DOKEZO Mwanafunzi wa darasa la 6 adaiwa kubakwa na watu watatu; abeba mimba. Polisi wadaiwa kuhaha kuficha ukweli

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nianze kwa kukupa ‘intro’ ya stori kabla sijakushushia mkeka kamili, ipo hivi hapa mtaani kwetu kuna mtoto wa kike wa Shule ya Msingi Barracks, Dar es Salaam, amefanyiwa ukatili kwa kubakwa na watu watatu katika nyakati tatu tofauti.

Hapa ninavyoandika mistari hii huyo binti haendi shule tena kutokana na kuwa amepata ujauzito, hasomi tena kwa ufupi shule ni kama haipo tena kwake na kibaya zaidi kuna watu wenye mamlaka yao ambao wamefikishiwa hiyo taarifa lakini wanaficha ukweli wa tukio hilo.

Inaniuma kwa kuwa namuona anavyoteseka kila siku kwa yale anayopitia ndio maana nimeamua niweke jambo hili wazi jamii ijue kinachoendelea.

Vitisho vinaendelea kwa mtoto, baba mtoto ambaye ni Askari Polisi wa Kituo cha Kilwa Road pamoja na familia yake kwa jumla.

Unaweza kujiuliza inakuwaje mtoto wa Askari anafanyiwa ukatili, unafichwa na wahusika kisha waathirika ndio wanakuwa hatarini, kunani nyuma ya pazia? Hapo ndipo filamu inapoanzia.

Nakushushia stori kamili
Baba wa mtoto ni Askari mwenye cheo cha ‘constable’, hiki ni cheoz cha chini, jamaa huyo na familia yake tunaishinao katika nyumba za kota za Polisi, Kurasini.

Mtoto ambaye ni mwathirika (jina lake nalihifadhi kwa sasa, lakini linaanziwa na H), ni Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Barracks iliyopo Kurasini, anaishi na baba yake, mama wa kufikia na wadogo zake wengine.

Mazingira ya kazi ya baba mtu ni kutoka asubuhi na kurudi usiku, hali ambayo ilisababisha akose muda wa kukaa na mwanaye, wakati mwingine kutokana na mazingira ya kazi alikuwa akisafiri au kuingia ‘shift’ za usiku.

Kuna siku mtu mzima mmoja alitembelea katika familia hiyo, ndipo akagundua kuwa kuna shida kwa mtoto, akakaa kikao na baba mtu lakini hawakufanikiwa kumshawishi binti kuzungumza chochote.

Ikabidi watu kadhaa washirikishwe ili kumshawishi mtoto kuzungumza, ndipo akakubali na kuweka wazi.

Mtoto aelezea alivyobakwa
Mtoto akafunguka kuwa kabla baba yake hajamleta mama wa kufikia, muda mwingi walikuwa wakiishi na dada wa kazi na watoto wengine.

Anaeleza mara ya kwanza alibakwa na Mjomba wake alipokuwa anatoka kuoga, mbakaji ambaye alifika nyumbani hapo kutembea akamtishia kuwa akisema atamfanya kitu kibaya. Binti akanyamaza.

Tukio la pili alibakwa na Mtoto wa Askari ambaye mama yake ni Assistant Inspector yupo kituo kimoja na baba mtoto.

Tatu alibakwa na mtu mwingine ambaye ni Askari Polisi. Matukio hayo yametokea Mwaka 2022.

Watuhumiwa wanaswa
Ikafunguliwa kesi Polisi, watuhumiwa wote watatu wakakamatwa, ambao ni 1. Daniel Huruma Kisanga (Askari Polisi), 2. Richard Msuya na 3. Emmanuel Gervas Ntandu.

Mambo yaanza kuwa magumu
Baada ya Mtoto wa Askari kuwekwa ndani, mama mtu akaanza kufanya juu chini ili mwanaye asiende jela, akatumia cheo chake kuanza kumkandamiza Askari ambaye ni baba wa mwathirika kwa kuwa anamzidi cheo.

Mambo yakawa magumu, baba mtu akawa anazidiwa nguvu kwa kuwa yule Askari ambaye ni bosi wake akaanza kupeleka mambo kienyeji na kimyakimya ili sakata liishe.

Kuna wakati Polisi wakaanza kumchukua mtoto na kumfanyia mahojiano bila uwepo wa baba Mtoto au ndugu mwingine yeyote.

Stori yafika kwa Waziri Gwajima
Ndugu wa Mtoto aliyeathirika wakafikisha ripoti kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima, alipoelezwa akatoa maelekezo kuwa wamuone mfu fulani ili awasaidie, mtu huyo yupo Manispaa.

Taarifa ilivyofika kwa mtu husika kwa maelekezo ya Waziri Gwajima kuwa aonwe, ndipo taarifa ikafika hadi kwa RPC wa Temeke.

Ikabidi hilo ‘file’ lihamishwe kutoka Kilwa Road kwenda Chang’ombe Polisi, mtoto akaenda kuhojiwa upya, wakati huo wale watuhumiwa wote wameshatoka ndani kwa dhamana.

Baba mtu naye akahojiwa pia lakini baada ya hapo ukafuata ukimya, hakukuwa na mwendelezo wowote kutoka kwenye mamlaka.

Vitisho kila kona
Baadaye Askari (baba mtoto) akapata safari ya kikazi akapelekwa karibu na mpakani lakini akiwa tayari ameanza kupokea vitisho kadhaa kuhusu suala hilo.

Huku nyuma, baadhi ya majirani wakaanza kuona kuna mienendo ambayo si mizuri, inatishia usalama wa mtoto, ikidaiwa kuwa amenusurika kubakwa kwa mara nyingine.

Kumbuka kuwa mtoto mwathirika alikuwa darasa la 6 wakati anatendewa ukatili na sasa haendi tena shule.

Licha ya Mtoto kuwatambua watuhumiwa wote na kueleza kila kitu alichofanyiwa, lakini watuhumiwa wapo nje na wanadai kuwa wanasubiri mtoto ajifungue ili vifanyie vipimo vya DNA.

Hali ilivyo nyumbani kwa mtoto
Mtoto anaendelea kulea ujauzito, anaishi na mama wa kufikia wote wakiwa wajawazito ujauzito, lakini usalama wa mtoto upo shakani zaidi kwa kuwa licha ya mamlaka kufanya uchunguzi hakuna mwendelezo wowote, vitisho vimekuwa vingi na hakuna kinachoendelea.

Naomba wanaoweza kumsaidie, sisi majirani zake ndio tunajua ukweli wote na uchungu wa kile famiia hiyo inachopitia hasa kwa mtoto husuka.
 
Huyo binti kwa nini anabakwa bakwa namna hii au kuna nguvu za Giza zinachangia.

Au pengine nyuma panaita au ni laana za baba yake(lipolisi)
 
Nimegundua ndio maana baadhi ya watu wanakuwa magaidi tu.

Ila ninaamini bado serikali italichukulia kwa uzito suala hili kulinda maslani ya mtoto na baba yake.
 
Mngekazia hapo kwa waziri, Nina imani atalisimamia mkizidi kumfuata.
 
Asa wakifungwa siwatamkosesha mtoto haki yake ya kulelewa na wazazi wote wawili ila swaumu Kal
Wangapi wanapeana mimba kwa makubaliano na kuridhiana na hawatoi malezi kwa watoto wao? Kumbaka mtu, ndio njia ya kujenga familia? Kama wanajali haki, wangembaka mtoto wa shule?
 
Back
Top Bottom