Mwanariadha Gabriel Gerald Geay atua Sydney Australia kushiriki mbio za Sydney Marathon Jumapili ijayo

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
310
288
IMG_3646.jpeg
Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania Gabriel Gerald Geay atua jijini Sydney Australia kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa ya Sydney Marathon tarehe 17 septemba 2023 jumapili.

Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha wanariadha zaidi ya elfu arobaini (40,000) wanaotoka katika nchi 66 duniani.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanzia , Bradfield Park, milsons point na kumalizikia Sydney Opera House Forecourt huko Sydney Australia.

Gabriel anakwenda akiwa na muda mzuri wa 2:03:00 kwa mbio za marathon, yaani kilomita 42.195 na akifanya vizuri zaidi itamuweka sehemu bora zaidi.

Pia, kwenye mbio hizi anatarajia kupata donge nono kutoka kwenye kampuni yake (Adidas), kupitia meneja wake.
 
🤣🤣🤣Hawa Watanzania wa kuwaza Simba na yanga hawawezi msapot
Labda angekuwa Max zengeli
Wazee wa kufata upepo
Kizazi Cha vilaza🤣🤣
 
Back
Top Bottom