Mwanamke: Je utayaangaliaje mafanikio ya bwana uliyeachana naye akiwa na mpenzi mwingine….?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,811
15,404
url1.jpg

Kuachwa huwa kunauma sana, na hasa inapotokea uliyeachana naye ulizaa naye, na hapo ndipo unapojikuta ukilazimika kuwa na mawasiliano na bwana huyo kwa takriban miaka 18 hivi.

Hebu tuchukulie hujapata mwenza na huyo mpenzi wako amekwishaoa. Je Utayachukuliaje mafanikio ya huyo mzazi mwenzako katika maisha yake ya ndoa ……………..?

Je wewe ni aina ya wanawake ambao humudu kujenga uhusiano bora na bwana aliyeachana naye bila kuathiri maisha yake ya ndoa na mwenzi wake au ni aina ya wanawake ambao hutafuta kila namna kwa mawio na machweo ili kuhakikisha wanavuruga ndoa ya bwana waliyeachana ili kumkomesha………….?
 
Maisha ya kijamii ni 'complicated' kidogo


Kuvuruga mahusiano ya mtu uliyeachana naye kwa makusudi ni kiashiria tu cha aina ya mtu
Ni mtu anayekubali kushindwa? Ni mtu wa kisasi? ni mtu wa roho ya kwa nini?

Hata katika kazi, kuna watu wanapenda 'kuharibia' wengine ni kama anasema 'bora tukose wote'

Hii haisababishwi na maumivu ya mahisiano tu
Mie naichukulia inaonesha 'personality' ya mtu kwa ujumla akiwa under pessure
anaweza kufanya maasi kwa umbali kiasi gani.
 
Katika safari nzima ya mapenzi mpaka ndoa, misukosuko huwa ni jadi, mingi zaidi huletwa na athari za mapungufu ya mmoja mmoja, ni wachache wanaoona na kukubali kubadilika na wengi hufumba macho kudhani matatizo/msukosuko hupita tuu, bila kufanya lolote
wanaoshindwa kutatua huishia kuachana,na yule aliesababisha ama ni mwanamke/ume marazote humwona mwenzake ndo chanzo na dua zake siku zote huwa ni mabaya
 
Inategemea na aina ya mwanaume uliyemuacha, kama alikiwa ngumi mkononi anakupiga hadi mtaa wa tatu unajua, au mwanaume malaya kupitiliza, au kama mwanaume hana msimamo amejaa ghubu hajiamini, au mama's boy hakuthamini unadhani ukiachana nae utamfuatilia? Kwanza ndo utazidi kumuombea na mkewe washikamane asikusumbue tena..
 
Hii mada inanihusu kiasi kikubwa, mdada aliyezaa na mtu wangu ananipa shida sana ananisingizia mengi mara nampgia simu za kumchamba, wakati hata namba yake ya simu sina na wala sina mpango wa kuijua yaan ananikwanza utafikiri mi ndo nilimfanya mpaka akaachwa, kweli changamoto izo zipo na si lingine linalowapa tabu walioachwa bali wivu.
 
kama mlikuwa na good time nzuri ni wazi utaumia sana unapokumbuka enzi hizo
 
Kweli hata kama ameshapata mwingine nitajaribu uhusiano wetu uwe ule unaohusiana na mtoto zaidi ya hapo sina ulazima wa kutaka kujua habari zake. In case by accident it happens, mafanikio yake nitayapima kama anamuonekano wa utulivu na aliyekuwa nae, ofcoz kikaz, mali na muongezeko wa watoto ambao wanaonyesha wanalelea katika familia bora.
 
ndoa huwa hatari sana wapendanao wanapoachana kikubwa naomba uvumilivu ndio swala la muhimu kwa kila mmoja
 
khaaa! hii ni staili ya roho ya korosho tu manake si kwenye mapenzi tu ha kaazini ila watu kama hawa huwa hawafanikiwi kabisaaaa.
 
Back
Top Bottom