nashukuru mzima
JF-Expert Member
- Jul 11, 2017
- 1,014
- 1,896
Habari za jioni, tunashukuru Mungu kwa uzima aliotupa.
Katika ulimwengu huu tunaoishi katika dunia ya utandawazi ambayo imeonekana imejitosheleza katika kila sekta, ila kuna taasisi moja kubwa sana ambayo ni Nndoa, taasisi hii inaundwa na mwanamke na mwanaume matokeo ya muda mrefu hadi mfupi uzalisha kiumbe (mtoto).
Ila Tukirudi katika jamii ya sasa imeonekana ndoa nyingi sana zinazofungwa hazidumu kwa muda mrefu sana na hakuna sababu za msingi kwa kuwa kila mtu anajaribu kutoa sababu kwa mitazamo wake anaona ni sahihi maana hadi muda huu hakuna utafiti wa moja kwa moja uliofanyika na ukaleta majibu ya moja kwa moja sababu ya ndoa kuvunjika.
Katika hhapisho hili nitaweka mambo matatu ambayo kama mwanamke akipata ni ngumu sana ndoa yake kudumu kwa muda mrefu.
Jambo la kwanza Elimu
Hili jambo la kwanza inapotokea mwanamke akapata elimu na akashindwa kuitumia basi ni ngumu sana kudumu katika ndoa yake. Elimu ni jambo la msingi sana katika dunia ya sasa pasipo kuzingatia misingi ya kijinsia kama ilivyokuwa inafanyika awali ambapo mwanaume ndio alikuwa anapewa kipaumbele katika hili.
Ila kwa sasa tuna wasomi wengi sana ambayo ni jinsia ya kike lakini inapotokea mahusiano ya ndoa yanahusishwa katika msingi ya Elimu ni ngumu sana kwa jinsia ya kike kuweza kuisimamia, hali ya Kufahamu kila kitu, hali ya kujiona kipekee, hali ya kutaka kuthaminiwa, imewafanya wanawake waweke hali hii katika ndoa zao na kupelekea ndoa nyingi kuvunjika kwa ndoa.
Jambo la pili Cheo/Wadhifa
Mara nyingi inapotokea mwanamke anapopata nafasi katika eneo la kazi au cheo chochote katika masuala ya kisiasa inatokea ugumu sana kuweza kutofautisha majukumu yanayotokea kati ya anapokuwa katika eneo la kutekeleza majukumu ya cheo chake na anapokuwa katika majukumu ya ndoa yake.
Na inapotokea inabainika na kichwa cha familia ambaye ni mwanaume, basi unatokea mtafaruku na hali ya kujiona anajitosheleza katika kila kitu ndipo uonekana hapo. Hivyo husababisha mtafaruku na ndoa kushindwa kudumu.
Jambo la tatu Pesa
Kwa maisha ya sasa kuna umuhimu mkubwa sana wa wanandoa kumiliki pesa na kuwa na uchumi wa uhakika, ila kwa mwanamke hali inakuwa tofauti sana inapotokea ana kipato kikubwa kuliko mumewe.
Ni wanawake wachache wanaweza kuendeleza heshima pindi wanapokuwa vizuri kiuchumi. Mwanamke analomiliki pesa ya kutosha katika kila kitu hali ya kujihisi anajitosheleza inajitokeza na anadhani anaweza kuishi katika hali yoyote ile pasipo na mwanaume yeyote yule, hivyo upelekea kushindwa kumuheshimu mume wake.
Hitimisho
Siyo muafaka ya kuwa wanawake wakiwa na hivi vitu hawadumu kwa ndoa, ila kwa asilimia kubwa inakuwa hivi.
Niwatakie majukumu mema ya kazi kesho.