Mwanamke ajifungua jiwe!

Mkuu,
Mimi nimesikia kwenye kipindi cha matukio cha Redio Free Afrika asubuhi hii. Nimepatwa na mshtuko baada ya kusikia maana ni ngumu kuamini. Sikuweza kusikia jina la huyo mama ila kama kuna ambaye kasikia atatujuza. Kuhusu picha, siwezi kuzipata maana sikuwepo huko na redio haitoi picha. Aliyeripoti redioni amemuhoji huyo mama na m/kiti wa kijiji chake na wote wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo!
umbea huo kaka...........

Mimi sipingi sana kwani nishawahi kumuona mtoto wa hivyo kwenye TV sio hapa TZ ila hiyo channel siikumbuki mana ni siku nyingi niliona hiyo story mwaka 2007. Na madoctor walielezea jinsi inavyotokea na hicho kiumbe hakiwi hai wala hakiendelei kukua na kinaitwa 'Stone Baby'.

Kuna Mama alipata ujauzito kufikia miezi kadhaa ujauzito haukuendelea kukua na baada ya hapo hakupata tena mimba. Ndio kuja kufanyiwa upasuaji na kumtoa huyo anayeitwa stone baby. Yeye alikuwa na umbo la binadamu unakiona kichwa na mwili ila viungo havionekani vizuri kwa kuwa hakuendelea kukua na amekuwa kitu kigumu kama jiwe.

Kutokana na Dr. aliyemfanyia upasuaji na akimuonyesha huyo mtoto alisema ni aina fulani ya fibre, na kile kiumbe kinaweza kukaa tumboni muda mrefu bila madhara kwa mama.

ona sasa kumbe inawezekana, waafrika sisi mawazo yetu yamekaa kishirikina tu halafu huko kanda ya ziwa wakikatana mapanga kisa macho mekundu, tunajidai kuwashangaa, tunasahau kumbe nasisi tunawaza ushirikina everytime!

Amejifungua kwa njia gani?naamini angejifungulia hospitali ya mkoa au rufaa angepewa scientific explanation na asingeenda radioni na hiyo story.
'Stone baby' kwa kitaalamu huitwa lithopedion/lithopedia hutokea kwa baadhi ya wanawake mara baada ya mimba iliyotungwa awali kuharibika na kufunikwa na calcified tissue.mimba hii huweza kukaa tumboni mwa mwanamke na akaendelea kupata mimba nyingine za kawaida bila matatizo.clinical officer,medical attendant lazima akose maelezo akiona kitu kama hiki!

umbea huo kaka...........

Mkuu,
Kama kutoa habari ni umbea basi vyombo vyote vya habari ni wambea!? Kama huna cha kuchangia ni bora ukajisomea na kupita kuliko kuandika upuuzi!

in medicine tuna kitu kinaitwa teratoma, ambayo inaweza kukontein any tissue hata bone tissue. ossified tissue ni ngumu kama jiwe

Dunia hii haiishi maajabu na vituko na huko kwenye vijiji vyetu ndio kabisa, jiwe linatoka hivi hivi unaliona, huruma

Back
Top Bottom