Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 666
Mwanamke hupenda na kuacha kupenda taratibu.
Ukiachana na mwanamke kicheche au kuwa anakulipizia baada ya wewe kumsaliti, mwanamke mpaka akuache lazima kuna sehemu ulianza kutetereka. Akakuvumilia akiamini utabadilika lakini wapi. Sasa amekuacha unaona ghafla lakini kamwe sio ghafla alianza taratibu ila haukumsoma vizuri. Pengine alikua anakuambia kabisa lakini ulikua haumtilii maanani.
Chanzo kikubwa cha kutetereka ni kubweteka.
Hii ni pale ambapo unaona umeshampata mwanamke (/mke) hivyo huna haja ya kuhangaika kwa kuwa unaona umeshaweka chombo ndani. Inawezekana umepunguza kumpeti tena kama zamani, au umemuachia uongozi yeye wa kufanya maamuzi. Mfano, kumuuliza maswali kama “leo twende wapi mpenzi” wakati we ndo inabidi uchague pa kwenda naye. Atakusaidia uongozi kwa muda lakini hatoufurahia, mana ameumbwa kuwa mfuasi wa kiongozi na sio kuwa kiongozi wa mhusiano.
Hivyo ni muhimu kujiangalia kwanza kabla ya kumlaumu mwanamke.
.
Okay, limeshatokea nini cha kufanya?
Cha kwanza, kata mawasiliano naye, USIMTAFUTE kutaka kujua chanzo cha kukuacha au amekula nini leo. Mwache maana ameshafanya hayo maamuzi, pia hata huyo aliyenae saivi akitetereka atakutafuta tu wewe.
Pata muda wa kupoza moyo. Ila jitahidi hayo maumivu yasikuendeshe mpaka watu (hasa huyo mwanamke) kuona umeanza kuchanganyikiwa.
Usitafute mwanamke kwa kulipizia kuachwa ila tafuta mwanamke kwa lengo lako kujenga naye maisha.
Pili, mrudie Mungu, na umwombe akupe baraka upate amani na mwanamke atakayekupa amani.
Tatu, jiendeleze kazini, tunza mwili wako na kufurahia maisha.
Hakikisha hata kama ni ngumu vipi mpotezee, mana tayari amekuonesha alivyo, je ungependa uendelee naye kwenye ndoa baada ya kukuonesha alivyo?
Inawezekana huyo ameondoka ili aje mwanamke bora zaidi, hivyo usikate tamaa kwa kuwa utampata aliyebora zaidi yake, cha muhimu ni kujiendeleza.
Nikutakie weekend njema na maandalizi mema ya wiki ijayo.