Mwanamke Mnyenyekevu Vs Mwanamke Mtumwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
MWANAMKE MNYENYEKEVU Vs MWANAMKE MTUMWA

Anaandika, Robert Heriel
Mume.

Wanaume wote Duniani wanapenda Mwanamke mnyenyekevu, lakini wapo wanaochanganya unyenyekevu na Utumwa. Kwa kweli wengi wanaposema Unyenyekevu humaanisha Utumwa. Wanahitaji Mwanamke mtumwa.

Mwanamke mnyenyekevu ni Nani?
Mwanamke mnyenyekevu ni Yule anayefuata misingi ya MKE, utiifu, heshima na adabu na Maadili yote ya Mwanamke.
Unyenyekevu ni kujishusha na kuwa mtiifu.

Lakini Kunyenyekea Kwa Nani na katika mazingira Gani? Unyenyekevu na utiifu lazima ufanyike Kwa MTU sahihi, muda sahihi na katika mazingira sahihi. Endapo unyenyekevu hautafanyika katika MTU sahihi, muda sahihi na mazingira sahihi basi utahesabika kama UTUMWA!

Mwanamke mnyenyekevu lazima amtii na kumuinamia Mwanaume mwenye upendo, mwenye Akili, na mwenye Kutenda HAKI.
Ikiwa mwanaume anakupenda, anaakili na anatenda Haki. Huyo mnyenyekee. Lakini akikosa kimojawapo hapo basi ni hakika atakufanya MTUMWA.

Wanaume wengi wanawanyanyasa Wanawake Kwa kisingizio cha uanaume wao. Wakiwataka Wanawake wanyenyekee hata kama wanawatendea isivyo Haki. Huo sio unyenyekevu Bali ni kufanyana watumwa.

MKE wangu, endapo nitakufanyia Isivyo Haki, nikafanya mambo yasiyo na Akili, na nikaonyesha sikupendi basi nakusihi usininyenyekee wala usinipe Utiifu wala heshima. Kwani haitahesabika kama unyenyekevu Bali UTUMWA.
Halikadhalika Taikon nawausia Binti zangu, Dada zangu, Mama zangu ikiwa mwanaume atakufanyia mambo yasiyo ya Akili, yasiyo na Haki na akaonyesha hakupendi usimnyenyekee wala kumuonyesha utiifu na heshima kwani huo NI UTUMWA!

Sisi Watibeli hatupendi kugeuza wengine Watumwa wetu, na wala hatupendi kugeuzwa Watumwa wa Watu wengine.

Familia lazima iwe na sheria. Na watu wote wawe sawasawa Chini ya hizo sheria mtakazoziweka. Baba kama Mtawala na Kiongozi wa familia lazima awe mfano WA kuzifuata hizo sheria zilizowekwa.
Hiyo ndio Haki, Akili na upendo ambao mwanaume lazima aonyeshe.

Mfano endapo Mume amezuia MKE asitaniwe na Wanaume au asiwe na mazoea na wanaume wengine basi sheria hiyohiyo aliyoiweka ifanye kazi pia na kwake. Kwamba naye asiwe na mazoea na utani na Wanawake.

Huwezi ukamnyenyekea MTU mwovu, mhalifu, na asiyetenda HAKI, asiyefanya mambo Kwa Kutumia Akili, na asiye na upendo. Huyo anakugeuza Mtumwa.
Hata Mungu mwenyewe Hana uwezo wa kugeuza Watu watumwa sembuse MTU.
Mungu hawezi kugeuza Watu watumwa Kwa sababu ni Mungu mwenye Upendo, Haki na mwenye AKILI.

Mfano, Unapika au unafua jikoni alafu Mumeo amekaa sebuleni anakuita umletee Gazeti ambalo lipo pembeni yake umbali wa hatua tano tuu. Huyo Mwanaume ni bwege, mpuuzi, Hana Akili, ni ngumu Sana kumheshimu na kumnyenyekea mtu wa Aina hiyo. Huo ni UTUMWA.
Labda awe anaumwa.

Haya umetoka umeenda Shopping, huku nyumbani umemuacha Mumeo na mtoto. Mtoto kamwaga maziwa sakafuni au kajikojolea, Mumeo Kwa vile ni hamnazo atakusubiri mpaka urudi kisa na mkasa kazi ya kufuta maziwa sakafuni amei-term kama ya kike.

Haya wote mpo nyumbani, ni Asubuhi. Kazi zipo nyingi. Kuna kusafisha nyumba, kuna kufua, kuna kuosha vyombo, kuna kupika kifungua kinywa, Badala musaidiane na Mumeo kuzipunguza Kazi ili mnywe chai Kwa pamoja, Mumeo anakuachia zote ambapo automatically mtachelewa kunywa chai au Yeye atakunywa pekeake huku MKE akiendelea kumalizia kazi zingine.

Alafu muda huohuo atakulaumu Kwa nini chai inachelewa kana kwamba Hana Akili ya kujua ni Kwa nini chai inachelewa. Hapo automatically lazima mafarakano yawepo. Unyenyekevu lazima ukae mbali na eneo hilo na Utumwa uanze kushamiri.
Ndoa inahitaji upendo, Haki na Akili ili wenza waweze kushirikiana. Ndoa ni ushirikiano.

Mwanamke mnyenyekevu anaruhusiwa kutoa Maoni yake, anauhuru wa kufanya uchaguzi na maamuzi kupitia mjadala.
Kwenye familia inayoongozwa Kwa Upendo, Haki na Akili Uhuru ni Jambo la lazima.
Wakati Mwanamke mtumwa ni kama Mdoli tuu, haruhusiwi na Hana Uhuru WA kutoa Maoni yake. Mwanaume ndiye anatoa kauli Kwa kila kitu pasipo hata kumshirikisha Mkewe Kwa sababu Mkewe anamuona kama mtumwa wake. Kikawaida Watumwa hawashirikishwi na Mabwana zao.

Taikon kama Watibeli wengine tunaamini katika Uhuru wa kimawazo, mijadala, na Maoni. Wazo au Oni zuri lenye Akili na Haki na lenye upendo ndio familia yetu itafuata wazo Hilo bila kujali limetoka Kwa Mume, MKE au Mtoto(kama amefikisha umri wa kuweza kuchanganua mambo).

Huwezi kusema Mimi kama Baba nimesema Jambo hili lazima lifanyike hivi au vile alafu ukiangalia Jambo lenyewe halina kichwa wala miguu alafu unataka Mkeo akunyenyekee ati kisa tuu wewe ndiye Baba kichwa cha nyumba. Huko ni kufanyana watumwa. Ni kujenga familia za kitumwa.
Inashauriwa Kabla mwanaume hajaleta shauri ndani ya familia lazima uwe umelitafakari Kwa kina ili unapolileta uweze kulitetea Kwa Hoja nzito zenye mashiko kiasi kwamba Mkeo na watoto au MTU yeyote akisikia akubaliane na wewe. Na sio utumie Mabavu.

Mwanamke mnyenyekevu Hapigwi lakini Wanawake watumwa wanapigwa na Waume zao.
Huwezi mpiga Mwanamke mnyenyekevu ndoa ikabaki salama.
Unampiga Kwa sababu ipi hiyo.
Mwanamke mnyenyekevu anajua wajibu wake, anajua Haki zake, anaakili. Kamwe hawezi kubali kupigwa Kwa sababu za kijinga na wanaume wapumbavu wasiojua mipaka Yao na wanaendeshwa na mihemko.

Mfano, umechelewa kurudi nyumbani, tena umelewa na Mbaya zaidi unanukia manukato na marashi ya kike. Mkeo anakuuliza unaanza kufokafoka na Kumpiga. Hiyo Kwa Sisi Watibeli Wanawake wetu hawatakubali Jambo kama Hilo litokee.
Badala ujibu Kwa Haki, upendo na Akili unaleta wendawazimu na uchizi wako.
Binti zangu, Dada zangu, wake zangu, Mama zangu msikubali Jambo kama Hilo kutokea.

Au Mmeshaweka sheria za mapato na matumizi ya Familia. Pato la familia linajulikana, kila mmoja anachozalisha kinafahamika na kinapaswa kuwasilishwa kwenye hesabu za siku au mwezi au Mwaka za familia yenu. Alafu Mwanaume anaulizwa Pesa kapeleka wapi Hana majibu yanayoeleweka. Hapo hakuna Familia.
Hiyo familia ni Bora ivunjwe Kila MTU Aishi kivyake na masuala ya malezi ya mtoto kuhusu matunzo yawekewe utaratibu kulingana na sheria za nchi au dini.
Peleka Mahakamani. Mkishindwa kuheshimu sheria mlizojiwekea Watu wengine (Mahakama) watawawekea na kuwalazimisha kufuata Kwa Nguvu.

Sheria za Mawasiliano ikiwemo mambo ya Simu na mitandao yakijamii.
Watu wenye Haki, Akili na upendo wanashikiana simu pasipo shida yoyote Ile.
Hakuna sababu hata Moja yenye mantiki inayoweza kuzuia wanandoa wasishikiane simu au mitandao ya kijamii. Hakuna hata Moja yenye usafi.
Sababu zinazopelekea wanandoa wasishikiane simu ni zile negative zote;
1. Ukosefu wa uaminifu, Utapeli na unafiki.
Jitu linajifanya linakupenda, ninyi nyote ni kitu kimoja na Mwili mmoja lakini hapohapo linakuzuia usishike simu yake. Hivi kuna unafiki wa kiwango cha juu kama huo?
Watibeli huwaga hatuna chakuficha, simu tunatumia wote hiyohiyo moja au zote mbili tunaweza kuachiana.
Uaminifu ni Sehemu ya Haki na Upendo.

Unageuka mtumwa Kwa kuhangaika kuficha simu, Mkeo au Mumeo akishika simu yako Roho inakutoka mpaka uhasama unazuka.
Hakunaga familia Bora yenye uaminifu inayojengwa Kwa namna hiyo. Isipokuwa inaitwa familia za kinafiki zinazozalisha kizazi cha Wanafiki na watumwa.

Huenda ikawa Taikon anaongea mambo magumu kutekelezeka lakini Watibeli mambo hayo ni mepesi Kwa sababu ni Haki, upendo na Akili na yanatufanya tuishi Kwa Amani na furaha. Na wale wanaoishi pamoja nasi hujihisi Salama na Amani na kamwe hawawezi kujihisi watumwa..

Ni Yule Mume Kutoka Tibeli Nyota yenye mbawa mbili irukayo Kutoka Ulimwengu mmoja mpaka mwingine.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
sawa
main-qimg-faf10c55e85353d0079b24c4fa140b7b.gif
 
Sawa
 
Kwa kuwa umetushambulia bila angalizo la Mila na desturi zetu nimeshindwa kuisoma yote natafakari umakusudi wa nia ovu ya kupotosha Mila na desturi maana mwanamke anameza ni mgumu kudigest issues.

Umeleta ujumbe wa kuimarisha kibri, jeuri na dharau na kwa msingi huo unakubaliana na sisi majabali na magwiji wa KATAA NDOA KATAA KuOA
 
Ulichokiandika ni sawa unawaelekeza wanawake waendelee kuwa viburi kwa waume zao.

Hivyo mtoa mada natarajia nawe utahusika kuwa chanzo cha baadhi ya ndoa kuvunjika na kuongeza idadi ya singo Mother hapa Duniani
 
Kupenda haki, upendo na Akili sio kuwa na Kiburi Mkuu.
 
Kwa kuwa umetushambulia bila angalizo la Mila na desturi zetu nimeshindwa kuisoma yote natafakari umakusudi wa nia ovu ya kupotosha Mila na desturi maana mwanamke anameza ni mgumu kudigest issues.

Umeleta ujumbe wa kuimarisha kibri, jeuri na dharau na kwa msingi huo unakubaliana na sisi majabali na magwiji wa KATAA NDOA KATAA KuOA

Na NI kwani Isiwe kumarisha Haki, upendo na AKILI.
Kwa nini Wanawake wanaodai hayo huonekana wanakiburi, Jeuri na dharau?
 
Kuna vita ya kisiri kati ya wanaume na wanawake. Ila naona wote wamejeruhiwa, wameumizwa moyo, wanashindwa kusamehe, wanasuburi kulipiza kisasi kwa mwenzi mpya
 
😀😀😀

Sehemu yoyote isiyo na Haki basi Kisasi ni lazima.
Tatizo la Kisasi cha Mwanadamu kinaumiza hata wasiohusika. Kwa hiyo inakuwa ni endless circle ya revenge
 
Na NI kwani Isiwe kumarisha Haki, upendo na AKILI.
Kwa nini Wanawake wanaodai hayo huonekana wanakiburi, Jeuri na dharau?
Kutenda kinyume na maagizo ya MUNGU ndio chanzo cha kuona kama ndoa ni utumwa.
  • Waefeso 5: 22-23 (Enyi wake watiini waume zenu, Mume ni kichwa cha mkewe)
  • 1 Petro 3:7 (Mke amtii mume na mume ampende mke wake)
 
Na hapo nimeeleza Mume anayepaswa kutiiwa na Mkewe anapaswa awe mwneye upendo, Haki na mwenye Akili.
Kama Hana hizo Sifa Hana thamani ya Kunyenyekewa na Mkewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom