Mwanamke SHANGINGI...............

Nilikuwa Tanga miaka ya hivi karibuni tumekaa sehemu sehemu basi wakapita madada walikuwa wanne wamevaa kiajabu ajabu na pia walikuwa wamejisiliba kupita kiasi. Basi dada mmoja katika kundi letu akasema, "Angalia wale makunyuu." mie nilikuwa sijawahi kulisikia hili neno nikauliza makunyuu ndio maana yake nini? Basi yule dada akajibu Kunyuu ni juu ya Shangingi au kwa maneno mengine Shangingi haoni ndani kwa Kunyuu.... mie nikabaki kushangaa shangaa tu.

dah..makunyuuu tena? lol
 

Asante kwa ufafanuzi ila nitakuwa na maswali machache -"USTAARABU" ni nini? "TABIA MBAYA" ni nini"

Umesema "Watu wa Kariakoo" walikuwa "wastaarabu" kabla ya watu wa "bara" kuwavamia huko "uswahilini" kulikokuwa na "ustaarabu"! Ina maana watu wa bara hawakuwa na "ustaarabu" na ndiyo maana walipochanganyika na watu wa "Kariakoo" ikatokea "tabia mbaya"?

Nitakuambieni kwanini "uswahili" unadharaulika.

Ukiangalia mentality ya watu wa Pwani, hasa DSM utaona wana kijitabia cha kudharau watu wa bara. Na kigezo chao kikuu ni kujifanya wanajua kukunja chapati, kunywa kahawa na kucheza bao wakiwa wamekunja miguu kwenye mikeka! Hili sijatunga mimi.Aliwahi kusema Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ( R.I.P) kwamba watu wa bara washamba wakuja hawajui kukunja chapati! Hivyo haya siyo maneno yangu bali ya watu wa Pwani. Sitaki kuamini hivyo ndivyo vigezo vya USTAARABU!

Kitu kingine,
utaona kwamba watu wa Bara wamekuwa wanadharauliwa sana na hawa "waswahili" kwa kisingizio ati wabara hawana "ustaarabu" na ndio maana nauliza "ustaarabu ni nini? Wabara walikuwa na haki kuja DSM na kwingineko kwani ni Watanzania. Kwamba wameenea kila kona ya DSM siyo kosa lao. Wenyeji wa DSM wanajiita "wenyeji" ukiwachunguza, hawakuzaliwa DSM.
Hoja yako ya wazungu kuja na kugawa matabaka - Uzunguni, Uhindini na Uswahilini - Ukichunguza utaona kuwa tabaka ziliwekwa kufuata "race" au rangi - USWAHILI siyo race! UAFRIKA ndio race.Jiulize kwanini kusiwe "Uafrikani" kukawa "uswahilini"? Food for thought!Characterists za uswahilini ni nini?
Kila mtu anakimbilia kukaa uzunguni, uhindini lakini hakuna anayekimbilia kukaa "uswahilini" badala yake kila mtu "anatafuta kukwepa uswahilini".

Niachie hapo.Nitarudi ikibidi. Tusichakachue mada ya Boss on Mashangingi.

Hapo kwenye blue, ukiona post za nyuma ndio kitu kimenisukuma kujibu hayo majibu uloyaona, nadhani hujasoma post tokea mwanzo ili uone jinsi "Waswahili" walivoshambuliwa na kubezwa, kuna mmoja amesema mashangingi yapo uswahilini, mwengine akasema vibaka wapo uswahilini.

Mimi kama MSWAHILI PURE ! kweli limenigusa kwa sababu nimekulia huko uswahili (Kariakoo) na kulikuwa hakuna hizo tabia ! tulikuwa na mila na desturi zetu za Kiswahili ambazo ndio zimetulea na kutufikisha hapa tulipo! Mapenzi na uungwana kwa yeyote yule awe mswahili mwenzio au mgeni !

Na nina hakika, umejibu post hii baada ya kuona "Mswahili" mimi nikijaribu pia kuelezea hisia zangu juu ya jinsi ustaarabu wetu wa Kiswahili ulivoingiliwa na makabila tofauti.


Na naweza kutolea mfano, zamani Waingereza walikuwa na mila na desturi zao! hili halipingiki, lakini sasa hivi na wenyewe wanalalama kuwa wameingiliwa na watu wa aina tofauti na kuziua kabisa tamaduni zao!

Na hapo katika nyeusi, nadhani huko uswahilini Kariakoo na magomeni mpaka Ilala (HAILALLAH) kila mtu anataka awe na nyumba sasa hivi maana HAPAKAMATIKI! kwa hilo tunashukuru Mungu sisi tuloachiwa vijijumba vichache baada ya vingine kuuzwa kwa kuogopa kutaifishwa na nyerere na azimio lake la arusha....

KAma ulivosema tusichakachue huu uzi...mada ni mashangingi.
 
Mfano mzur wa shangingi ni yule mdada alieshrikishwa kweny nyimbo ya msanii A.T(VIFUU TUNDU).maana maneno yao yanafanana sn ya huy mdada coz yamekaa kipashupashu!"mwanamke mbeya utamjua tu mdomo wake, mweusiiii km kunguru"."umeona wap nyumba ya udongo ikapigwa deki,inahu...!!!horii weeee!!!"
 
ni mmama au mdada mwembamba/mnene, anayependa kujiweka soap soap, mjanja mjanja, huwezi kumlaghai kirahisi, mchesi

anaependa kwenda na wakati, anapenda vitu vizuri, anauwezo wa kuongea na yeyote, bila hofu yoyote kwa kifupi wana confidence sana. anaweza kuwa malaya au sio malaya itategemea mapenzi yake kuhusu ngono
 
inawezekana shangingi anakuwa na tabia za zaidi ya umalaya wa kawaida - labda u-tigo ndani!
 
ni mmama au mdada mwembamba/mnene, anayependa kujiweka soap soap, mjanja mjanja, huwezi kumlaghai kirahisi, mchesi

anaependa kwenda na wakati, anapenda vitu vizuri, anauwezo wa kuongea na yeyote, bila hofu yoyote kwa kifupi wana confidence sana. anaweza kuwa malaya au sio malaya itategemea mapenzi yake kuhusu ngono

ni kama unasema a confident woman ndio shangingi?????
 
The Boss, shangingi huwezi kumpata kwa definition. Utamjua kwa lifestyle yake. Na sio tendo moja au mbili, ni sequence fulani ya matendo, namna yake ya kusema, ya kucheka, ya kufikisha habari, ya kureact akishangaa, akifurahi, akichukia etc.
Kwa hiyo ushangingi ni lifestyle... ngumu kuidefine kwa kweli.
Njoo huku mabaoni niku-introduce kwa ulimwengu huo uwaone. lol
 
Mashangingi yana nyama hayo!!gemu lao ni noma..wako vizuri sana kumfulaisha mwanaume.
 
Back
Top Bottom