

Le Mutuz System

Hao wamama wa ccm wanao tukana huwaoni?
 
- Unajua mpaka leo siamini kwamba Freeman Mbowe alikuwa amekaa pale anamsikiliza huyu dogo na hakusema kitu. kweli Freeman unaamini baba yako marehemu mzee Aikaeli alikuwa anakubali kusafiri kila kona ya Tanzania na MWalimu huyu anayetukanwa na Mbunge wako namna hii? jamani kweli sasa Chadema mnaitafuta laaana!!

Le Mutuz System


Ha ha haa ama kweli dunia ina mambo, wewe kila siku watu wanakuambia humu mambo ya kukumbatiana na vitoto na kupiga picha unamuaibisha mzee wetu pale Kazembo huwa unajibu nini!!!???????

Kaka hebu acha masihara bana leo umejua matendo ya watoto yanatia aibu wazazi wao au hata kuwafedhehesha!!!?????

Consistent ni taabu sana kwa baadhi yetu humu kumbe!!!!
 
Ha ha haa ama kweli dunia ina mambo, wewe kila siku watu wanakuambia humu mambo ya kukumbatiana na vitoto na kupiga picha unamuaibisha mzee wetu pale Kazembo huwa unajibu nini!!!???????

Kaka hebu acha masihara bana leo umejua matendo ya watoto yanatia aibu wazazi wao au hata kuwafedhehesha!!!?????

Consistent ni taabu sana kwa baadhi yetu humu kumbe!!!!

- Yaani mimi Celebrity kupiga picha na Macelebrity wengine unasema ni sawa na Tundu Lissu kusimama mbele ya bunge na kumtukana matusi ya nguoni baba wa Taifa? Are u serious au unatania?

Le Mutuz System
 
Una uhakika hayo maneno yote uliyoyanukuu yalisemwa na Tundu Lisu? au mengine umeongezea mwenyewe ili kuhalalisha hoja yako?
Wenyewe ndo wanamuona mjanja bonge la Spin Doctor wa Lumumba eti! Papaa Msofe, Alex Masawe haya ni maneno yake mwenyewe akidhani anampaka matope Mhe Lisu! Hoja alizozitoa Tundu Lisu zilikuwa za nguvu kiasi cha Ikulu ikilazimika kutoa nyaraka ya Muungano baada ya miaka 50! Kifuatacho ni kuangalia content za hiyo nyaraka kwa undani zaidi! Hapa napo mtegemee hoja za nguvu kutoka kwake! Kwa tunaojua kinachoendelea tunasema SASA Ngoma Inogile!!! ndo kwanza saa 4! Jiandaaeni vilivyo! Inasemekana Mmeagiza kupewa msaada wa kisheria USA na kuwa Technocrats wako Mwanza wakianza kuwa noa akina Chande et al! Suala la Msingi hapa ni Je? Katiba hii itakuwa ya Marekani au ya Wananchi wa Tanzania?...only time will tell....
 
Hapa kuna watu wanatuchonganisha watanzania!!! Kuitwa mnafiki ni tusi la nguoni? Na yale yanguoni yataitwaje? Unadhani sita angemuacha aendelee na ya nguoni? Tatizo la Viongozi wetu hawataki kuukubali ukweli,na wale wanaoshiba visent vya ccm nao wanatetea pasipokujua wanachokitetea,eti ni mcmamo wa chama!!! Cmamia nafsi yako inavyokutuma cyo mcmamo wa chama. Na sasa mmeanza kuwatisha watu makanisani,etimkikubali serikali tatu nchi itaingia kwenye machafuko kwasababu jeshi litachukua nchi!!! Nakumbuka uzushi huu ulianza toka tulipota kuingia kwenye vyama vingi!!! Lissu hajamtukana matusi ya nguoni baba wa Taifa.Nenda kwenye kamusi ya Kiswahili kaangalie maana ya neno Mnafiki,kisha njoo utuambie tena kuwa ni tusi la nguoni!!
 
- Kaka mbona kama huwa nakuona una akili I mean kusimama mbe;le ya umma kumtukana baba yako aliyetangulia mbele ya haki unasema ni sawa? Kisa katiba tu?

LE Mutuz System

Kaka akili ni relative term ila ukiamua kuipima kwa kukubaliana tu na kila tukitofautiana niwe mjinga pia sawa ila kama ninazo itabaki kuwa hivyo na kama sina bahati mbaya na hasara kwa wazazi na Taifa!!!!

Iko hivi siasa ni mchezo wa hovyo nawe unajua hili wazi na mchana kweupe!!!!!!!!
Kwani kauli za hovyo zimaeanza leo!!!?????


Si tuliambiwa tule nyasi..........ulisema nini????!!!
Watu waliambiwa wapige mbizi ..........unakumbuka!!?????
Watu waliambiwa kama umeme ghali wawashe vibatari...........hukuona!!?????
Juzi mtu kasema hawezi zuia mvua hata angekuwepo.............hukutetea wewe kauli ile?????

Kama tunawachekea tuendelee tu mpaka yatufike makubwa, mimi sina ushabiki wa chama chochote na nasema humu kila siku wanasiasa sio wa kuchukuliwa poa sababu wao na sisi tunaishi tofauti kabisa!!!! Na in real sense wanaishi kwa gharama zetu sisi wavuja jasho.........!!!!

Ndio maana sishitushwi na hayo maneno ni kawaida yao kutukana na wala haitakuwa mwisho, note my words!!!!!!
Na kama kweli una akili hili haliwezi kukunyima usingizi
 
Ninyi mnaouza twiga wake na kuuza madawa ya kulevya sehemu aliyoiita takatifu mbona hamuombi radhi?

Mchwa akitaka kuteketea huvishwa mabawa na kuwa kumbikumbi. That's Tundu Lisu and Chadema. Wameshajiona kuwa ni kumbikumbi wakati ni mchwa. Walitegemea kubebwa na bunge kumbe ndo mwisho wao.
 
Lisu amekosa maadili,huwezi muita baba wa taifa Tapeli au Jambazi,

Nikweli kuwa baba wa Taifa amelifanyia Taifa hili mambo mengi sana ya maana, Binafsi namheshimu sana kwa umoja wetu na uwezo wake wa kuzuia rasilimali zetu kukwapuliwa kama ilivyo sasa! Namkubali zaidi kwa yeye kukiri kuwa kuna MAMBO YA KIPUMBAVU mengi aliyafanya katika utawala wake! JKN alikuwa na mapungufu mengi yeye kama yeye MFANO! Alihakikisha Uchagani watoto hawafaulu hata kama wanaakili kiasi gani! Shule zilizokuwa na Waalimu, mazingira mazuri watoto wenye akili walikuwa wanafelishwa kwa zaidi ya miaka 20 plus bila ya kufaulisha hata mwanafunzi mmoja! AJABU ya Musa watoto hao hao walikuwa wakienda kurudia kwenye shule za Dodoma, singida, shinyanga, mwanza, moro, pwani nk Walikuwa wanafaulu sana! Leo hii utakuta akina masanja wengi ambao ni wachagga! Technocrats wengi wa nchi hii ni wachagga !!! Itoshe kusema JKN alikuwa na mapungufu mengi ikiwemo kuwabania mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kwa saana
 
Tundu lisu anazichangaya sheria halafu anawachangaya na wenzake haya jk alishamaliza kuyasema hivyo hatushangai sana.
 
- Yaani mimi Celebrity kupiga picha na Macelebrity wengine unasema ni sawa na Tundu Lissu kusimama mbele ya bunge na kumtukana matusi ya nguoni baba wa Taifa? Are u serious au unatania?

Le Mutuz System

Ndio hapo sasa uone globalization ilivyoleta kitahanani.....yale wewe unaona sawa wengine wanaona mbaya ile wewe unaona mbaya yeye kasema tena bungeni mbele ya kadamnasi na vyombo vya habari viko on!!!!!! Na hana mpango wa kuomba radhi so kama ni kuvumiliana kijamii basi iende tu mpaka siasani!!!!!

M deadly serious kama Taifa hatujiangalii upya basi iko siku tutasikia mabaya zaidi, wakubwa washike hatamu kujirekebisha wadogo watafuata!!!!!
 
Tundu Lissu.. "yule Nyerere aliishi maisha ya ulaghai,udanganyifu na vitisho kama vile majambazi/matapeli Papaa Musofe na Alex Massawe!?"
tafadhali Le mutuz thibisha kauli hii kama kweli alisema Mh.Lissu vinginevyo mods wafanye utaratibu wa kurudisha hadhi ya jukwaa hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom