Mwanamke mwenye hekima uijenga nyumba yake

Showmax

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
6,594
12,579
Methali 14:1-18
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Mwenye mwenendo mnyofu humcha Mwenyezi-Mungu, lakini mpotovu humdharau Mungu. Mpumbavu hujiadhibu mwenyewe kwa kuropoka kwake, lakini mwenye hekima hulindwa na maneno yake. Bila ng'ombe wa kulima ghala za mtu ni tupu, mavuno mengi hupatikana kwa nguvu ya ng'ombe wa kulima. Shahidi mwaminifu hasemi uongo, lakini asiyeaminika hububujika uongo. Mwenye dharau hutafuta hekima bure, lakini mwenye busara hupata maarifa kwa urahisi. Ondoka mahali alipo mpumbavu, maana hapo alipo hamna maneno ya hekima. Hekima ya mwenye busara humwonesha njia yake, lakini upumbavu wa wapumbavu huwadanganya wenyewe. Wapumbavu huchekelea dhambi, bali wanyofu hupata fadhili kwa Mungu. Moyo waujua uchungu wake wenyewe, wala mgeni hawezi kushiriki furaha yake. Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa, lakini hema ya wanyofu itaimarishwa. Njia unayodhani kuwa ni sawa, mwishoni yaweza kukuongoza kwenye kifo. Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi. Mtu mpotovu atavuna matunda ya mwenendo wake, naye mtu mwema atapata tuzo la matendo yake. Mjinga huamini kila kitu anachoambiwa, lakini mwenye busara huwa na tahadhari. Mwenye hekima ni mwangalifu na huepa uovu, lakini mpumbavu hajizuii wala hana uangalifu. Mwenye kuwaka hasira haraka hutenda kipumbavu, lakini mwenye busara ana uvumilivu. Wajinga hurithi upumbavu, lakini wenye busara hutuzwa taji ya maarifa.
Mwanamke mpumbavu ubomoa nyumba yake mwenyewe kwa kinywa chake kiwakacho moto na kutema sumu kama fira.
Ameen
 
Back
Top Bottom