OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
Wanabodi.
Mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela.
Kijana huyo Abubakari Kikulu mbali na kupiga picha hiyo Lema pamoja na Nassari, kijana huyo alionyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.
Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawadhi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro alimhukumu kifungo cha miaka minne jela, ili iwe fundisho.
My Take...
Chadema mmesababisha kijana wa watu kaenda jela ni jukumu lenu kuitunza familia yake pamoja na kusomesha watoto wake.
Kwanza ni kusahihishe ameenda jela miaka miwili amepatikana na makosa mawili na kila kosa ni miaka miwili na adhabu zinakwenda pamoja hivo atakaa jela miaka miwili na sio minne!Nikirudi kwenye mada yako chadema wamesababishaje? Ndio walimtuma ajifanye mwanajeshi kumbe sio? Kwanza ulitakiwa uipongeze chadema kwani umaarufu wake umesababisha mhalifu kujulikana na kufikishwa kwa pilato! chadema hata siku moja hailei wala kufumbia macho waovu na wahalifu angekuwa ameeonewa chadema ingeingilia lakini aliposomewa mashitaka amekubali hapo hapo akala mvua zake mbili! na natarajia hata police aliyegombea ujumbe wa nec ccm pia afikishwe mahamani ili kuwe na fair ground!