MWANANYAMALA, DAR: Mtoto ang'atwa na mbwa baada ya mwanamke kumuingiza ktk banda lenye mbwa wakali

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Mwanamke mmoja mkazi wa Mwananyamala anadaiwa kumvuta na kumuingiza ndani ya banda la mbwa Mtoto Mohammed Shaaban mwenye umri wa miaka kumi mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi mwananyamala na kung’atwa sehemu ya mwili wake.

Inadaiwa mama huyo alimkuta mtoto huyo akichungulia getini kwake.

Mbwa waliomshambulia mtoto huyo na kumng’ata ni wa mama huyo, lakini pia mtoto huyo amekosa huduma ya sindano ya kichaa cha mbwa katika hospitali mbili za serikali huku mtuhumiwa akiwa hajachukuliwa hatua yoyote.

Chanzo: ITV
 
Nilikuwa na haraka sikupaona kwenye chanzo asante maan nimerudia kupasoma tena
 
Mwanamke mmoja mkazi wa Mwananyamala anadaiwa kumvuta na kumuingiza ndani ya banda la mbwa Mtoto Mohammed Shaaban mwenye umri wa miaka kumi mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi mwananyamala na kung’atwa sehemu ya mwili wake.

Mbwa waliomshambulia mtoto huyo na kumng’ata ni wa mama huyo, lakini pia mtoto huyo amekosa huduma ya sindano ya kichaa cha mbwa katika hospitali mbili za serikali huku mtuhumiwa akiwa hajachukuliwa hatua yeyote.
Mashuhuda wasimulia.
Hapa ndipo huwa nashindwa kulielewa jeshi la polisi na madaktari wetu kwa ujumla.
Wengi wa Madakatari wa kitanzania kwa ujumla hawana utu. Hawaji kazi zao wala maadili ya kazi zao. Walichoweka mbele ni mkwanja tu. Kuokoa maisha ya watu siyo sehemu inayopelewa kipaumbele na baadhi na madaktari wengi wa Kitanzania. Wao wamejaa kiburi, jeuri dharau na kujiona wao ndio wasomi wakuu. Polisi wetu hivyo hivyo, hawako kwa ajili ya kulinda raia bali wengi wao wanafanyakazi kwa kutanguliza maslahi binafsi. JPM anakazi kubwa pamoja na kujitanabaisha kuwa ana nia ya kubadilisha mfumo wa utendaji kazi serikali. Ina uma sana kuona watu waliopewa dhanmana kuokoa maisha au kulinda usalama wa wananchi wanakuwa wa hovyo namna hii.
 
Hospitali mbili za serikali hazina first aid ya shambulio la mbwa

Tanzania ina mbwa zaidi ya milion 7

Chanjo za mbwa Tanzania ZILIPIGWA stop?

Nadhani huyu mtoto,

Ananikumbusha WATOTO WA MAMA NTILIE, japo siombi Mungu iwe vile
 
Huyo mama anajeuri iliyopta kiasi! Angekuwa mwanangu nahs nisingesubr na hao police maana nao hakna kitu, itakua Mtoto aliingia getin na mbwa wakamsakama! Tz inaweza siasa tu na maslah yao binafsi!
 
Mwanamke mmoja mkazi wa Mwananyamala anadaiwa kumvuta na kumuingiza ndani ya banda la mbwa Mtoto Mohammed Shaaban mwenye umri wa miaka kumi mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi mwananyamala na kung’atwa sehemu ya mwili wake.

Inadaiwa mama huyo alimkuta mtoto huyo akichungulia getini kwake.

Mbwa waliomshambulia mtoto huyo na kumng’ata ni wa mama huyo, lakini pia mtoto huyo amekosa huduma ya sindano ya kichaa cha mbwa katika hospitali mbili za serikali huku mtuhumiwa akiwa hajachukuliwa hatua yeyote.

Chanzo: ITV
Miaka 10 yupo daraja la kwanza?, halafu anachungulia kwenye mageti ya watu?, hebu mjadala uanzie hapo kwanza
 
Hapa ndipo huwa nashindwa kulielewa jeshi la polisi na madaktari wetu kwa ujumla.
Wengi wa Madakatari wa kitanzania kwa ujumla hawana utu. Hawaji kazi zao wala maadili ya kazi zao. Walichoweka mbele ni mkwanja tu. Kuokoa maisha ya watu siyo sehemu inayopelewa kipaumbele na baadhi na madaktari wengi wa Kitanzania. Wao wamejaa kiburi, jeuri dharau na kujiona wao ndio wasomi wakuu. Polisi wetu hivyo hivyo, hawako kwa ajili ya kulinda raia bali wengi wao wanafanyakazi kwa kutanguliza maslahi binafsi. JPM anakazi kubwa pamoja na kujitanabaisha kuwa ana nia ya kubadilisha mfumo wa utendaji kazi serikali. Ina uma sana kuona watu waliopewa dhanmana kuokoa maisha au kulinda usalama wa wananchi wanakuwa wa hovyo namna hii.
Umeandika kwa jaziba. Tatizo la madaktari hapo lipo wapi?
Sindano ya chanjo ya kinga ya kichaa cha mbwa hutolewa kwa baadhi ya hosipitali na siyo kila hospitali. Hapo kutakuwa na uzembe wa kumpeleka mtoto kule hosipitali zinakopatikana chanjo stahiki. Hapo madaktari wamezembea wapi?
Kuhusu hao polisi, mleta mada hakuonesha udhaifu ama ni uzembe gani uliotokea hadi huyo mhalifu kushindwa kutupwa jela.
Sasa kama mtuhumiwa hajaripotiwa polisi, hapo polisi kosa lao hapo pia liko wapi?
 
Wazee hapo hakuna haja ya kulaumu Polisi, hivi hiyo taarifa ilifikishwa kituoni na isichukuliwe hatua?
Mtu yoyote na aipeleke hiyo taarifa kituo cha polisi cha karibu bila shaka hatua zitachukuliwa tu, askar hawawezi kuelewa kila kitu katika mitaa yetu.

Halikadhalika na madaktari. Hivi ni nani mwenye wajibu wa kupeleka dawa katika hospitali za umma? Ss kama jawabu ni hio kosa la daktari ni lipi?
 
Mbwa waliomshambulia mtoto huyo na kumng’ata ni wa mama huyo, lakini pia mtoto huyo amekosa huduma ya sindano ya kichaa cha mbwa katika hospitali mbili za serikali huku mtuhumiwa akiwa hajachukuliwa hatua yeyote.
Chanzo: ITV

Mkuu wa nchi alisema anasoma kila kitu kinachoandikwa, hata katuni za Masoud Kipanya nazo anasoma, hopefully amesoma hii pia na wenye jukumu la kumchukulia hatua mwenye mbwa watakuwa njiani kikazi zaidi sasa hivi
 
Mbona sikuelewi!jamii inatakiwa itoe taarifa kwa mamlaka husika na pia sioni lawama zako kwa madaktari zipo kwa sura ipi,ni ukosefu wa chanjo za kichaa cha mbwa mahospitalini,au kuna mahali panaonyesha uzembe wa kitabibu umefanyika? Suala la ukosefu wa dawa ni tatizo la nchi Nzima. Nenda bohari la dawa lililopo karibu nawe uliza Mara ya mwisho wao kuwa na hizo dawa Zach Kichaa cha mbwa ilikuwa lini. Kama sijasahau Sana ilikuwa ni December mwaka Jana. Tengeneza point zinazoelekea kukosoa au kulaumu palipo na mapungufu. Tusitumie mitazamo na hisia zetu muda wote.
 
Hapa ndipo huwa nashindwa kulielewa jeshi la polisi na madaktari wetu kwa ujumla.
Wengi wa Madakatari wa kitanzania kwa ujumla hawana utu. Hawaji kazi zao wala maadili ya kazi zao. Walichoweka mbele ni mkwanja tu. Kuokoa maisha ya watu siyo sehemu inayopelewa kipaumbele na baadhi na madaktari wengi wa Kitanzania. Wao wamejaa kiburi, jeuri dharau na kujiona wao ndio wasomi wakuu. Polisi wetu hivyo hivyo, hawako kwa ajili ya kulinda raia bali wengi wao wanafanyakazi kwa kutanguliza maslahi binafsi. JPM anakazi kubwa pamoja na kujitanabaisha kuwa ana nia ya kubadilisha mfumo wa utendaji kazi serikali. Ina uma sana kuona watu waliopewa dhanmana kuokoa maisha au kulinda usalama wa wananchi wanakuwa wa hovyo namna hii.
Madaktari wamefanya kosa gani kwa huyo mgonjwa?
 
Huyo mama anajeuri iliyopta kiasi! Angekuwa mwanangu nahs nisingesubr na hao police maana nao hakna kitu, itakua Mtoto aliingia getin na mbwa wakamsakama! Tz inaweza siasa tu na maslah yao binafsi!
Dah...halafu kesho unaambiwa mwanao ni bonge la kibaka.... Na hapo alikuwa anaspy ili akawape ramani wazee wa kazi
 
Back
Top Bottom