Mwanamke kukuweka sero anastahili kusamehewa?

Mimi wife nilishamwambia hata itokee tumegombana au nimemuudhi vipi, asije akajaribu kuniweka ndani hata kwa dakika moja maana ndio itakuwa mwisho na hakuna atakayeweza kunibadilisha hata akusanye ndugu zangu na zake combined.
Umetisha brooo
 
Hili ni jambo zito sana. Nakushauri utulize kwanza kichwa chako. Pia pata muda wa kuzungumza kwa kina na mwenza wako. Kwa masimulizi yako, natamani kukushauri usimsamehe, umpige chini. Lakini sifanyi hivyo kwa kuwa natambua utakapokuwa unayaishi matokeo ya maamuzi yako, sitokuwepo kukusaidia. Tuliza kichwa mkuu. Zungumzeni kwa kina pasi unafiki. Mwishowe, utafanya maamuzi ambayo katu hutoyajutia.
 
Mimi wife nilishamwambia hata itokee tumegombana au nimemuudhi vipi, asije akajaribu kuniweka ndani hata kwa dakika moja maana ndio itakuwa mwisho na hakuna atakayeweza kunibadilisha hata akusanye ndugu zangu na zake combined.

Kwani usipobadilika utamkomoa nani? Hata yeye Si atamove on tu!
 
Kama mlipigana akakupeleka polisi na umeshapata dhamana nadhani ni muda muafaka na wewe kumpeleka police ili ajue ubaya wa case,hiyo sio ya kujiuliza mara mbili utajikuta unaingia ngome bila kutegemea.

Huwezi mpeleka mwanamke Polisi yeye ndiyo anakupeleka!
 
ingelikuwa amekukuta umelala na kuamua kukupeleka polisi ningekushauri umwache,lakini sasa angalia mlikuwa mnalumbana naye katika kujihami akaona akuleke selo,by the way mke huwa hapigwi makofi ila hupigwa kwa mapambo,maua,mavazi na maneno matamu.
 
Usiseme tulipigana. Ulimpiga mkeo. Kwanin na wewe kabla hujampa kipondo usiite ndugu kwanza.. Mkuki kwa nguruwee!!!!
 
Usiseme tulipigana. Ulimpiga mkeo. Kwanin na wewe kabla hujampa kipondo usiite ndugu kwanza.. Mkuki kwa nguruwee!!!!

Weweee mi nimekupenda bureee, na kupigana tusidanganyane, hauanz kwa siku moja kumdundaaa, ulianza kidogo kidogo kumstua na vibao, ndio maaan kaona utazoea, alijitutumua ndani ukamzidi. Mi naona POLISI ILIKUA HAKI YAKO ili akili yako ikae sawa. KUMBUKA hta ukimuacha hyo sk hz hamna mwanamke anayekubali unyanyasaji wa kijinsia, utandawazi huuu we mpige tu uone nn kitafuata.
 
Achana nae,watu wanashauri ujinga humu,wewe hustahili kusamehewa ila yeye ndo anastahi,halafu yeye hana makosa ila wewe ndo una makosa?mfumo dume lazima uwepo tu,kama wewe mwanamme halafu unapinga mfumo dume unakua na akili kama ccm,kwani mungu alivyoanza kumuumba adamu alikosea? Sasa huko makanisani na misikitini mnaenda fanya nini?
 
Huwezi mpeleka mwanamke Polisi yeye ndiyo anakupeleka!
Lakini mdau hapo juu kasema “walipigana" sio kwamba yeye alimpiga mwanamke akakaa kimya,kama walipigana ni haki yake naye kwenda police kuripoti nakufungua kesi pia kupeleka malalamiko dawati la jinsia ili asikilizwe isiwe ni kesi ya upande mmoja..kuwa mwanamke sio kwamba afanye fujo ndani ya nyumba mkorofishane yeye akimbilie polisi mwanaume uogope kwamba nawewe huwezi kumreport,ndiyo maana tuna madawati ya malalamiko kwenye vituo vya usalama.
 
Nina mke tumeishinaye kwa miaka kadhaa juzi kati imetokea kutoelewana kati yetu ugomvi wetu ulikuwa mkubwa kiasi cha kupigana japo hakuna aliyeumia kati yetu, baadaye alikimbia police na kufungua kesi ya shambulio nilikamatwa na kuchukuliwa maelezo na kuwekwa ndani kesho yake kaja na ndugu zangu kama watatu akiomba msamaha na mdhamana nisiende mahakamani baadaye nilidhaminiwa. Je huyu binadamu anastahili msamah? Au nimpotezee maana alikuwa na nafasi ya kushirikisha ndugu kabla ya yote.
Kumpiga mwanamke ni udhaifu namba 1.
 
Napenda sana wanaume wajinga wanapoumia roho baada ya mtenda kutendewa, unabahati alikutoa, mie usingeniona na ndugu taarifa hakuna kupewa mpaka uzoee kunyea debe. No man shall ever lay a finger on his wife, Period.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Ndoa si kwa kila mtu, kwako ili kukidhi maneno yako ni bora uwe single for life lakini mwanamme alizaliwa na mwanamke hawezi kushindwa kugusa mwili wa mama yake either kwa mapenzi au ushenzi
 
Ndoa si kwa kila mtu, kwako ili kukidhi maneno yako ni bora uwe single for life lakini mwanamme alizaliwa na mwanamke hawezi kushindwa kugusa mwili wa mama yake either kwa mapenzi au ushenzi
Kugusa ndio kupiga kama hujui lugha usichangie, kama uelewa jitahidi kuelewa....
 
Ni scanie vyeti vyako nione kiswahili ulipata ngapi ndo tuendelee kujadiliana, scan vya form four tu vingine sihitaji
 
Nina mke tumeishinaye kwa miaka kadhaa juzi kati imetokea kutoelewana kati yetu ugomvi wetu ulikuwa mkubwa kiasi cha kupigana japo hakuna aliyeumia kati yetu, baadaye alikimbia police na kufungua kesi ya shambulio nilikamatwa na kuchukuliwa maelezo na kuwekwa ndani kesho yake kaja na ndugu zangu kama watatu akiomba msamaha na mdhamana nisiende mahakamani baadaye nilidhaminiwa. Je huyu binadamu anastahili msamah? Au nimpotezee maana alikuwa na nafasi ya kushirikisha ndugu kabla ya yote.
Umekoma bwana , wengi mnahitaji kupelekwa selo.
kama unampenda mnasongesha life tu.
 
Back
Top Bottom