'Mwanajeshi' aliyepiga picha na Lema afungwa jela miaka minne

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,889
32,289
599784_464571190273470_1016292069_n.jpg

430928_109903545848532_1614025018_n.jpg
9709_209331452537196_801742473_n.jpg


406583_209331985870476_1524064033_n.jpg


MTU aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela.

Abubakari Kikulu (29), alipiga picha na mbunge huyo Desemba 23 mwaka jana, baada ya Lema kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara eneo la Mererani, ikiwa ni sehemu ya mikutano aliyoifanya kutokana na Mahakama ya Rufani Tanzania kumrejeshea ubunge wake.

Mbali na kupiga picha hiyo na Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, kijana huyo alionekana katika picha hiyo akionyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.

Hata hivyo, baada ya picha hiyo, JWTZ lilimtilia shaka kijana huyo na kutangaza rasmi kumsaka, ili lijiridhishe kama ni mmoja wa wanajeshi wake.

Baada ya kumsaka kwa takriban siku 12, kijana huyo alikamatwa Januari 13, katika Mji wa Bomang'ombe wilayani Hai na baada ya kupekuliwa alikutwa na sare hizo.

Jana, Kikulu alifikishwa mahakamani mjini Moshi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kusomewa mashtaka mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya kama ilivyodaiwa mahakamani.

Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, alimhukumu kifungo cha miaka minne jela, ili iwe fundisho wa wakosaji wengine wa aina hiyo.

Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alimsomea mshtakiwa huyo mashitaka yake mawili, likiwamo la kujifanya Ofisa wa Jeshi, wakati akijua ni uongo.

Wakili huyo alidai mahakamani kuwa Januari 3, mwaka huu katika eneo la Bomang'ombe wilayani Hai, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama mtumishi wa umma.

Katika shtaka la pili, wakili huyo alidai siku hiyo hiyo katika Mtaa wa Msikitini, eneo hilo la Bomang'ombe, mtuhumiwa alipatikana na sare za JWTZ kinyume cha sheria.

Sare hizo ni pamoja na suruali moja, mashati mawili na kofia mbili, vyote vikiwa na alama za Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya Hakimu Kobelo kumuuliza mshtakiwa kama ni kweli alitenda makosa anayoshitakiwa, mshtakiwa huyo alikiri makosa yake katika hali ambayo haikutarajiwa.

Kutokana na kukiri kwake makosa hayo, Hakimu Kobelo alimhukumu kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kwanza la kujifanya Ofisa wa JWTZ na miaka mingine miwili kwa kosa la pili.

Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema kuwa kwa kuwa adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja (concurrent), mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, kosa alilolifanya mtuhumiwa huyo ni baya na linastahili adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya sare za majeshi nchini.

Chanzo: Mwananchi - Januari 12, 2013

My Take...

Chadema mmesababisha kijana wa watu kaenda jela ni jukumu lenu kuitunza familia yake pamoja na kusomesha watoto wake.
 
Wanabodi.

Mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela.

My Take....

Chadema mmesababisha kijana wa watu kaenda jela ni jukumu lenu kuitunza familia yake pamoja na kusomesha watoto wake.

Hahahaha jamani wewe jamaa unatatizo gani?
Hivi ccm inahusika na gharama za kesi ya lema au wanachama ndiyo watalipa?
 
Umeitoa wap hiyo habar!?
Kifungu kip cha sheria kimehusika kumfunga!?
Chadema hawakumlazimisha kupiga picha, ilikuwa ni hial na utash wake kama m2 mzima mwenye akil timamu.!

Kwa hiyo utaki kukubali kuwa mwanajeshi wa Chadema kaenda jela miaka minne.
 
Wanabodi.

Mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela.

My Take....

Chadema mmesababisha kijana wa watu kaenda jela ni jukumu lenu kuitunza familia yake pamoja na kusomesha watoto wake.


Acha mambo ya ajabu mkuu na ''my take'' yako hiyo. ni wapi katika katiba ya nchi imeandikwa mwanajeshi asipige picha na raia?????????????????????? Chadema ndiyo walimvisha magwanda nyumbani kwake?????????? Waliyovaa kiraia na kwenda kumteka Ulimboka waliitunza familia yake???????????

acheni nasema.
 
na yule polisi aliyeenda kugombea dodoma akakamatwa, kafungwa miaka mingapi?

True this is double standard....kabisa...,Yule Askari Polisi alifanya Kosa kubwa kuliko Hilo la aliyevaa sare....kwa mazingira ya vijijini kuna vijana wengi ambao walikuwa na ndoto ya kuwa wana jeshi na hawakufanikiwa...wanavaa sare za Ndugu Zao wastaafu...elimu inahitajika.

Sasa Watu wataanza Kuhoji Askari wanaofanya siasa....Kama wenyeviti wa Kamati za siasa

Watu wataendelea Kuhoji kwanini viongozi wa CCM wanashirikishwa kwenye vikao Vya kupendekeza vijana wa kuajiriwa jeshi,Polisi ,usalama etc..kuanzia mitaani hadi wilayani....eti lengo kuhakikisha vijana wapinzani au wa wazazi wapinzani hawaingii kwenye vyombo Vya usalama...

Nadhani pamoja na ukweli wa Kosa la kijana ....tujiandae Watu kuanza Kuhoji haya....na haipendezi jeshi letu la ulinzi likaingizwa kwenye siasa Kama Polisi
 
Ritz; Nakuona kama unacheka vile............. zomba; Rejao; thatha; hebu chekeni kwa pamoja tuwaone............!


Ritz; Umesema CDM imemsababishia kijana wa watu kifungo??????
Kwa kweli unanichekesha tumia akili wewe mtumwa feki,,,,haya mambo ya familia na watoto kwenda shule ni mambo ya kawaida na utaona mwenyewe na utashaangaa na magamba wako.



Wanabodi.

Mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela.

My Take....

Chadema mmesababisha kijana wa watu kaenda jela ni jukumu lenu kuitunza familia yake pamoja na kusomesha watoto wake.
 
Last edited by a moderator:
Acha mambo ya ajabu mkuu na ''my take'' yako hiyo. ni wapi katika katiba ya nchi imeandikwa mwanajeshi asipige picha na raia?????????????????????? Chadema ndiyo walimvisha magwanda nyumbani kwake?????????? Waliyovaa kiraia na kwenda kumteka Ulimboka waliitunza familia yake???????????

acheni nasema.

Mkuu huyo siyo mwanajeshi ni muhuni tu wa Chadema ambaye alivalishwa na Lema sare za Jeshi nakupiga naye picha kulichafua jeshi letu kujiingiza kwenye siasa.
 
hii kesi mbona imewahi sana kutolewa hukumu, yaan kukamatwa wiki iliyopita na hukumu wiki hii.
Aisee hii haijawahi tokea Tanzania,ingekuwa hv na kwa Mafisadi mbona ingekuwa raha sana.
 
Kwa shitaka/kosa gani? manake sidhani kupoz na Lema pekee ni tatizo mwanajeshi kupoz na mwananchi wake ambaye ndiye mwajiri wake kuna tatizo gani? kwani kashikwa na kadi ya chama? labda kama ishu ni kwamba sio mjeshi kiukweli lakini katinga mijigwanda.
 
Wanajeshi wangapi wanapiga picha na wabunge wa ccm hawafungwi kama sio uonevu nin?i
 
Back
Top Bottom