Mwanamke akutwa na bunduki Sumbawanga

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Shangwe Lodrick (35) Mkazi wa Bangwe Kata ya Izia Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya Shotgun iliyotengenezwa kienyeji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Shadrack Masija amesema "Kupitia taarifa fiche Askari walifika nyumbani kwa Mtuhumiwa kukiwa na taarifa za kwama anajihusisha na matukio ya uhalifu ambapo walifanya upekuzi na kumkuta na silaha hiyo kinyume na sheria"

Polisi wamesema bunduki hiyo ilikuwa inatumika kupora fedha kwenye vituo vya mafuta na maduka yanayotoa huduma za miamala ya kifedha.
 
Back
Top Bottom