Mwanafunzi auawa kikatili baada ya kubakwa, kuchinjwa shingo na kunyofolewa sehemu nyeti

Ukiangalia tukio la mauaji pale TAG-Bukoba, watuhumiwa wa uchawi Kigoma, Albino wa Kinyerezi nk, mwezi tu uliopita unaona kuwa Tanzania imejaa watu katili na wabaya kama ilivyo sehemu nyingine duniani na huenda tukawa hata zaidi.
Badala ya kuendelea kuimba 'nyimbo za nchi ya amani' ni bora kutafuta kiini cha mambo haya ili kuyakomesha au basi hata kuyapunguza.
 
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu. Familia yake wajaaliwe subira na wauwaji Mungu awalipe hapahapa duniani na siku ya mwisho wapate adhabu kali.

Mwandishi Chachu Ombara umeweka picha zinazotaja jina lake, ulipoandika jina limehifadhiwa una maana gani?

Mkuu kwenye habari ya kwanza nadhani unaona chanzo cha habari,inamaanisha sio mimi niliyeandika habari hiyo.

Pili majina huwa yanafichwa kwasababu mbalimbali maana hii kesi bado kubwa sana na haijathibishwa pasipo shaka kuwa mtuhumiwa ni kweli katenda kosa.Katiwa mbaloni kwa ushahidi wa mazingira na kukutwa chupi yake ina damu lakini haimaanishi kuwa ile damu moja kwa moja ni ya mtoto aliyeuawa.

Haya yote ni kazi za kiupelelezi na wanaotakiwa kutoa taarifa na wapelelezi waliopewa hilo jalada la kufuatilia hilo tukio.
 
nisingependa kusema ila jaamani wanaume si muwabishie hao waganga kweli dudu lako kubwa unamwingizia mtoto kwa nini kutesa mtoto jamani jamani kwani wakubwa tumeisha mpaka mfanyie watoto .... uchungu aliopata huyu mtoto ni mkubwa mno damu yake haitaenda bure ...... nikikamata mwanaume anayebaka namuua

Sio wanaume wote jamani wengine tunasingiziwa au ndio samaki mmoja akioza basi wote wameoza.Dunia ina mambo kua uyaone.
 
Watuhumiwa wamekamatwa tayari, wana umri wa miaka 16 kila mmoja, ila idadi yao bado haijatajwa.
wanasema eti walimuua ili asiweze kusema kwa wazazi wake.

Mwenye taarifa zaidi atujuze.
 
Madame B, sheria inasemaje kuhusu mtu mwenye umri wa miaka 16 kutenda kosa la jinai?
 
Last edited by a moderator:
Unyama sana huu, kumfupisha maisha binti wa watu.

Shirki kitu kibaya sana, utabakaje mtoto?
 
Kweli binaadamu tumekuwa wanyama sana yaani nimeishia kumwaza mtoto wangu wa kike roho imeniuma sana sana jamani oh my good god kwanini unaacha mambo haya yatokee kwa watu wasio na hatia jamani
am dought about your existence kweli unatulinda nakutuacha tuteseke namna hiyo jamani
 
Madame B, sheria inasemaje kuhusu mtu mwenye umri wa miaka 16 kutenda kosa la jinai?

...Kwanza hairuhusiwi kutaja jina lake kwenye vyombo vya habari mpaka uchunguzi utakapokamilika.
Na, endapo atapatikana na hatia basi jina lake litawekwa hadharani, na hukumu ikitolewa hupelekwa jela ya watoto huku akisindikizwa na adhabu ya viboko.
...na endapo kifungo chake kitakuwa kirefu, basi atakapofikisha miaka 18 atahamishiwa jela ya watu wazima.
 
Last edited by a moderator:
Nimetoka stationery wanahadisia mtuhumiwa alokamatwa ni mtoto wa miaka 15. Nimetoka fasta mwili ulivyokuwa unanisisimka.
 
Nimetoka stationery wanahadisia mtuhumiwa alokamatwa ni mtoto wa miaka 15. Nimetoka fasta mwili ulivyokuwa unanisisimka.
Itakuwa wamembambikiza mtoto wa watu, mtoto wa miaka 15 peke yake afanye hayo yote bila ya kuwa na wenzake au wakubwa. Kuna uwezekano mkubwa waliofanya ukatili ni watu wazima wenye akili zao timamu
 
Back
Top Bottom